Envaya

Envaya

Dar es Salaam Flooding Community Survey

How has your daily life been affected by the flooding?

Nimepoteza vitu vingi sana hasa vyombo vya ndani, ambapo itaniwea vigumu kupata vyombo vingine kama nilivyokuwanavyo kabla ya mafuriko kutokea. Hivyo hali hii imeniongezea ugumu wa maisha.
Mfumo mzima wa maisha umepotea, sielewi nianzie wapi kuanza upya maisha nahitaji msaada wa kibinadamu ili niweze kuishi, hali ni mbaya sana tena sana.
Rasilimali zote za kazi(Mbao za kuuza) zimesombwa na maji
kwa sasa sina hakika wa maisha,nina maanisha sina msingi wa kuendesha maisha yangu ya kila siku,mimi nilikuwa na duka la rejareja,kwa bahati mbaya vitu vyote vilipelekwa na maji.
imenirudisha nyuma sana kimaisha,kwa kuwa sina mtaji wa kuendesha biashara zangu,nilikuwa na duka la vyakula vya jumla,nafaka zote ziliharibika kwa mafuriko na nyingi zilipelekwa na maji.
Mafuriko yaliyotokea yamenisababishia kuwa na maisha na magumu, maana nimepoteza vitu vingi sana ambavyo vilivyokuwa vinaniwezesha kusukuma gurudumu la maisha kama kawaida, mfano shughuli yangu kubwa ilikuwa ni kuuza chipsi, mishikaki, nyama ya kuku, mayai lakini kwa bahati mbaya mafuriko haya yamesomba vifaa vyote vya kutengenezea chipsi, zaidi ya hapo vyombo vya ndani kama vile kitanda, radio, godoro, viti, vifaa vya kupikia vilisombwa na mafuriko, sasa hapo nini kimebaki kama siyo kuhangaika tu? Mpaka sasa sijui nitafanya nini ili kuweza kuinuka kiuchumi na kuboresha maisha.
Asilimia tisini ya vyombo au mali zangu zote ziliharibika na nyingine kusombwa na maji, kwa mfano kitanda kimeharibika, godoro na makochi, sahani, sufuria, ndoo za maji vyote vilisombwa na maji.
kukosa ajira na kubaki na madeni ya nguo za wateja , mafundi wangu kukimbia, watoto wa sekondari kushindwa kuendelea na masomo mpaka nitakapopata pesa za kuwanunulia vifaa vya shule, msongo wa mawazo na kupata ugonjwa wa presha ambao sikuwa nao mwanzo ,magonjwa ya mlipuko kwa watoto wangu wadogo ikiwemo maralia.
kupoteza mtaji, mali za gharama kupotea ,kumbukumbu muhimu kupotea, kuharibu bajeti ya familia ya kila siku,kughalimika upya kwa mahitaji ya shule za watoto wangu,ujumla maisha yamerudi nyuma
kukaa mazingira hatarishi nyumba isiyo imara, watoto kurudi nyuma kimasomo, kuanza tena upya maisha kwani inabidi kununuliwe vitu muhimu vya ndani,kulala chini kwenye mikeka ambayo inatusababishia tuumie mbavu
yameniathiri kisaikolojia kufikiria wapi nitaanzia kurudisha maisha yangu ya mwanzo, kuharibu mipangilio ya maisha kwa sababu pesa niliyotenga kwa ajili ya masomo ya watoto wangu imetumika kufanyia mambo mengine muhimu kwa wakati huu.
kuharibu mali zote , nyumba kupata nyufa hivyo kuhitaji ukarabati mkubwa, kuathriri elimu ya watoto wangu kwani hawana kumbukumbu zozote za masomo hasa wa sekondari, lawama kuongezeka ndani ya familia ambapo unasababisha upendo kupungua.
kuleta hasara kwa kupotelewa na vitu vyote pamoja na pesa , watoto mpaka sasa hawajaenda shule, magonjwa ya mlipuko ,maralia inayotokana na maji ambayo mpaka sasa hayajakauka eneo hili. fangasi miguuni ukurutu na kukosa maji na choo kwani naomba kujisaidia kwa jirani yangu
yamenirudisha nyuma kiuchumi na kimaendeleo, kunisababishia madeni kwani mtaji wangu wa biashara ni mkopo wa benki ya akiba na watu binafsi.
Kupoteza mtaji wa duka la kawaida na mbao{ajira}, kunirudisha nyuma kimaendeleo, kuingia gharama upya kwa ajili ya mali za ndani na vifaa vya shule kwa watoto.,kupoteza vyeti vya ndoa na nyaraka nyingine muhimu.kukosa uhakika wa chakula wa kila siku.
nyumba yangu ilizingilwa na maji hivyo kuta kulika na kumong,onyoka, magonjwa kama maralia , homa za matumbo zimesumbua familia yangu , baadhi ya nyaraka muhimu kuharibika kutokana na unyevu nyevu,
kulala nje siku kumi kwani maji yalichukua muda huo kukauka ,kuingia gharama za ujenzi wa ukuta na kuanza maisha upya, kuingia usumbufu wa kufuatilia vyeti upya,gharama za vifaa vya shule kwa watoto na gharama ya vifaa vya kufundishia, kupoteza kumbukumbu za serikari mimi kama mjumbe wa nyumba kumi eneo hili.
kurudisha maendeleo nyuma ,watoto kutokwenda shule ,kukosa sehemu salama ya kuishi ongezeko la magonwa kwa familia malaria , kuhara,na upele .
kukosa sehemu ya kulala, magonjwa ya mlipuko, kurudi nyuma kimaendeleo,ujumla maisha yameharibikana nimerudi kwenye umaskini.,kukosa choo, na maji.
yamesababisha nikose ajira , sehemu salama ya kulala,magonjwa kwa watoto wadogo waliokuwa wanachezea maji machafu,kukosa choo ,kukosa uelekeo wa maisha na watoto wangu kuathirika kimasomo,kwani wamechelewa kuanza shule kwa kukosa vifaa muhimu vya shule.
« Previous questionNext question »

« Back to report