Envaya

Envaya

Dar es Salaam Flooding Community Survey

How has your daily life been affected by the flooding?

Mahali pa kuishi ni tabu kutokana na mahali pa kuishi kuharibika kabisa.
vyombo , kama magodoro , vyombo vya kuhifadhia maji safi, na vitanda vyote vimepotea
familia hizi hazina vitu kwa ajili ya matumizi ya ndani na ya kila siku.
Haya mafuriko yamekuwa ni janga, maana mpaka dakika hii nimebaki mdomo wazi maana naona ni bora na mimi maji yangenichukua nikafa tu, maana sina maana tena kuishi, karibu kila kitu nilichokuwa nacho kimepotea, nimebaki tu na nguo ambazo nilikuwa nimevaa wakati wa mafuriko yanatokea, sasa sijui nitaishije ukizingatia maisha ya Dar Es Salaam yalivyo magumu.
Kwa ujumla mafuriko haya yameongeza sana kiwango cha umasikini katika maisha yangu, maana mali zangu zote zimepotea, hata pesa ambazo nilikuwa nazo zipatazo laki tano ziliweza kuchukuliwa na maji, maana siku ile mafuriko yanatokea pesa hizo nilikuwa nimeziweka kwenye kabati ya meza ambapo nilikuwa nimepanga kuzitumia siku inayofuata kwa ajili ya kununulia biashara yangu huko kariakoo, lakini kwa bahati mbaya zimetwaliwa na maji, sasa sijui nitafanya nini.
miundombinu imeharibika,miundombinu hiyo ni kama mifereji ya maji machafu,njia imeharibiwa na mafuriko na kufanya usumbufu mkubwa kwa kwetu sisi wakazi wa kigogo kati.
The feeder roads were destroyed and the only bridge we use as an outlet from our area was washed away hence hindering our travel to our daily work places
Yamenirudisha nyuma sana.Kwanza biashara yangu imekufa kwasababu sina tena mtaji,watoto hawaendi shule maana sina pesa tena.
Nilikuwa nafanya biashara ya kushona nguo ila sahivi nimestisha kwasababu sina wateja na pia akili yangu bado haijatulia kutokana na haya mafuriko.Kwahiyo napata shida sana kupata pesa ya kujikimu katika kuendesha maisha yangu.
maisha yamekuwa magumu kupita maelezo na hatujui hatma yetu
« Previous questionNext question »

« Back to report