Respondent: | Counselling and Family Life Organization (CAFLO) |
---|---|
Time Submitted: | February 2, 2012 at 2:08 PM EAT |
Msimbazi bondeni-darajani, Vingunguti.
Mtaa huu unahitaji barabara nzuri za kupitika, mitalo mikubwa na ya kutosha kwa ajili ya kupitisha maji mengi, pia kwa sasa tunahitaji kupata mabomba ya maji ya matumizi ya kila siku.
Nyumba yote ilifunikwa na maji, hivyo vitu vyote vya ndani na hata vya nje vilifusombwa na maji.
Mafuriko yaliyotokea yamenisababishia kuwa na maisha na magumu, maana nimepoteza vitu vingi sana ambavyo vilivyokuwa vinaniwezesha kusukuma gurudumu la maisha kama kawaida, mfano shughuli yangu kubwa ilikuwa ni kuuza chipsi, mishikaki, nyama ya kuku, mayai lakini kwa bahati mbaya mafuriko haya yamesomba vifaa vyote vya kutengenezea chipsi, zaidi ya hapo vyombo vya ndani kama vile kitanda, radio, godoro, viti, vifaa vya kupikia vilisombwa na mafuriko, sasa hapo nini kimebaki kama siyo kuhangaika tu? Mpaka sasa sijui nitafanya nini ili kuweza kuinuka kiuchumi na kuboresha maisha.
Tangia mwanzo hapa kwetu maji ni ya shida kiasi chake, maana kulikuwa na kisima kimoja tu cha maji, na kisima hicho kimeharibiwa na mafuriko, kinahitaji ukarabati. Hivyo hali ya upatikanaji wa maji siyo nzuri.
Before flooding: Nilikuwa nimejiajiri mwenyewe. | Now: 0 |
(No Response)
« Back to report