Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya utawala bora kwa wanafunzi wa shule za Wilaya ya Chamwino yanayoendeshwa na MED kwa uhisani wa Oxfam.
Mgeni rasmi katika mahafali - Chidachi alkimpa mkono wa pongezi mmoja wa wahitibu wa darasa la saba katika shule ya msingi Chidachi.
Mratibu wa Shrika la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) Bw. Davis Makundi (aliye vaa shada) akiwa kwenye mahafali ya nane ya shule ya Msingi Chidachi.
Uendelezaji wa Mji wa Dodoma unaozingatia ujenzi wa nyumba bora za kuishi unafanyika na kuufanya mji wa Dodoma kuwa nadhifu na wa kuvutia, Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA hainabudi kushughulikia suala la miundombinu ya barabara kwa haraka ili kukidhi mahitahi ya wakazi wa mji huu.
Mandhari ya mji wa Dodoma inazidi kubadilishwa kwa kuboreshwa na wawekezaji mbalimbali kama ambavyo eneo hili la Independence Square linavyoonekana baada ya uboreshwaji uliofanywa na Benki ya Biashara ya Akiba (ACB.
Tatizo la maji katika Mtaa wa Chidachi Manispaa ya Dodoma linawafanya wakazi wa eneo hilo kutumia zaidi ya saa 5 kwa siku kwa ajili ya kutafuta maji.
USALAMA KAZINI UZINGATIWE Na MED Media Unit.
Suala la usalama kazi ni lisipopewa kipaumbele tunaweza kujikuta tukipoteza nguvukazi kutokana na uzembe wa kutokufuata taratibu za usalama wa wafanyakazi. Mpiga picha wa MED amekutana na hali hii ya kutishia maisha ya wafanyakazi ambao kampuni husika haijajulikana wakiendelea na kazi katika jengo la ghorofa la Mackay House ambao wanatumia vitendeakazi duni katika kazi hiyo.
Wafanyakazi wanne wote wanaume wanafanya kazi ya kuwangua rangi ya zamani katika jengo hilo kwa kutumia ngazi za mbao na wao bila kuvaa mikanda maalum itumikayo kwa ajili ya kujizuia endapo itatokea hatari ya kuteleza.
Picha na Marafiki wa Elimu Dodoma.
Kitaifa
Waliofeli kidato cha nne waula, ufaulu sasa waongezeka
Share bookmark Print Email Rating
Na Fredy Azzah, Mwananchi (email the author)
Posted Jumapili,Mei26 2013 saa 18:59 PM
Kwa ufupi
- Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
SHARE THIS STORY
Dar es Salaam. Idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani wa kidato cha nne mwaka jana imeongezeka kwa kati ya asilimia 20 na 23 baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), kufanya marekebisho alama za viwango vya ufaulu, Mwananchi limebaini.
Habari ambazo gazeti hili imezipata zinasema matokeo hayo ambayo yamewezesha kiwango cha ufaulu kupanda na kufikia asilimia kati ya 54 na 57, huenda yakatangazwa wiki hii pamoja na yale ya kidato cha sita ambayo pia yamechelewa kutangazwa.
Chanzo cha habari kutoka Necta kimesema matokeo hayo mapya yanaonyesha kuwa, ufaulu wa kuanzia daraja la kwanza hadi la nne umeongezeka kutoka asilimia 34.5 kwa matokeo yaliyotangazwa awali na huenda yakafikia asilimia 57. Hii inamaanisha kwamba watahiniwa wapatao 82,000 ambao awali walikuwa wamepata sifuri katika matokeo ya awali sasa wamepanda na kupata madaraja ya ufaulu katika matokeo mapya.
Kwa matokeo hayo, watahiniwa wa mwaka 2012 watakuwa wamefanya vizuri kuliko wa mwaka 2011, ambao watahiniwa 225,126 sawa na asilimia 53.37 ya 349,390 waliofanya mtihani huo walifaulu.
Msemaji wa Necta, John Nchimbi alisema upangaji wa matokeo hayo ulikuwa bado unaendelea. “Ninachojua kwa sasa ni kuwa mchakato unaendelea na matokeo yatatangazwa mapema tu ili watoto waweze kujiunga na shule mapema,” alisema Nchimbi.
Pia alisema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha sita umekamilika.
Matokeo ya awali
Matokeo ya awali yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa yalionyesha kuwa kati ya watahiniwa 367,756 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana, waliokuwa wamefaulu kwa daraja la kwanza mpaka la tatu walikuwa 126,847 sawa na asilimia 6.4. Waliopata daraja la nne walikuwa ni 103,327 sawa na asilimia 28.1.
Katika matokeo hayo, watahiniwa 240,909 sawa na asilimia 65.5 walipata sifuri, hesabu ambayo imebadilika katika matokeo mapya ambayo yanaonyesha kuwa sasa waliopata daraja hilo ni 158,100 ambayo ni asilimia 43.
Hata hivyo, habari kutoka Necta zinasema kuwa licha ya kuwezesha kuongezeka kwa waliofaulu, matumizi ya kanuni mpya ya kukokotoa matokeo hayo yalisababisha zaidi ya wanafunzi 2,500 kushuka ufaulu ikilinganishwa na awali.
Maofisa mbalimbali wa Necta pamoja na wale wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake, walikutana mwishoni mwa wiki iliyopita kukubaliana masuala mbalimbali juu ya matokeo hayo pamoja na suala la matokeo ya wanafunzi hao 2,500 kabla ya kutangazwa wiki hii.
“Baada ya wajumbe kujadili suala lile, busara ilibidi itumike kwa hiyo hakuna mwanafunzi ambaye alama yake itashuka, kwa kawaida isingewezekana mtoto ambaye matokeo yalitoka akiwa amefaulu leo umwambie ameshuka,” kilieleza chanzo chetu.
Chanzo Mwananchi Mei 27, 2013
WASICHANA NA CHANGAMOTO KATIKA MABARAZA YA WANAFUNZI
Ikionekana kama ilishazoeleka ya kuwa viongozi wengi wanaopaswa kuongoza kundi au vikundi vya watu ni lazima awe mwanaume na hivvyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuendelea na ile dhana ya mfumo dume katika jamii zetu.
Hili limeanza kuwa tofauti na mazoea hayo yanayoonekana kama kupitwa na wakati hasa kwa kile kinachoonekana kama ni mapinduzi ya amani na yenye changamoto ya kuleta mabadiliko hayo kuanza kuchukua nafasi kuanzia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo mashuleni.
Katika hali isiyo ya kawaida katika shule nyingi za msingi katika Wilaya ya Chamwino zimekuwa na mabaraza mengi ya wanafunzi ambayo kwa sasa yanaongozwa na wasichana nahii imeonyesha kuwa kwa sasa mapinduzi makubwa ya kuondoa ile dhana ya mfumo dume huenda ikapotea kabisa na kuwa na usawa pasipo na ubaguzi.
Hizo ni moja ya juhudi za Shirika lisilo la kiserikali la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) linalotekeleza mradi wa Haki Zangu Sauti Yangu chini ya ufadhili wa Shirika la kimataifa la Oxfam GB tawi la Tanzania,katika Shule 20 zikiwemo 16 za Msingi na 4 za Sekondari.
Aidha awali ya yote wakati wa kuendesha mafunzo yake katika shule hizo kuna baadhi ya wadau walionyesha wasiwasi wao katika kudhani ya kuwa elimu hiyo ingeweza kuwa na matokeo tofauti ya uelewa wa kudai haki zao kama wanafunzi kwa kuwa na usumbufu kwa baadhi ya wanafunzi na walimu wao jambo ambalo limeonekana kuwa tofauti na lenye msaada mkubwa kwa walimu wenyewe.
“mwanzo nilikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya haya mafunzo kwani niliamini kuwa ni kama tunaanza kuwajengea chuki wanafunzi dhidi ya walimu wao pindi watakaposhindwa kuelewa kile wanachofundishwa, lakini imekuwa tofauti na ni msaada mkubwa sana kwa sisi walimu kwani kwa sasa kazi nyingi zinafanywa na wanafunzi wenyewe’, alisema Mwalimu Hamisa Chama.anae fundisha shule ya Msingi Chalula iliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Akiongea na maofisa wa MED mwanafunzi Given Mbaigwa wa Shule ya Msingi Mkapa iliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma alisema ya kuwa mwanzo alikuwa na woga wa kutaka kugombea nafasi hiyo lakini alijipa moyo na kuamua
WAKETI KWENYE UDONGO DARASANI KWA UHABA WA MADAWATI
Wanafunzi katika shule ya msingi Chalula iliyopo Mvumi Makulu Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wanakabiliwa na uhaba wa madawati na kusababisha kuketi chini huku baadhi ya madarasa yakiwa hayana sakafu.
Hayo yalibainika hivi karibuni wakati wa ziara iliyofanywa na shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) ambapo lengo lilikuwa kufuatilia mradi wa ‘Haki zangu Sauti yangu’ unaotekelezwa katika shule 20 zikiwemo shule 16 za Msingi na 4 za Sekondari zilizopo wilaya ya chamwino pamoja na ufuatilaji wa matumizi ya maendeleo ya vitabu walivyotoa msaada katika shule hizo.
Kwa mujibu wa Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Amina Mohamed, hali ya madawati katika shule hiyo ni mbaya kwani imefikia hatua wanafunzi wa darasa la tatu kuketi chini kwenye udongo kutokana na darasa kutokuwa na sakafu na kuwepo kwa msongamano wa wanafunzi 150 katika darasa moja.
Licha ya kuishukuru MED kwa kutoa msaada wa vitabu 1015 vya kiingereza, Hisabati na Atlasi katika shule hiyo, mwalimu huyo alisema kuwa mahitaji ya vitabu bado ni makubwa. Changamoto nyingine katika shule hiyo ni hali mbaya ya uchakavu wa majengo yasiyo na milango.
Tatizo la upungufu wa madawati imewakumba pia wanafunzi wa shule ya Msingi Mvumi Makulu kutokana idadi ya madawati 100 waliyo nayo kati ya madawati 407 yanayohitajika.
Mwalimu mkuu wa Shule hiyo, Mary Mabichi alisema wanakabiliwa na upungufu wa madawati 307 na vyumba vya madarasa ni vidogo hali inayosababisha wanafunzi kuketi kwa kusongamana. Alisema kuwa walijitahidi kushirikisha jamii ili kuweza kupunguza ukubwa wa tatizo hilo na waliweza kuchangia madawati 40.
Mabichi alisema wanafunzi wengi wanakaa wakiwa wamesongamana na madawati hayo yako katika madarasa mawili kati ya saba yaliyopo ambapo dawati moja hukaliwa na wanaafunzi watatu hadi wanne.
Alisema kuwa darasa la sita na saba huketi kwenye madawati huku madarasa yaliyobaki wanafunzi wanakaa chini. Pia alisema wanafunzi wa chekechea wamepewa madawati 10 ili wasione taabu kuja shuleni kwani wakati mwingine kukaa chini kunasababisha baadhi ya wanafunzi kuchukia shule.shule hiyo ilipokea jumla ya vitabu 1036 kutoka shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma.(MED)