Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

 

WAKETI KWENYE UDONGO DARASANI KWA UHABA WA MADAWATI

Wanafunzi katika shule ya msingi Chalula iliyopo Mvumi Makulu Wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma wanakabiliwa na uhaba wa madawati na kusababisha kuketi chini huku baadhi ya madarasa yakiwa hayana sakafu.

Hayo yalibainika hivi karibuni wakati wa ziara iliyofanywa na shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) ambapo lengo  lilikuwa kufuatilia mradi wa ‘Haki zangu Sauti yangu’ unaotekelezwa katika shule 20 zikiwemo shule 16 za  Msingi na 4 za Sekondari zilizopo  wilaya ya chamwino pamoja na ufuatilaji wa matumizi ya maendeleo ya vitabu walivyotoa msaada katika shule hizo.

Kwa mujibu wa Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Amina Mohamed, hali ya madawati katika shule hiyo ni mbaya kwani imefikia hatua wanafunzi wa darasa la tatu kuketi chini kwenye udongo kutokana na darasa kutokuwa na sakafu na kuwepo kwa msongamano wa wanafunzi 150 katika darasa moja.

Licha ya kuishukuru MED kwa kutoa msaada wa vitabu 1015 vya kiingereza, Hisabati na Atlasi katika shule hiyo, mwalimu huyo alisema kuwa mahitaji ya vitabu bado ni makubwa. Changamoto nyingine katika shule hiyo ni hali mbaya ya uchakavu wa majengo yasiyo na milango.

Tatizo la upungufu wa madawati imewakumba pia wanafunzi wa shule ya Msingi Mvumi Makulu kutokana idadi ya  madawati 100 waliyo nayo kati ya madawati 407 yanayohitajika.

Mwalimu mkuu wa Shule hiyo, Mary Mabichi alisema wanakabiliwa na upungufu wa madawati 307 na vyumba vya madarasa ni vidogo hali inayosababisha wanafunzi kuketi kwa kusongamana. Alisema kuwa walijitahidi kushirikisha jamii ili kuweza kupunguza ukubwa wa tatizo hilo na waliweza kuchangia madawati 40.

Mabichi alisema wanafunzi wengi wanakaa wakiwa wamesongamana na madawati hayo yako katika madarasa mawili kati ya saba yaliyopo ambapo dawati moja hukaliwa na wanaafunzi watatu hadi wanne.

Alisema kuwa darasa la sita na saba huketi kwenye madawati huku madarasa yaliyobaki wanafunzi wanakaa chini. Pia alisema wanafunzi wa chekechea wamepewa madawati 10 ili wasione taabu kuja shuleni kwani wakati mwingine kukaa chini kunasababisha baadhi ya wanafunzi kuchukia shule.shule hiyo ilipokea jumla ya vitabu 1036 kutoka shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma.(MED)

18 Werurwe, 2013
« Inyuma Ahakurikira »

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.