Log in
Marafiki wa Elimu Dodoma (MED)

Marafiki wa Elimu Dodoma (MED)

Dodoma, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Ukurasa huu unakujuza mambo mengi ambayo ama unayafahamu au huyafahamu. Si vibaya kama unayafahamu ukajikumbusha na kama huyafahamu ukayafahamu na kwenda kuwajuza wengine. Karibu saaaaaaaana Mdau!!!

 Hii ni Ofisi ya Walimu katika shule ya Msingi Mzula Wilayani Chamwino. Je wajua kwamba hapa ndipo wanakokaa Walimu na kufikiria namna ya kuboresha taaluma katika shule yao? Jiulize kama ofisi iko hivi, madarasa, madawati na vitendea kazi vingine vikoje? 


Licha ya kuwepo kwa Mkataba wa Haki za watu wenye Ulemavu; Idadi kubwa ya watu wenye ulemavu  bado kundi kubwa la wahusika hawajafikiwa na taarifa sahihi juu ya uwepo wa Mkataba huo.

 

Hivi unafahamu kwamba kati ya shule 10 zilizofanya vibaya katika mtihani wa Taifa wa kidato cha nne 2010; shule tano kati ya hizo zimetoka Dodoma?  Shule hizo ni Changaa, Kolo, Kikore, Hurui na Thawi. Haijalishi zinatoka Wilaya gani ila ni za Dodoma; Tufanye nini kuepuka aibu hii mwakani?

  • Shule ya Sekondari Changaa ambayo ni miongoni mwa shule 5 za Sekondari zilizofanya vibaya zaidi Kitaifa katika Mtihani wa Kidato cha nne 2010; hivi sasa ina jumla ya wanafunzi watatu tu (3) wa kidato cha nne ambapo wasichana ni wawili na mvulana mmoja tu? 

Haikuwa kazi ndogo kufika Changaa; hapa Power tiller inakoma. Ilitulazimu kushuka kwenye gani na kutembea kwa miguu ili kupunguza uzito kwenye gari.

  • Katika ziara yangu kwenye shule ya Changaaa tarehe 4/04/2011 nilifika shule hiapo ambapo nilifanikiwa kuonana na mwanafunzi mmoja wa shule hiyo aliyekuwa ambaye ni miongoni mwa wanafunzi watatu wa kidato cha nne (iv) ambaye alihudhuria masomo kwa siku hiyo. Binti hiuyo aliyefahamika kwa jina la Kurwa Martin alisema yeye ataendelea na masomo hadi hapo atakapo hitimu hata kama atabaki peke yake katika darasa hilo.

 Shule ya Sekondari Pahi ina Maabara ila hawajui Funguo ziliko?

Unaweza usiamini ila hiyo ni hali halisi tuliyo ikuta kwenye Shule ya Sekondari ya Pahi iliyoko Wilayani Kondoa. Katika hali ya mshangao; walimu wote wa shule hiyo hawakuwa na funguo za Maabara hiyo licha ya kujinadi kuwa wana maabara inayotumika na wanafunzi wa shule hiyo.Hiki ni chumba cha maabara kama kinavyoonekana ambacho licha ya kukosekana kwa funguo zake; niliamua kupiga picha kwa kuchungulia dirishani na kufanikiwa. Ama kweli shule za kata zina mambo na vijambo; kama baabara hii inatumika kama tulivyo fahamishwa na walimu wa shule hiyo; kulikoni suala la kupata funguo liwe gumu kiasi cha kutuchukua zaidi ya dk 27 kusubiri na zisipatikane? Kuna jambo hapa! tulifanyie kazi!!                                                

Dodoma   bahari?            Na. Fullgence Makundi

Mkoa wa Dodoma ni Mkoa ulio katika orodha ya Mikoa ya nyanda kame ambayo hupata mvua zake kidogo sana kwa mwaka. Kutokana na hali hiyo ya hewa katika Mkoa wa Dodoma ndiyo maana wakulima wa Mkoa huu hulima mazao yanayo stahimili ukame kama karanga, mahindi, mtama, alizeti, ufuta mihogo na mazao mengine ambayo hayahitaji kiasi kikubwa cha mvua.Hali hii ya ukame katika mkoa huu inakatisha kabisa matumaini ya wakazi wa Mkoa huo kujihusisha na uwekezaji mkubwa katika Kilimo na kulazimika kujihusisha zaidi mana biashara za aina mbalimbali.
Kutokana na hali ya ukame wakazi wa Dodoma wanalazimika kuchimba visima vifupi vya maji na kuyatumia maji hayo yasiyo safi wala salama kwa shughuli mbalimbali za kila siku kama kufua, kuoshea vyombo, kuogea nk.Dodoma inafurahisha machoni kwa namna ambayo inaonekana kaika kipindi cha kiangazi. Adha pekee ambayo ni kero kwa wananchi wa Dodoma ni hali yake ya hewa ambapo joto kali inaloambatana na upepo mkali.