MIAKA SABA SHULE HAINA MWALIMU WA HESABU
Wakati serikali ikiwa imeunda tume ya kuchunguza chanzo cha matokeo mabaya ya kidato cha nne kwa mwaka 2012, zipo sababu nyingi zinazoonyesha dalili za awali za majibu yatakayoletwa na tume hiyo mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi wake.
Hivi karibuni yalitangazwa matokeo ya watahiniwa wa kidato cha nne kwa mwaka wa masomo wa 2012 na kuonyesha ya kuwa 60.1% ya wanafunzi waliofanyamtihani huo walishindwa kufikia vigezo vya kuendelea na masomo. Hali hiyo ilionekama kama kuishitua jamii na wadau wa Elimu nchini.
Pamoja na kuwa na walimu wengi waliopo vyuoni na hata wale walipangiwa vituo vya kazi shule ya sekondari ya Buigiri iliyopo katika Wilaya ya Chamwino haijawahi kupangiwa mwalimu wa hesabu kwa mika saba sasa. Hali hii imesababisha kuwepo na mwenendo wa kusuasua katika somo hilo, kwani imelazimika kwa shule kuajili walimu wa muda wa kuweza kutoa msaada wa Huduma hiyo kwa wanafunzi wake.
Akiongea na Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) katika ofisi yake Makamu Mkuu wa shule ya Buigiri sekondari Mwl. Razalo Njamasi alisema ya kuwa tatizo la kutokuwa na mwalimu wa hesabu katika shule yake ni la muda mrefu ambalo mpaka sasa hawajapangiwa mwalimu wa hesabu katika shule hiyo, ‘Tunalazimika kutafuta mwalimu wa muda kwa ajili ya kusaidia watoto wetu lakini serikali kama serikali haijawahi kutupangia mwalimu wa hesabu na tuna mwaka wa saba sasa tangu shule hii imeanza kufundisha’, alisema mwalimu Njamasi.
Aidha tatizo la kutokuwa na mwalimu wa somo hilo linalounganisha masomo ya sayansi limeonekana kama kuwa ni janga kwa wilaya ya Chamwino limeikumba pia Shule ya sekondari ya Chamwino ambayo yenyewe ina mwalimu mmoja tu wa hesabu ambaye hutoa huduma hiyo kwa zaidiya wanafunzi 472, hayo yalibainishwa na Mkuu wa shule hiyo Bwana Fedinand Komba alipokuwa akitoa taarifa fupi juu ya maendeleo ya Mradi wa Haki zangu Sauti yangu mradi unaoendeshwa na Shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma kwa ufadhili wa shirika la kimataifa la Oxfam GB ya Uingereza tawi la Tanzania.
Bwana Komba alibainisha kuwa kwa kawaida mwalimu hupaswa kuwa na vipindi 40 kwa muhula lakini kutokana na tatizo la uhaba wa walimu analazimika kuwa na vipindi visivyopungua 60 kwa muhula, kitu ambacho kinamfanya hata yeye mwalimu mwenyewe kushindwa kuwamudu wanafunzi wote kwa wakati,’badala ya kufundisha vipindi 40 mwalimu huyu analazimika kufundisha vipindi zaidi ya 60 kwa muhula kitu ambacho inakuwa si rahisi kwa mwalimu huyu kuwamudu wanafunzi kwa wakati’, alisema mwl. Komba.
Lakini pia pamoja na hayo yote katika shule nyingi kumeonekana kuna changamoto ya kutokuwa na walimu wa masomo ya sayansi kama vile katika masomo ya Chemistry na Physics kitu ambacho kwa mujibu wa baadhi ya walimu walidai inasababishwa na kutokuwa na vifaa vya kufundishia kwa vitendo katika maabara za shule.’walimu wengi wanashindwa kuja kwanza unakuta vifaa vya kufundishia hakuna na kama unavyojua masomo haya mwanafunzi anapaswa kujifunza kwa vitendo zaidi kuliko kusiliza na kuandika tu’, alisema mmoja wa walimu wa Sekondari ya Chamwino.
Kuna haja kwa serikali kukaa na kujipanga upya katika kuhakikisha ya kuwa mgawanyo wa walimu unazingatia na uhitaji wa masomo yanayokuwa hayana kabisa walimu tena kwa kuyapa kipaumbele masomo ya sayansi ambayo mara nyingi ndio huonekana wanafunzi wengi hawafanyi vizuri katika mitihani yao ya mwisho kwenye masomo haya.
Katika utekelezaji wa kweli wa maendeleo ya Tanzania tunahitaji viongozi wachapakazi wenye moyo wa kutumikia wananchi na kukubali ushauri bila kujali nyadhfa zao. Bi.Fatma Said Ally ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino ni miongoni mwa viongozi ambao wanapongezwa na wananchi kutika juhudi zake za kuwa karibu na wananchi,taasisi pamoja na wadau katika Wilaya yake kwa lengo la kuwaletea maendeleo. MED inampongeza kiongozi huyu na kumtakia kila la kheri katika kutimiza azma yake ya kuifanya Wilaya ya Chamwino kuwa Wilaya zenye maendeleo chanya.(Pichani aliye simama ni mkuu wa Wilaya ya Chamwino Bi.Fatma Said Ally,kulia ni Bw. Baltazar Ngowi Afisa utumishi mkuu wa halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na kushoto ni Bw.Davis Makundi mratibu wa shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma.)(MED).
Hili ni jengo la choo cha Shule ya Msingi Ndebwe iliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma choo ambacho wanafunzi hukitumia wawapo shuleni hapo.
Hili ni moja ya tundu la choo hicho kinachotumiwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Ndebwe Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Kiranja Mkuu wa Shule ya Msingi Ndebwe Iliopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma,Rossemary Masaka. Haya ni moja ya mafanikio ya mradi wa HAKI ZANGU SAUTI YANGU,mradi ambao umeleta mapinduzi katika chaguzi mashuleni Wilayani Chamwino tofauti na zamani ambapo walimu ndio walikuwa wakiteuwa viongozi,jambo ambalo lilikuwa likiwanyima haki wanafunzi kuchagua viongozi wanaowataka. Hapa wanafunzi wa Shule ya Msingi Ndebwe walitumia Demokrasia kuchagua vingozi katika shule yao bila kujali jinsia.
Wanafunzi kutoka shule za msingi za,Mvumi misheni,Mvumi co,ed,Nyerere,Ilolo,Ndebwe,Mvumi makulu,,Chalula na Muungano. Wakifuatilia mafunzo juu ya chaguzi za Demokrasia na uundwaji wa mabaraza mashuleni,kutoka kwa maafisa wa shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma hawako pichani,ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa HAKI ZANGU SAUTI YANGU unaoendeshwa na shirika hili katika shule 14 za msingi na 6 za sekondari zilizopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma,mradi ambao unafadhiliwa na OXFA GB.
Shirika la Marafiki wa Elimu Mkoani Dodoma pia hutumia vyombo vya habari kutoa Elimu kwa jamii kuhusiana,Elimu,Demokrasia na Utawala bora,kama inavyoonekana kwenye picha.
Mratibu wa shirika la Marafiki wa Elimu Dodoma,nd.Davis Makundi akiendesha mafunzo ya chaguzi za Demokrasia na uundwaji wa mabaraza katika shule 16 za msingi na 4 ZA sekondari zilzopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma,ikiwa ni moja ya utekelezaji wa mradi wa HAKI ZANGU SAUTI YANGU unaoendeshwa na shirika hili kupitia ufadhili wa OXFAM GB.
UJIRA WA WALIMU UZINGATIE MAZINGIRA WANAYOPANGIWA
Imekuwa ni kama kawaida kusikia ya kuwa wapo walimu wengi wanaoshindwa kulipoti kwaenye vituo vya kazi kutokana na sababu mbalimbali ikwemo ugumu wa mazingira ya kufanyia kazi, vitendea kazi na hata uhakika wa maslai yao kuwafikia kwa wakati.
Hayo yamezungumzwa na wadau wa elimu mkoani Dodoma wakati wakiwa kwenye shughuli za ugawaji wa msaada wa vitabu katika wilaya ya chamwino mkoani humo. Akiongea na mratibu wa shirka lisilo la kiserikali la marafiki wa elimu mkoani Dodoma Mwl Abinery Malogo wa shule ya msingi Wiliko alisema wamekuwa wakipata shida sana hasa pale wanapojikuta asilimia zaidi ya 25% ya mishahara yao inatumika katika nauli katika kipindi kinapofika cha kwenda kuchukua mishahara yao. Aidha mwl malogo alilalamikia pia kuona walimu waliopo mijini waapewa kiwanngo sawa na wale wanaoishi vijijini.
(Moja kati ya ofisi ya walimu kama inavyoonekana katika shule ya msingi Mzula iliyopo wilayani Chamwino)
kitu ambacho amedai kuwa hali hiyo imekuwa ni tatizo kubwa na linaloonekana kama ni uonevu kwani kwa wao kukubali kutumikia maeneo ya vijijini.
Hakika kama walimu waliopo vijijini wangekwa wanapatiwa kiwango kikubwa tofauti na wanachopewa sasa hakika walimu wengi wengi ambao wamekuwa wakipangiwa katika maeneo ya vijijini wangekuwa wanaripoti kwa wakati na kufanya kazi kwa moyo mmoja na kuwa na uhakika wa kuwa na maisha bora na ya mfano kwa wote wanaopenda kuwa walimu.
Mbali na ugumu wa mazingira pia baadhi ya vitu vilivyoonyesha kuhatarisha maisha ya wlimu hao ni pamoja na uchakavu wa majengo, kama vile ofisi za walimu,vyoo kutokuwa na madarasa ya kutosha kitu kinachowalazimu baadhi ya wanafunzi kufundishiwa sehemu zisizo kidhi matakwa yao, pia ukosefu wa madawati ya kukalia wanafunzi imeonekana ni kikwazo katika maeneo mengi wilayani humo. Mbali na ukosefu wa madawati lakini pia wapo wanafunzi wanaosomea chini ya miti kitu ambacho kinaonekana kama ni hadithi za kale, lakini ukweli ndivyo ulivyo kwenye maeneo mengi ya vijijini mkoani Dodoma.