WASICHANA NA CHANGAMOTO KATIKA MABARAZA YA WANAFUNZI
Ikionekana kama ilishazoeleka ya kuwa viongozi wengi wanaopaswa kuongoza kundi au vikundi vya watu ni lazima awe mwanaume na hivvyo kuchangia kwa kiasi kikubwa kuendelea na ile dhana ya mfumo dume katika jamii zetu.
Hili limeanza kuwa tofauti na mazoea hayo yanayoonekana kama kupitwa na wakati hasa kwa kile kinachoonekana kama ni mapinduzi ya amani na yenye changamoto ya kuleta mabadiliko hayo kuanza kuchukua nafasi kuanzia katika Nyanja mbalimbali zikiwemo mashuleni.
Katika hali isiyo ya kawaida katika shule nyingi za msingi katika Wilaya ya Chamwino zimekuwa na mabaraza mengi ya wanafunzi ambayo kwa sasa yanaongozwa na wasichana nahii imeonyesha kuwa kwa sasa mapinduzi makubwa ya kuondoa ile dhana ya mfumo dume huenda ikapotea kabisa na kuwa na usawa pasipo na ubaguzi.
Hizo ni moja ya juhudi za Shirika lisilo la kiserikali la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) linalotekeleza mradi wa Haki Zangu Sauti Yangu chini ya ufadhili wa Shirika la kimataifa la Oxfam GB tawi la Tanzania,katika Shule 20 zikiwemo 16 za Msingi na 4 za Sekondari.
Aidha awali ya yote wakati wa kuendesha mafunzo yake katika shule hizo kuna baadhi ya wadau walionyesha wasiwasi wao katika kudhani ya kuwa elimu hiyo ingeweza kuwa na matokeo tofauti ya uelewa wa kudai haki zao kama wanafunzi kwa kuwa na usumbufu kwa baadhi ya wanafunzi na walimu wao jambo ambalo limeonekana kuwa tofauti na lenye msaada mkubwa kwa walimu wenyewe.
“mwanzo nilikuwa na wasiwasi mkubwa juu ya haya mafunzo kwani niliamini kuwa ni kama tunaanza kuwajengea chuki wanafunzi dhidi ya walimu wao pindi watakaposhindwa kuelewa kile wanachofundishwa, lakini imekuwa tofauti na ni msaada mkubwa sana kwa sisi walimu kwani kwa sasa kazi nyingi zinafanywa na wanafunzi wenyewe’, alisema Mwalimu Hamisa Chama.anae fundisha shule ya Msingi Chalula iliyopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.
Akiongea na maofisa wa MED mwanafunzi Given Mbaigwa wa Shule ya Msingi Mkapa iliyopo wilayani Chamwino Mkoani Dodoma alisema ya kuwa mwanzo alikuwa na woga wa kutaka kugombea nafasi hiyo lakini alijipa moyo na kuamua