Log in
Marafiki wa Elimu Dodoma (MED)

Marafiki wa Elimu Dodoma (MED)

Dodoma, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

MED ni kifupisho cha Maneno Marafiki wa Elimu Dodoma. MED ilianzishwa mwaka 2009 kama kikundi kidogo cha wanachama wa programu ya Harakati za Marafiki wa Elimu inayoendeshwa na shirika la HakiElimu.

Kufuatia maendeleo mazuri ya shughuli za Marafiki wa Elimu chini ya uwezeshwaji wa HakiElimu; Marafiki wa Elimu Dodoma waliamua kwa kauli moja kuanzisha asasi ya wanaharakati ambayo itaendeleza shughuli za uana harakati na wakati huo huo kuendesha shughuli zao kama Asasi Huru ambayo inaweza kuomba usajili na kusajiliwa kwa mujibu wa sheria ya NGO Na. 24 ya mwaka 2002. Hadi sasa (2011) MED ina jumla ya wanachama zaidi ya 157 Mkoani Dodoma.