Vyanzo na ubora wa maji kwenu yamepata athari gani kutokana na mafuriko?
Kwa wastani hali ya maji siyo nzuri, wakazi wa mtaa huu tunategemea zaidi maji ya visima, na kipindi cha mafuriko visima hivi viliweza kuharibika, hivyo hali ya upatikanaji wa maji ni ngumu.
Mabomba hayatoi maji, maji tunayotumia ni machafu sana, kutoka kwenye visima na mabwawa yaliyosimama katika maeneo haya.
Mabomba yote ya maji yamesombwa na mafuriko na kwa sasa tunatumia maji ya visima ambayo si salama kwa matumizi ya binadamu
vimeharibiwa kwa asilimia kuwa,na kwa utafiti mdogo niliofanya hapa mtaani,wakazi wengi tunaumwa taifodi,nafikiri hii ni kutokana na maji kutokuwa salama.
vimehariwa kwa sana na mafuriko haya ya mwaka jana
Tangia mwanzo hapa kwetu maji ni ya shida kiasi chake, maana kulikuwa na kisima kimoja tu cha maji, na kisima hicho kimeharibiwa na mafuriko, kinahitaji ukarabati. Hivyo hali ya upatikanaji wa maji siyo nzuri.
Kwa sasa vyanzo vya maji si vya uhakika, kutokana na kwamba visima vingi viliharibiwa na mafuriko.
Maji hakuna kabisa bomba letu lilisombwa na mafuriko, maji ya kisima si salama baada ya muingiliano wa maji taka
kubomoka kwa vyoo kumesababisha uharibufu wa maji safi.Hivyo tunahitaji tupatiwe huduma upya ya maji .
Mpaka sasa maji kwa ujumla hakuna tokea siku yalipotokea mafuriko
vyanzo vya maji inabidi kuanza upya ,kwa kutandika mabomba ,na kujenga visima na kurekebisha mitaro ili visije kuharibiwa tena
Kwa kweli vyanzo vya maji vimeharibika na mafuriko hivyo msaada wa maji ni muhimu sana kwetu
toka mafuriko yatokee eneo hili hatuna tena maji safi kwani mabomba mengi yalisombwa na maji na mengine kupasuka ,visima kuchanganyika na maji ya vyoo,hivyo maji ni shida sana
eneo hili kwa sasa halina maji kutokana na mafuriko tunachota au kununua kutoka eneo la kizuiani ambalo liko mbali kidogo na eneo hili
maji kwa eneo hili hakuna kabisa kutokana na mafuriko, visima kuharibika na mabomba yalipasuka
kwangu nina bomba ambalo halikupata madhara isipokuwa majirani zangu vyoo na ,visima vilibomoka hivyo maji safi na taka kuchanganyika
Hatuna kabisa maji maeneo haya mabomba yalipasuka wakati wa nvua ,visima kwa maji ya kawaida havifai tena
tumekosa maji kabisa kwani wakati wa mafuriko mabomba yalichimbuliwa na maji hivyo kupasuka kwa kukanyagwa na magari.
visima vya maeneo haya vimebomoka hivyo kuchandanyikana na maji taka.
maji yetu ni ya visima kutokana na kubomoka kwa vyoo na wananchi wengine kutapisha vyoo vyao wakati wa mafuriko kumesababisha maji yasiwe salama.
« Rudi nyuma kwenye ripoti