How did the flooding affect your own property and possessions?
Vyombo vyangu mfano sahani, sufuria, redio, vikombe, vijiko vilisombwa na maji, Magodoro, TV, kabati, vitanda vyote viliharibiwa na maji, vile vile nyumba niliyokuwa nimepanga ilibomoka upande mmoja.
Vitu vyote vya lazima kwa maisha ya mwanadamu, vimechukuliwa na maji
Vyombo vyote vya ndani vimesombwa na maji, mfano magodoro, nguo, vyakula, sare za watoto wa shule.
sina hata kitu kimoja katika nyumba yangu,samani zote na vitu vyote vimepelekwa na maji,
mafuriko yamwahiribu nyumba imekuwa na nyufa nyingi.vifaa vya ndani vimeharibika,sina hata kilichosalimika.
Nyumba yote ilifunikwa na maji, hivyo vitu vyote vya ndani na hata vya nje vilifusombwa na maji.
Nyumba niliyokuwa nimepanga iliharibika sana baadhi ya vyumba vilibomoka, vyombo vya ndani vilisombwa na mafuriko, hata baadhi ya mifugo kama vile kuku, bata ilipotea.
choo changu kimeanguka, nyumba imepata nyufa ,vitu vyote vya ndani vimeharibika , magodoro, vitanda , kabati la vyombo, redio nguo cherehani 3 na mahine ya kudarizi, nguo za wateja na vifaa vyote vya ushonaji viliharibika ,na vifaa vya shule vya watoto wangu.
Mali zote za familia yangu zimepotea nakuharibika, Vitanda ,sofa set mbili, redio ,tv ,jokofu, jiko la umeme, mifugo, {kuku wa kisasa elfu mbili} 2,000 vifaa vyote vya mradi wa kuku taa za chemri,chakula na ,madawa, ungo wa tv uliibiwa , vifaa vya shule ,kopyuta ,taptop na ,simu vilipotea . .
Ukuta wa nyumba yangu ulibomoka na kuta nyingine kubaki na vyufa , vitu vyote vya ndani kasoro redio iliyokuwa kwa fundi vyote vimeharibika ,magodoro makabati jokofu, kopyuta , vitanda ,viti vifaa vya shule pamoja na sare za watoto vimepotea msingi na sekondari.
Vyombo vya ndani vimeharibiwa na maji, friji, tv, deki, simu , redio ,vitanda ,magodoro, kabati,nguo za familia nzima ,sare na vifaa vya shule ,milango na mabati yaliibiwa tulipokimbia nyumba na kutafuta hifadhi
nyumba yangu imepata nyufa, mali zote za ndani zimeharibika ,vifaa vya watoto wangu wa shule vimeharibka , kumbukumbu muhimu zote zimeharibika, naomba nipatiwe eneo lingine kwa usalama wangu na familia yangu
vyombo vyote vya ndani viliharibika ,viti,vitanda, magodoro, kabati, jokofu, redio, tv vifaa vya watoto wa shule na pesa zilizokuwa kwenye kibubu takribaini laki moja na nusu{150,000}zilipotea
biashara ya mkaa wenye thamani ya milion moja na laki mbili {1,200,000}ulipotea, pesa za mauzo ya siku mbili laki tatu {300,000}zilipotea {mfanya biashara wa mkaa eneo hili}
Mali zote za ndani ya nyumba yangu ziliharibika, biashara yangu ya mbao iliathrbiwa na maji [mbao kuvimba} vifaa vya ujenzi ,sementi imaharibika ,na vifaa vya duka langu vilibiwa na vibaka wakati wa mafuriko,
ni mifugo tu iliyopotea kutokana na mafuriko vitu vingine viko salama ,,mbuzi kondoo , kanga kuku, na bata
kuvunjika kwa ukuta wa nyumba yangu, vifaa vyote vya ndani kuharibika na kupotea,Tv,radio friji, komputa,vifaa vya shule vya kufundishia, vifaa vya shule watoto wangu ,vyeti vya shule na vya kuzaliwa watoto viliharibiwa na maji
nyumba yangu ilizingilwa na maji hivyo iko hatarini kubomoka, samani zote za ndani zimeharibika,nguo na vifaa vyote vya shule vimeharibika
mali zote za ndani zimeharibika,kabati ,vifaa vya jikoni, vitanda,magodoro, tv ,radio,na kuta za nyumba kubomoka, choo,kisima cha maji vyote vimebomoka
Mali zote za ndani zilipotea kasoro nguo tu,Tv.radio, kabati 2 , magodoro,vitanda ,vyombo vya jikoni, vyombo vyote vya mamalishe{ biashara ya chakula}sare na vifaa vyote vya watoto wa shule
« Back to report