Envaya

Envaya

Dar es Salaam Flooding Community Survey

What is your neighborhood's most important need right now?

Usafi wa mazingira ikiwa ni pamoja na kusafisha mifereji pamoja na kuchimba mifereji mikubwa ya maji.
Ujenzi wa makazi mapya ya kudumu, kurudishwa kwa mabomba ya maji.
Miundo mbinu na huduma za jamii kwa ujumla.
1.msaasda wa vyakula
2.magodoro
3.mavazi kwa jamii,wengi wetu tumepoteza samani zetu za ndani kwa asilimia 100
4.mavazi kwa watoto wetu hususani uniform za watoto wa shule
5.wakazi wengi wetu tumepoteza mitaji yetu kwa ajili ya mafuriko
kitu kinachohitajika na mtaa wetu kwa sasa ni
1. kusaidia wajasiliamali wadogowadogo mitaji kwa ajili ya kuweza kuendesha biashara zao zilizoharibiwa vibaya na mafuriko
2.tupatiwe misaada uniform kwa ajili ya wanafunzi wetu
3.tunahitaji maji kwa matumizi ya kila siku
4.njia au barabara ziboreshwe.
Mtaa huu unahitaji barabara nzuri za kupitika, mitalo mikubwa na ya kutosha kwa ajili ya kupitisha maji mengi, pia kwa sasa tunahitaji kupata mabomba ya maji ya matumizi ya kila siku.
Kwanza kabisa mtaa huu kwa sasa ni mchafu sana, hivyo usafi wa mazingira unahitajika sana, pili watu wa hapa wanahitaji sana kupata elimu ya afya na utunzaji wa mazingira, maana wakazi wengi wa hapa wanadhani kuwa suala la kusafisha mazingia ni jukumu la serikali.
kuhamishwa moja kwa moja tupelekwe sehemu nyingine yenye usalama isiyojaa maji,kabla ya kuhamishwa tupatiwe madawa ya kupuliza na vyandarua tujikinge na maralia pamoja na mongwa ya mlipuko.
Kujengewa mifereji na mitaro thabiti inayoruhusu maji kutiririka kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa urahisi , kiwanda cha KTM kifungue mifereji yake ili maji yafuate njia yake , kudhibiwe magonjwa ya mlipuko.kwa kusaidiwa madawa.
Kuboreshewa mfereji kutoka bara bara ya kilwa hadi mto kizinga, tujengwe mitaro itakayo ruhusu maji kupita bila kutuama katikati ya nyumba zetu, tupatiwe dawa za kuua wadudu katika eneo hili na vyandarua ili kudhibiti maralia .
Tupate mchanga,kokoto, mawe na kifusi cha kutosha ili tupate muinuko kwenye eneo hili, kuzibuliwe njia za maji chini ya daraja ambalo limeziba njia ya maji na kisababisha maji kukosa njia yake na kukimbilia maeneo ya makazi yetu
Tunahitaji kifusi kitakachoinua eneo hili , kokoto na mawe ya kutenganisha mto na maeneo ya nyumba zetu, kujengwe mitaro thabiti itakayoelekeza maji kutoka maeneo ya juu mpaka mto kizinga.
Tukarabatiwe nyumba zetu zilizoharibika wakati na mafuriko, tuboreshewe mitaro nyumba hadi nyumba, zijengwe njia za maji kutoka barabara ya kilwa na kuelekezwa mto kizinga badala ya kuelekezwa kwenye majumba yetu
kujengwe mitaro na mifereji ambayo itawezesha au itakayoelekeza maji kupita kwa urahisi kuelekea mto kizinga ,
kumwagwe kifusi kiinue eneo hili ambalo lilididimia kutokana na ujenzi wa barabara ya kilwa ;kuzibuliwe njia ya maji darajani iliyozibwa na ujenzi wa barabara kuu ili njia zote mbili zipitishe maji, mitaro ya nyumba hadi nyumba ijenjwe ili maji yasituame
kimwagwe kifusi ili kilete muinuko kutokana na eneo hili kuathiriwa na ujenzi wa barabara kuu ya kilwa, mitaro midogo ijengwe nyumba hadi nyumba ili kurusu maji kutiririka na kuelekea mto kizinga
kifusi cha kuinua maeneo yetu, mitaro midogo ijengwe ili kuruhusu maji kuingia mto mzinga, Kiwanda cha KTM kuzibue njia ya maji kilipojenga mifrreji yake ,ikiwezekana tutafutiwe maeneo ya kuishi ili tutoke mabondeni
miundo mbinu ,iboreshwe,hasa katika barabara kuu ya kilwa road ambayo imejengwa vibaya na kuziba mwelekeo wa maji,kupatikane vifusi ili kuinua maeneo yaliyoathiriwa na maji
tunahitaji msaada wa kukausha
maji ambayo mpaka sasa bado yametuama katika maeneo yetu, kutengenezewa mitaro midogo midogo itakayoruhusu maji kupita kwa urahisi, vyandaruail kuzuia mbu, dawa za kusafishia mazingira yetu ili kuua wadudu .,kukarabatiwa nyumba zetu na visima.
Tejengewe mitaro kwa mpangilio itakayoruhusu maji kutiririka kwa urahisi wakati mvua zikinyesha ,tupewe madawa ya kufanyia usafi mazingira ambayo bado maji hayajakauka na kuhifadhi wadudu,
« Previous questionNext question »

« Back to report