Interview 7
1.Unaishi eneo gani?!
Magulumbasi 'B'
2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!
- Mfereji mkubwa unaotoka barabara kubwa ya Nyerere mpaka bahari ya hindi utengenezwe ili kuruhusu maji kupita wa urahisi.
- Kivunjwe kiwanda cha mwenye kampuni ya Ruby kilichojengwa sehemu iliyoziba mfereji wa maji.
- Kuzibitiwe taka kwa kuwekwa sehemu maalamu ya kutupwa taka.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?!
Vitu vyangu vyote vya ndani vimechukuliwa na maji,mali zote za duka langu lililokua nyumbani lenye thamani ya zaidi ya Mil 15 kupotea.
Vifaa vyangu kama deep freezer nilivokua natumia kukopesha kwa watu kupotea.
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?!
- Ajira niliyokua nategemea kutokana na duka langu haipo tena baada ya mimi kustaafu.
- Magonjwa ya mlipuko ambayo yamemaliza akiba yangu yote iliyokua imebaki kwa gharama za matibabu kwangu na familia yangu.
5.Vyanzo vya ubora wa maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko?!
Bomba langu limeharibika kipindi cha mvua hivyo sina njia ya kupata tena maji bila gharama ambayo sina uwezo nayo kwa sasa.
6.Kama una kazi,inakuchukua muda gani kutoka nyumbani mpaka eneo lako la kazi?!
Nimestaafu sina kazi.
Interview 6
1.Unaishi eneo gani?!
Keko mwanga 'B'South
2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!
- Nahitaji mifereji iboreshwe kwa kutanuliwa.
- Kubomolewa nyumba zilizojengwa bila mpangilio.
- Kujengwe makaravati yatayowezesha maji kupita kwa urahisi.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?!
Ukuta wa nyumba ulibomoka,vitu vya ndani vyote viliharibika,mashine yangu ya kaz ya welding ilipotea.
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?!
- Nimekosa ajira kwani mashine yangu iliyokua inanipa ajira imepotea.
- kurudi nyumba kimaendeleo maana sina mali yoyote ndani.
5.Vyanzo vya ubora vya maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko?!
Watu walioko kwenye miemuko walizibua vyoo na vingine kuharibiwa na maji,vilisababisha vyanzo vya maji ya kisima kuchanganyika na maji taka,na hivyomaji yanayotumika kutokua salama.
6.Kama una kazi,inakuchukua muda gani kutoka nyumbani mpaka eneo lako la kazi?!
wakati nna kazi ilikua inanichukua dakika 15,kwa sasa sina kazi.
Interview 5
1.Unaishi eneo gani?!
Keko mwanga 'B'
2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!
Kuzibuliwa mitaro,kujengwe mifereji,kuvunjwe kuta zitazozuia maji.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?!
Vitu vyangu havikuharibika,niliwahi kuvihamisha juu ya bati.
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?!
- Uchafu maana maji taka bado yamezingira nyumba yangu.
- Magonjwa kutokana na uchafu uliozingira nyumba.
5.Vyanzo bora vya maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko?!
Kisima changu kimebomoka hivyo inatubidi kuchota maji kwenye maeneo ya miinuko ambayo kwangu ni gharama ambayo siwezi kumudu.
6.Kama una kazi,inachukua muda gani kutoka nyumbani mpaka eneo lako la kazi?!
Sina kazi.
Interview 4
1.Unaishi eneo gani?!
Keko mwanga 'A'
2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!
- Kutengeneza mifereji,kudhibiti na kubomoa watu waliojenga bila mpango maalumu.
- Tuliopo mabondeni tuhamishwe maeneo bora zaidi.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?!
Mali zangu zote za ndani zimepotea,vifaa vya kazi yangu kama mashine ya kuranda zimepotea zenye zaidi ya thamani ya Mil 2 na laki tano.
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?!
- Yameniathiri kiuchumi maana vifaa vyangu vya kazi vimeharibika hivyo siwezi kufanya kazi yangu inayoniingizia hela.
- Magonjwa kama Malaria,kuharisha na tumbo kuumwa kwa mimi na familia yangu.
- Choo changu kuharibika.
5.Vyanzo bora vya maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko?!
Tunakosa maji ya kunywa kutokana na maji yetu ya kisima kuchanganyika na maji taka,hivyo maji tunayotumia si salama kwa matumizi bora kwa afya ya binadamu.
6.Kama una kazi,inakuchukua muda gani kutoka nyumbani mpaka eneo lako la kazi?!
Hainichukui muda wowote maana ofisi yangu ilikua hapohapo nyumbani.
Interview 3
1.Unaishi eneo gani?!
Magulumbasi 'B'
2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!
- Kuvunjwe nyumba ambazo zimejengwa kando ya mtaro,kutengenezwe njia ya maji kutoka keko darajani mpaka bahari ya hindi.
- Kutengenezwe njia ndogo ndogo zitazoweza kupitisha maji kwa urahisi na mitaro izibuliwe mara kwa mara.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?!
Tv na redio ndivyo vimeharibika,vingine niliwahi kuhamisha kutoka ndani ya nyumba.
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye Maisha yako ya kila siku?!
Magonjwa kama Malaria,Kuharisha,kutokana na maji taka mbu hawazuiliki hata kwa matumizi ya chandalua.
5.Vyanzo bora vya maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko?!
Bomba lilipasuka hivyo hatuna kabisa maji ya kutumia,inatubidi kwenda kuchota maji kwenye mabomba ya watu na kutugharimu hela kuyapata maji hayo.
6.Kama una kazi,inakuchukua muda gani kutoka nyumbani kwako mpaka eneo lako la kazi?!
Sina muda maalumu maana biashara yangu ni ya kuzunguka kwa watu na kukopesha bidhaa ninazouza.
Interview 2
1.Unaishi eneo gani?!
Keko Magurumbasi 'A'
2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!
- Kutengenezwe mkondo wa maji kutoka darajani,mpaka kurasini shelly ili kuruhusa njia ya maji kuelekea bahari ya hindi.
- Kuwepo na eneo maalumu la kuweka taka.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?!
Vitu vyote vya ndani vimeharibika,TV,kabati,magodoro na vitanda.
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?!
- Yamenirudisha nyuma kimaendeleo.
- Nimepata magonjwa ya mlipuko
5.Vyanzo vya ubora wa Maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko.?!
Maji tunayotumia yamechanganyika na maji taka.
6.Kama una kazi inakuchukua muda gani kutoka nyumbani kwako mpaka eneo lako la kazi?!
Inanichukua dakika 5 kufika eneo langu la kazi maana nafanya kazi saloon eneo la keko.
Survey ya Athari za Mafuriko,Keko Wilaya ya Temeke.
Yafuatayo ni Maswali na majibu:
1.Unaishi eneo gani
Mtaa wa Magulumbasi 'A'
2.Mtaa wako Unahitaji kitu gani sana sana
Mtaa wangu unahitaji
- Kutengenezewa mirefereji midogo midogo itayoweza kuzunguka nyumba na kupitisha maji kwa urahisi sehemu zote.
- Kutengeneza mipaka itayosaidia kutenganisha nyumba hadi nyumba.
- Kuhamishwa na kutafutiwa maeneo ya kuishi.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba yako na vitu vyako
Vitu vyote vya ndani vilielea juu ya maji na kusombwa na kupotea,bidhaa zangu za biashara(Machinga) nazo pia zilipotea,(nguo za kike na za kiume,urembo)
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku
Baada ya kupoteza mtaji,maisha yameendelea kuwa mabaya maana hata pesa ya kula na kutunza watoto sina.
5.Vyanzo vya ubora wa maji kwenu vimepata athari gani kutokana na mafuriko.
Maji ya kutumia kwa matumizi ya kawaida ya kisima yamechanganyika na maji taka hivyo kuleta athari za magonjwa ya mlipuko hasa kwa watoto.
6.Kama una kazi inachukua muda gani kutoka nyumbani kwako mpaka sehemu yako ya kazi.
Kwa sasa sina kazi baada ya mtaji wangu kupotea,ila wakati bado nna ajira ilikua inanichukua dakika 15 kufika sehemu yangu ya kazi.
5}Vyanzo vya ubora wa maji kwenu yamepata athari gani kutokana na mafuriko?
Athari ni kubwa zinazotokana na mafuriko kwani maji tunayotumia ni ya visima hivyo kutokana na kubomoka kwa vyoo maji tunayotumai siyo salama kwa matumizi ya binadamu .vilevle tuko mabondeni hivyo maji machafu yanayotoka meaneo yaliyo kwenye miinuko na majalala ya kiholela uchanganyikana na maji tunayotumia,Hivyo hatuna jinsi ukizingatia maji ni uhai kwa binadamu tunalazimika kuyatumia wakati tunajua yana mdhara makubwa kwetu kumekuwepo pia ugumu wa upatikanaji wa maji kwani visima vingi vimegeuka kuwa mashimo ya takataka
6}Kama una kazi unachukua muda gani kutoka nyumnani mpaka ofisini?
Ninatumai muda mfupi kufika kazini kwani nafanya biashara ya mama lishe iliyopo karibu na maeneo haya,ni kama dakika 10 tu.
6]Kama una kazi inakuchukua muda gani kufika ofisini
Maswali na majibu ya wahanga wa mafuriko{Mto mzinga Mbagala Mission)
1)Mtaa wako unahitaji kitu gani?
Tunahitaji, maji safi na salama, barabara, mitaro ya kuruhusu maji kupita kwa urahisi kipindi cha mvua
2)Unaishi eneo gani? {Mtaa gani}
Mtaa wa darajani mto mzinga Mission
3}Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?
Mali zangu zote zimepotea ikiwemo ,pesa, nguo magodoro ,vitanda,na vyombo vyote vya ndani.vingine viilchukuliwa na maji wakati vilivyosalia kuchukuliwa na vibaka wakati tulipokimbia ili tusichukuliwe na maji.
mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?
Kupoteza mali, nyumba yagu kubomoka baadhi ya sehemu, kuvuruga mipango yangu ya kiuchumi na mipango ya maendeleo kwani sikuweza kwenda kutafuta pesa wakati nikiwa katika kipindi kigumu cha misukosuko ya mafuriko, na mtaji kupotea .Kwa ujumla nimebaki sina mwelekeo wa kimaisha.
5)Vyanzo vya ubora wa maji ,kwenu yamepata athari gani kutokana na mafuriko|?
kumekuwa na athari kubwa kwenye suala la maji kwani maji tunayotumia ni ya visima hivyo baada ya vyoo kubomoka maji tunatoyumia siyo salama kwa matumizi ya kibinadamu. Na ikizingatiwa umuhimu wa maji kwa binadamu ni uhai hivyo hatuna jinsi ya kufanya
We have been conducting a survey on the areas which affected by floods in which the Tanzania Govement have never reached , such as Mto kizinga Mbagala Mission, Mto Kizinga Mtongani bondeni, Bonde la mpaka wa Mbagala and Yombo Buza , Keko viwandani and others..The mentioned places and others,are places which the media did not visit hence it was visible to access the aids which was given by the Govenment and other stake holders .Following this situation we think there are need of assisting them like other victims from Jangwani , Kigogo, Mbezi and other places. This shows that there are ignorance following the grade or class of the areas cause the Kinondoni and Ilala municipal were visible and coverd by the media which let them being knowm and be assisted ,but for Temeke municipal the situation was worse but no body bothered till to date .