Dar es Salaam Flooding Community Survey
Before flooding: dakika 1 kwani ni eneo la hapa nyumbani | Now: dakika 0 kwani siendi popote nabangaiza hapa nyumbani |
Dar es Salaam Flooding Community Survey
Mfereji mkubwa wa kutoka darajani mpaka barabara ya kilwa shell ya Ruby utengenezwe ili kuruhusu maji kupita kipindi cha mvua
Before flooding: dk 15-20 | Now: siendi kazini kwani mtaji wa matunda umekisha |
Interview 10
1.Unaishi sehemu gani?!
Keko mwanga 'A'
2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!
Kuboresha miundo mbinu,mfano mfereji mkubwa kupanuliwa,mifereji midogo midogo ijengwe itakayotiririsha maji kwenye mfereji mkubwa.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?!
- Vitu vyote vya ndani vimeharibika.
- Nyumba imebomoka ukuta.
- Mifugo kama kuku,bata imekufa baada ya kusombwa na maji.
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?!
- Magonjwa mlipuko kutokana na uchafu wa maji taka kuzingira nyumba yangu.
- Kuishi mazingira hatari baada ya ukuta wa nyumba yangu kubomoka hivyo kulala sehemu hatarishi.
- Nimepoteza rasilimali.
5.Vyanzo vya ubora wa maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko?!
Vyanzo vya maji mtaani kwetu vyote vimeharibika hivyo kukosa upatikanaji wa kira maji safi na salama.
6.Kama una kazi,inakuchukua muda gani kutoka nyumbani mpaka eneo lako la kazi?!
Interview 9
1.Unaishi eneo gani?!
Keko magulumbasi 'A'
2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!
- Sehemu maalumu ya kuweka taka ili uchafu usizibe mifereji ya maji
- Kujengwe mifereji midogo midogo itakayowezesha kupitisha maji nyumba hadi nyumba.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?!
- Nimepoteza vifaa vyangu vya kazi kwa maji,nilikua mama ntilie.
- Vifaa vya ndani vyote kuharibika kama friji,tivi,redio,makochi na nguo zangu na za watoto.
Vifaa vyote vya shule vya watoto kuharibika.
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?!
Sina ajira kutokana na vifaa vyangu vya kazi kupotea.
Watoto kukosa vifaa vya shule,kushindwa kulipa ada kutokana na uchumi wangu kushuka sina ajira.
5.Vyanzo vya ubora wa maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko?!
Kisima cha jirani tulipokua tunachota maji kuharibika,inatulazimu kwenda mbali kutafuta maji ya kununua kwa gharama ambayo sina uwezo nayo.
6.Kama una kazi,inakuchukua muda gani kutoka nyumbani mpaka eneo lako la kazi?!
Wakati nimejiajiri ilikua hainichukui muda wowote maana sehemu ya kazi ilikua nyumbani,sasa sina ajira.
Interview 8
1.Unaishi eneo gani?!
Magulumbasi 'B'
2.Mtaa wako unahitaji kitu gani sana sana?!
- Nyumba zilizoharibika watusaidie kuzirekebisha.
- Tupewe eneo maalumu la kuweka taka zinazoziba mifereji.
- Kuta zinazoziba njia ya maji zibomolewe.
3.Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi nna vitu vyako?!
Vitu vyangu vyote vya ndani vimepotea.
4.Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?!
- Mume wangu amenikimbia kutokana na ugumu wa maisha na majukumu kuongezeka baada ya mafuriko.
- Magonjwa kwa watoto.
- Uchafu umezunguka nyumba kuhatarisha afya ya familia yangu.
5.Vyanzo vya ubora wa maji vimepata athari gani kutokana na mafuriko?!
- Kisima kimeharibika hivyo tunakosa maji ya kutumia.
- kujengwe mifereji itayosaidia kupitisha maji taka kwenye sehem maalumu yasizagae mitaani na kwenye nyumba za watu.
6.Kama una kazi,inakuchukua muda gani kutoka nyumbani mpaka eneo lako la kazi?!
Sina kazi ni mama wa nyumbani.