Mtaa wa One Way maarufu kwa biashara mbalimbali ukiwa kimya kutokana na maduka kufungwa kuhusiana na mgomo wa wafanya biashara.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya utawala bora kwa wanafunzi wa shule za Wilaya ya Chamwino yanayoendeshwa na MED kwa uhisani wa Oxfam.
Mgeni rasmi katika mahafali - Chidachi alkimpa mkono wa pongezi mmoja wa wahitibu wa darasa la saba katika shule ya msingi Chidachi.
Mratibu wa Shrika la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) Bw. Davis Makundi (aliye vaa shada) akiwa kwenye mahafali ya nane ya shule ya Msingi Chidachi.
Uendelezaji wa Mji wa Dodoma unaozingatia ujenzi wa nyumba bora za kuishi unafanyika na kuufanya mji wa Dodoma kuwa nadhifu na wa kuvutia, Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu CDA hainabudi kushughulikia suala la miundombinu ya barabara kwa haraka ili kukidhi mahitahi ya wakazi wa mji huu.
Mandhari ya mji wa Dodoma inazidi kubadilishwa kwa kuboreshwa na wawekezaji mbalimbali kama ambavyo eneo hili la Independence Square linavyoonekana baada ya uboreshwaji uliofanywa na Benki ya Biashara ya Akiba (ACB.
Tatizo la maji katika Mtaa wa Chidachi Manispaa ya Dodoma linawafanya wakazi wa eneo hilo kutumia zaidi ya saa 5 kwa siku kwa ajili ya kutafuta maji.