Envaya

Envaya

Utafiti wa jamii kuhusu hali ya mafuriko jijini Dar-es-salaam

Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?

wakazi wengi wamehama makazi kutokana na nyumba kujaa maji na kuta kuanguka
Baadhi ya familia zimehama makazi hadi sasa hazijarudi kwenye makazi yao ya awali
Familia nyingi hazina vitu vya ndani ka magodoro, vyombo vya kupikia, ndoo za kuhifadhia maji safi na kadhalika
Kwa mimi hapa nimepanga hivyo sina nyumba, lakini ninachokwambia ni kwamba mafuriko haya yameniharibia vifaa vyangu vyote vilivyokuwa ndani kwa mfano, kitanda na godoro vimeondoka, friji, TV, Redio, nguo, viatu, vyombo vya kupikia vimesombwa na maji.
Kwa ujumla mafuriko yameleta maafa makubwa sana katika familia yangu, maana nimepoteza vitu vyote vya ndani mfano vyombo vyote, vitanda, nguo, vilevile hata nyumba yetu imeweza kuharibika kwa kupata nyufa nyingi zinazotokana na kujaa maji mengi.
yameharibu thamani nyingi za ndani,sakafu imebomoka, nyumba imepata nyufa nyingi,
Nyumba iko safi ila vitu vyote vya ndani viliharibiwa kama vile,vitanda,nguo,magodolo na makabati
godoro mbili zimepotea na redio kaseti moja pamoja na vyombo vya ndani
Nimepoteza vyombo vingi sana kama vile,nguo,tv,fridge na mashine ya kushonea
« Swali lililotanguliaSwali lifuatalo »

« Rudi nyuma kwenye ripoti