Respondent: | Counselling and Family Life Organization (CAFLO) |
---|---|
Time Submitted: | 26 Mutarama, 2012 at 06:59 EAT |
Msimbazi bondeni, Kombo, Vingunguti.
Watu wengi wanaoishi eneo hili wameathirika sana na mafuriko haya, siku ile ya mafuriko nyumba nyingi zilijaa maji na kusababisha mali nyingi kuharibika na kupotea, baadhi yetu sasa hatuna sehemu ya kuishi, hivyo nionavyo mimi ni kwamba tupatiwe mahitaji muhimu na ya dharura mfano tupewe malazi mf magodoro, vyakula, nguo, n.k.
Kwa mimi hapa nimepanga hivyo sina nyumba, lakini ninachokwambia ni kwamba mafuriko haya yameniharibia vifaa vyangu vyote vilivyokuwa ndani kwa mfano, kitanda na godoro vimeondoka, friji, TV, Redio, nguo, viatu, vyombo vya kupikia vimesombwa na maji.
Haya mafuriko yamekuwa ni janga, maana mpaka dakika hii nimebaki mdomo wazi maana naona ni bora na mimi maji yangenichukua nikafa tu, maana sina maana tena kuishi, karibu kila kitu nilichokuwa nacho kimepotea, nimebaki tu na nguo ambazo nilikuwa nimevaa wakati wa mafuriko yanatokea, sasa sijui nitaishije ukizingatia maisha ya Dar Es Salaam yalivyo magumu.
Ninachojua ni kwamba visima vya maji tuliyokuwa tunatumia navyo vimeathirika na mafuriko haya, baadhi ya visima vimebomoka, waliokuwa wanamatenki ya maji nayo yamesombwa na mafuriko kwa hiyo hali ya maji ya matumizi ni mbaya, tunaishi kwa neema.
Before flooding: Sina kazi ya kuajiriwa nilikuwa nafanya biashara zangu ndogondogo. | Now: (No Response) |
(No Response)
« Back to report