Envaya

Envaya

Utafiti wa jamii kuhusu hali ya mafuriko jijini Dar-es-salaam

Mafuriko yameleta athari gani kwenye nyumba unayoishi na vitu vyako?

Milango ya nyumba ilivunjika,nyumba kupata ufa na vitu vyake vyote vilienda na maji.hana godolo wala nguo anategemea misaada kutoka kwa watu
Makabati yangu yameharibika,sofa,vitanda na nguo vyote vimeharibika na mafuriko
Makabati/masofa yote yameharibiwa,vitanda pamoja na nguo zote zimeharibiwa
vyumba vitatu vimechukuliwa kabisa na mvua na choo pia
barabara hazipitiki pia madaraja hakuna tunaishi kama ndege
mafuriko yalizoa chumba changu kizima na vitu vyote mazulia pia yalibebwa
nyumba zetu zilikuwa hapa lakini zimebomolewa na mvua na hapa tulikuwa wakazi Kumi katika eneo hili ambalo mafuriko yamezoa kila kitu.Yuko mama mjane mahali hapa kabla ya mvua alikuwa akisaidiwa na sisi lakini wote tumegeuka ombaomba sasa.
Nyumba yangu ya vigae imebomoka na sina fedha za kukarabati
Mh mimi Nyumba yangu imeharibiwa kabisa sina mahali pa kuishi nilikuwa na nyumba ya vigae lakini leo iko kama gofu.
Choo changu kimezolewa na maji na vifaa vya ndani
mafuriko yamevunja ukuta wa nyumba na kuharibu kabisa vitu vyote vya ndani
yaani vitu vyote vimeharibika,magodoro,vyombo,TV,Sina hata mwelekeo yaani tunasaidiwa tu na watu mbalimbali hali ni mbaya
mafuriko yameharibu shule yangu na Library yangu ambayo ilikuwa na vitabu vingi na computers nne
« Swali lililotanguliaSwali lifuatalo »

« Rudi nyuma kwenye ripoti