Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations
Hassan Luheko Mnaute, mwenyekiti wa Organization for Land and Agriculture Improvement Mobile: 0788 715 532 / 0654 269 456, TANDAHIMBA. Ninatoa wito kwa Asasi za kiraia kuwa, tubuni miradi yenye kuleta faida kwa nia ya kujipatia rasilimali fedha ili kusaidia Asasi zetu kuwa na uwezo wa kujiendesha pia kuwa na amasa kwa wafanyakazi wa Asasi, kufanya kazi kwa ufanisi ili Asasi za kiraia ziweze kuyafia malengo. Tukumbuke Asasi nyingi wafanyakazi wake ni wa kujitolea. ENVAYA juu, ninaiombea isonge mbele.

large.jpg

Washiriki wa mdahalo wa siku moja wa kujadili changamoto mbali mbali zinazoikabili sekta ya Ardhi, ulioandaliwa OLAI kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society (FCS) wilayani Tandahimba - Mtwara

IJUE OLAI: Organization for Land and Agriculture Improvement, ni Asasi ya kiraia iliyoasisiwa mwaka 2010 na kupata usajili wake mwaka 2011 katika wizara ya Maendeleo ya jamii, jinsia na watoto na kupata namba ya usajili ooNGO/oooo4476. DIRA YA OLAI: Kuwa na jamii yenye mtazamo angavu kwenye nyanja za Elimu, Afya, Ardhi na kilimo, Mazingira, Utawala bora na Haki za binadamu. DHIMA YA OLAI: Kuiwezesha jamii ya Tandahimba na Tanzania, kuzitambua fursa mbali mbali, kushiriki kwa ufanisi ili kuwawezesha kuyaboresha maisha yao. MAWASILIANO: P.O BOX 62 Tandahimba. Simu: 0788715532 / 0654269456. Tovuti: www.envaya.org/olai. Email: olaitandahimba8@gmail.com

large.jpg

Walemavu nao walishirishwa wakati wa utekelezaji wa mradi wa sheria Na. 5 ya ardhi

Katika muda wa miaka 3 ya 2012 - 2014 na 2015, Asasi ya Organization for Land and Agriculture Improvement (OLAI) imekuwa ikitekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wananchi na wajumbe wa mabaraza ya Ardhi ya vijiji na kata, kuhusu sheria Na. 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999, na kanuni zake za mwaka 2002, kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society (FCS) kwa ruzuku jumla ya Tshs. 51,990,000/= katika kata 7 zenye vijiji 42 katika Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba iliopo mkoani Mtwara - Tanzania. Walengwa wa moja kwa moja ni 550 na wasio wa moja kwa moja ni 43607 ambao ni wakazi wa eneo la mradi. Wakati wa utekelezaji wa mradi, yalishirikishwa makundi mbali mbali wakiwemo vijana, wazee, wanawake na walemavu. Mradi huo umewapelekea wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sheria Na. 5 ya ardhi na kuweza kupata hati ya Haki miliki za mashamba chini ya sheria hiyo.

large.jpg

Hii ni Nembo ya Organization for Land and Agriculture Improvement (OLAI)

large.jpg

Ndg. Hassan Luheko Mnaute, Mwenyekiti wa Organization for Land and Agriculture Improvement (OLAI)

ORGANIZATION FOR LAND AND AGRICULTURE IMPROVEMENT (OLAI) kwa sasa imekuwa mdau mkubwa wa sekta Ardhi kwa kutoa Elimu ya sheria Na. 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999. OLAI akiwa mwanachama wa Haki-Elimu Tanzania, iko katika harakati za kuwasaidia wanafunzi wa shule za sekondari ambao hali ya maisha ni duni, kuchangia kulipa ada kwa mwaka mmoja. Hatua hiyo, inachukuliwa baada ya Olai kutambua kuwa Elimu ni ufunguo wa maisha. Tunaomba Asasi mbalimbali kutuunga mkono jambo hili, ili kuona azma hii ya OLAI inafanikiwa. Mawasiliano:- P.O BOX 62 TANDAHIMBA, Mobile: 0788 715 532 /0654 269 456, Email: olaitandahimba8@gmail.com Tovuti: envaya.org/olai

large.jpg

Kushoto ni mratibu wa mradi Ndg. Hassan Luheko Mnaute, kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya ORGANIZATION FOR LAND AND AGRICULTURE IMPROVEMENT (OLAI) Ndg. Salum Said Mnaguluta.

large.jpg

Kushoto aliekaa ni Mratibu wa mradi Ndg. Hassan Luheko Mnaute, na aliesimama ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Tandahimba Mh. Ally Nalinga Ndingo akifunga mafunzo yaliyoandaliwa na OLAI kwa ufadhili wa The Foundation.