Parts of this page are in Swahili. Edit translations
Katika muda wa miaka 3 ya 2012 - 2014 na 2015, Asasi ya Organization for Land and Agriculture Improvement (OLAI) imekuwa ikitekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wananchi na wajumbe wa mabaraza ya Ardhi ya vijiji na kata, kuhusu sheria Na. 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999, na kanuni zake za mwaka 2002, kwa ufadhili wa The Foundation for Civil Society (FCS) kwa ruzuku jumla ya Tshs. 51,990,000/= katika kata 7 zenye vijiji 42 katika Halmashauri ya wilaya ya Tandahimba iliopo mkoani Mtwara - Tanzania. Walengwa wa moja kwa moja ni 550 na wasio wa moja kwa moja ni 43607 ambao ni wakazi wa eneo la mradi. Wakati wa utekelezaji wa mradi, yalishirikishwa makundi mbali mbali wakiwemo vijana, wazee, wanawake na walemavu. Mradi huo umewapelekea wananchi kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu sheria Na. 5 ya ardhi na kuweza kupata hati ya Haki miliki za mashamba chini ya sheria hiyo.
December 11, 2015
Comments (1)