Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

large.jpg

Kushoto aliekaa ni Mratibu wa mradi Ndg. Hassan Luheko Mnaute, na aliesimama ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Tandahimba Mh. Ally Nalinga Ndingo akifunga mafunzo yaliyoandaliwa na OLAI kwa ufadhili wa The Foundation.

July 31, 2014
« Previous Next »

Comments (2)

HASSAN LUHEKO MNAUTE (CHAUME, TANDAHIMBA, MTWARA~TANZANIA) said:
OLAI pamoja na mambo mengine, tayari imekwisha kufanya savei katika Kata tatu (3) za Lienje, Luagala na Ngunja na kubaini uwapo wa maambukizi mapya ya UKIMWI kutokana na viashiria mbalimbali, ikiwemo ulevi, mmomonyoko wa maadidili. Katika utafiti huo, pia OLAI imegundua kuwa hali ya mbaambukizi hayo, yapo kwa vijana ambao wapo shuleni hasa wale wa Sekondari. Kwa vijana vipo vishawishi kama matumizi ya simu zenye (memory card) na hasa zenye picha za ngono. OLAI hujishughulisha na uhamasishaji kuhusu maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI. Ombi kwa Asasi za kiraia, viongozi wa serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali ya Kitaifa na kimataifa, kutoa ushirikiano kwa OLAI ili kuielimisha jamii kuhusu jambo hili.
September 11, 2014
Hassan Luheko Mnaute, Mwenyekiti mwenyekiti wa Asasi ya OLAI (Kijiji cha Sokoine, Kata ya Chaume, Wilaya ya Tandahimba, Mkoa wa Mtwara - Tanzania.) said:
Organization for Land and Agriculture Improvement (OLAI), imefanya utafiti na kubaini kuwa, kupo kukukosekana kwa Elimu ya mpiga kura. Uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, wilaya ya Tandahimba kulitokea machafuko makubwa na kuleta madhara ambayo yalisababisha watu wengi kuyahama makazi yao. Hii yote ni kwa sababu jamii kukosa Elimu ya mpiga kura. OLAI inatoa wito kwa wadau, kuwa OLAI ina dhamira ya kutoa Elimu ya mpiga kura kuhusu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, na chaguzi zijazo pindi fursa itakaporuhusu. Mashirika yasiyo ya kiserikali, kutoa ushirikiano juu ya hili
September 18, 2015

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.