Mafuriko yameleta athari gani kwenye maisha yako ya kila siku?
Maisha ninayoishi ni kama ya ndege.Leo niko kwa huyu,kesho niko kwa Yule.Sina makazi.
Mafuriko yamenisababishia shinikizo la damu.Naanza maisha upya.Nitakosaje kufikiria?
Kama nilivyokwambia kwamba nadaiwa,nimechanganyikiwa.Naishi kwa kubangaiza.Sina la kukwambia zaidi
B4)Nina watoto wawili ambao wanafanya mtihani mwaka huu.Mmoja yuko kidato cha sita na mwingine kaingia kidato cha nne.Wanalia sana wakidai vifaa vyao vya kusomea walivyotegea vingewasaidia kujiandaa na mtihani vimesombwa na maji.Wameathirika kisaikolojia.Sidhani kama watafanya vizuri katika mitihani yao. Na hata hela ya kuwapeleka tuisheni sina sasa.
Kazi ninayofanya ni ya kibarua.Mshahara wake ni mdogo sana.Sidhani kama nitarudi tena kwenye kiwango cha maisha niliyokuwa nayo.Ni umaskini wa ghafla.
Nafikiria kurudi kijijini maana maisha ya Dar es salaam sitayaweza.Labda nipate mtu wa kunisaidia kodi ya nyumba walau miezi sita na mtaji wa biashara ndogo ndogo nilizokuwa nikifanya.
Ndiyo hivyo naanza maisha upya.Sijui nananzia wapi na elimu yangu ndogo hii.Ningekuwa nimesoma ningetafuta ajira.Biashara zangu za umachinga zimesombwa na maji.
Mmomonyoko huu wa udongo ambao umepanua kingo za mto huu ni tishio kwa makazi yetu.Wadau wa mazingira waangalie namna ya kutusaidia kukabiliana na mmomonyoko huu.
Kama unavyoona nyumba yangu iko kwenye hatari ya kubomoka kama mvua za masika zijazo zitakuwa kubwa.Tunajitahidi kuweka magunia ya michanga kuzuia mmomonyoko wa udongo uliosababishwa na mafuriko usiendelee lakini uwezo sina wa kugharimia kununua kokoto kuudhibiti mmomonyoko kama inavyofanya kampuni ya AMI pale mabibo relini.
Mifugo yangu ambayo niliitegemea kwa kipato imesombwa na maji na mimi ni mstaafu sina shughuli sasa ya kuniingizia kipato.
Vifaa vyangu vya kazi vilichukuliwa pamoja na chumba kilichosombwa na maji.Hali yangu ya kipato ni mbaya.Kazi yangu ni ufundi seremala.Napata kazi lakini nashindwa kuwahudumia wateja kwa sababu ya kukosa vifaa vya kazi.
Kwanza mafuriko hayo yamepoteza vitu vingi vya ndani na vingine vimeharibika, nimepoteza radio, TV, nguo, vyombo vya kupikia na kulia, vitanda na magodolo havifai kwa sasa, vifaa vya shule vya watoto wangu vimeharibika, hivyo mafuriko haya yameleta matatizo makubwa katika maisha yangu, hali imekuwa mbaya, maana sina uhakika kuwa hata watoto wangu watarudi shuleni.
Kwanza kabisa nimepoteza mali nyingi, sasa hali hii imeniathiri kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu mipango ya maisha niliyokuwa nimepanga haitaenda kama ilivyokuwa imepangwa, zaidi nimerudi nyuma sana kimaendeleo, Ila Mungu mkubwa.
Kusema kweli mafuriko haya yamenirudisha nyuma kimaendeleo kutokana na kwamba nimepoteza viti vingi sana kama ambavyo nimeshaeleza. Kwa hiyo kiwango cha umasikini kwa sasa kimeongezeka.
Zaidi ya asilimia 90 ya vitu vyangu vyote vimepotea, pia nimepoteza shilingi laki mbili na nusu ambazo pia zimesombwa na maji. Kwa hiyo mafuriko hayo yameongeza umasikini katika maisha yangu,
Mafuriko haya yameongeza kiwango cha umasikini katika maisha yangu na familia kwa ujumla, maana nimepoteza vitu vingi vya thamani, ambapo sijui kuwa nitapata vitu vingine kama nilivyokuwa navyo kabla ya mafuriko. Pia mwanangu ameshindwa kwenda shule kutokana na kupotelewa na vifaa vya shule, hali hii inarudisha nyuma maendeleo yake kielimu.
Maisha yangu hayana muelekeo na sijui nianzie wapi,
Mafuriko yameathiri sana makazi ya wananchi
kutokana na mafuriko hayo familia nyingi zinaishi nje na wengi wana lala nje
Mahali pa kuishi bado ni kitendawili
« Rudi nyuma kwenye ripoti