Respondent: | Counselling and Family Life Organization (CAFLO) |
---|---|
Time Submitted: | January 27, 2012 at 11:18 PM EAT |
Kombo bondeni, Vingunguti.
Watu wa mtaa huu wanahitaji kupewa elimu ya afya na ya kutunza mazingira, hasa kwa upande wa kuweka mifereji mizuri ya kupitisha ikienda sambamba na kusafisha mifereji hiyo.
Mimi ni mpangaji na nyumba ambayo nilikuwa nimepanga, ilikuwa na jumla ya wapangaji kumi, lakini cha kusikitisha mafuriko haya yameleta maafa makubwa sana, maana mali au vitu mbalimbali vimepotea, kibaya zaidi ndugu wa mpangaji mwenzangu amesombwa na maji na kufariki, hivyo unaona ni kwa jinsi gani ambavyo mafuriko yameathiri maisha yetu.
Zaidi ya asilimia 90 ya vitu vyangu vyote vimepotea, pia nimepoteza shilingi laki mbili na nusu ambazo pia zimesombwa na maji. Kwa hiyo mafuriko hayo yameongeza umasikini katika maisha yangu,
Mafuriko haya yamechafua maji ya matumizi, kwa maana kwamba maji yaliyopo sasa ni machafu hayafai kwa matumizi, hali ngumu kwa sababu maji ya visima yamechanganyika na maji ya vyooni, maana kipindi cha mafuriko vyoo vingi vilijaa maji na vingine vilibomoka kabisa, uchafu mwingi kutoka vyooni uliingia kwenye visima vya maji, sasa unaweza kuona jinsi tulivyo na maji machafu kwa sasa, hali siyo shwari.
Before flooding: Mimi ni mama wa nyumbani, ila nilikuwa nauza maandazi na mchicha. | Now: 0 |
(No Response)
« Back to report