Respondent: | Counselling and Family Life Organization (CAFLO) |
---|---|
Time Submitted: | 28 Mutarama, 2012 at 11:23 EAT |
Kombo msimbazi bondeni, Vingunguti
Kwa mtazamo wangu naona nivema kwanza watu wa mtaa huu wapate elimu ya jinsi ya kukabiliana na majanga mfano mafuriko, maana nasema hivyo kwa sababu nimeona jinsi watu walivyoteseka kipindi mafuriko yanatokea na mimi mwenyewe nikiwemo, Vilevile tunahitaji tuwekewe mitalo mikubwa yenye uwezo wa kupitisha maji mengi.
Athari ni kubwa kwa maana kwamba nyumba tunayoishi imepoteza ubora, mafuriko yamesababisha ikawa na nyufa nyingi. Kubwa zaidi mali au vitu vingi vya ndani vimepotea na vingine kuharibika, kama vile vitanda, viti, meza, kabati, vifaa vyote vinavyotumia umeme.
Kwanza kabisa nimepoteza mali nyingi, sasa hali hii imeniathiri kwa kiasi kikubwa sana kwa sababu mipango ya maisha niliyokuwa nimepanga haitaenda kama ilivyokuwa imepangwa, zaidi nimerudi nyuma sana kimaendeleo, Ila Mungu mkubwa.
Kwa ujumla ubora wa maji hakuna, maana mafuriko yameharibu vyanzo vya maji, pia maji haya yatakuwa yamechafuliwa na maji machafu hasa yanayotoka vyooni, sasa hii ni hatari kwa afya zetu.
Before flooding: Sina kazi ya ofisini, nafanya biashara ndogondogo. | Now: 0 |
(No Response)
« Back to report