How has your daily life been affected by the flooding?
maisha yameharibika sana
Pesa zangu zote zilienda na maji huwa ninaweka kwenye kabati zote zilienda na maji.Nilikuwa nimehifadhi za kujengea kibanda,kwahiyo nimeshindwa hata kupeleka watoto shule.
maisha yamekuwa magumu sana kwa upande wetu
maisha yamekuwa magumu sana
maisha yamekuwa magumu sana
Mafuriko yamenirudisha nyuma sana kimaendeleo,kwanza mimi ni Mama ntilie kwahiyo vyombo vyote vya kupikia vilienda na maji.Maisha yanaanza upya sijui nianzie wapi.Nimeacha shughuri zangu ili kushughurikia hili suala.
biashara zimepotea na hali ya maisha ni ngumu sana
Mafuriko yamenirudisha nyuma sana kimaendeleo,yani kwa maana nyingine naanza upya maisha yangu.Mimi ni Mama ntilie vyombo vyote vya kupikia vimeenda na maji pia nimeacha kazi ili kushugulikia athari hizi za mafuriko.
mvua imebeba siiting room na vyumba vya kulala na sina hata mwelekeo yaani hapa nasubiri kudra za mwenyezi Mungu kwani mama yangu amefariki hivi karibuni na nimezidi kuchanganyikiwa
shida zimenijaa wala sijui la kufanya
hakuna tunaloweza kulifanya tunahifadhiwa na wenzetu hapa na hatujui hatima ya maisha yetu na watoto wetu
sina jambo la kufanya na pia nimeadhirika kiakili
maisha ni ya shida sana kwani tunaishi juu ya mto hakun tena nafasi sehemu kubwa imechukuliwa na maji
sina mwelekeo nimechoka sijui pa kuanzia.Sina fedha na hakuna msaada wowote japokuwa mbunge wetu na viongozi wengine walituahidi misaada lakini hatujawaona tena na tumebakia tunahangaika kama wakimbizi
siwezi kwenda kujisaidia hadharani hakuna usiri.Pia vitu vya ndani sina vya kutumia naishi kwa kuombaomba
sina mahali pa kuishi na pia naishi kwa wasiwasi mkubwa kwani serikali haijatuambia nini cha kufanya na hatujui tufanyeje kwani wamesema tusubiri kwanza.Nimeadhirika kiakili pia.
yaani sina hata mwelekeo.nimeganda kabisa kimaisha sina mume mimi ni mjane na maisha yameharibika kabisa
mafuriko yameniharibia maisha yangu ya kila siku kabisa.
« Back to report