Respondent: | Promotion of Education Link Organisation (PELO) |
---|---|
Time Submitted: | January 29, 2012 at 11:17 PM EAT |
Msimbazi bondeni
Kwa kweli inahitajika nguvu ya pamoja kushinikiza serikali kumwondoa Yule mfanyabiashara aliyezungusha ukuta eneo la Kigogo sambusa ili mvua za wakati mwingine,maji yake yasizuiliwe na ukuta yakarudia kuingia kwenye nyumba za watu na kusababisha mafuriko.
Mtaji wa biashara nilikuwa nimekopa kwenye taasisi ya fedha.Kikundi changu wananidai fedha nilizokopa.Wamenifuata kuangalia kama kuna vitu vimesalia katika mafuriko ili wavipige mnada,wakanikuta sina kitu.Wananisumbua.
Kama nilivyokwambia kwamba nadaiwa,nimechanganyikiwa.Naishi kwa kubangaiza.Sina la kukwambia zaidi
Mimi hapa kwa sasa ni mkazi wa muda kwa kuwa serikali inasema mwezi wa pili tuondoke inakuja kuvunja makazi.Hivyo vyanzo vya maji viwe vimeathiriwa au la,hali kadharika vyanzo vya maji hili si swala la kufikiriwa.Hata kama kungekuwa na uharibifu,serikali haiwezi kuja kufanya maboresho sehemu ambayo inataka kuvunja nyumba.
Before flooding: nusu saa | Now: nusu saa |
(No Response)
« Back to report