Envaya

Envaya

Utafiti wa jamii kuhusu hali ya mafuriko jijini Dar-es-salaam

Respondent: Counselling and Family Life Organization (CAFLO)
Time Submitted: 27 Januari, 2012 22:48 EAT
Sinai, Vingunguti
Eneo hili halina njia au mifereji sahihi ya kupitisha maji, hivyo mvua ikinyesha maji yana twama, kiasi kwamba mafuriko yaliyopita yaliweza kuleta madhara makubwa mno. Hivyo mtaa huu unahitaji kuwe na mitalo inayoeleweka kwa ajili ya kupitisha maji hasa wakati wa mvua.
Vitu vingi vimeharibika sana kwa mfano vifaa vya ndani pamoja na vyakula vyote viliharibiwa na maji, madaftari, nguo za shule za mtoto wangu vyote vilisombwa na maji, hivyo mpaka sasa hivi mwanangu hajaenda shule kutokana na athari za mafuriko.
Mafuriko haya yameongeza kiwango cha umasikini katika maisha yangu na familia kwa ujumla, maana nimepoteza vitu vingi vya thamani, ambapo sijui kuwa nitapata vitu vingine kama nilivyokuwa navyo kabla ya mafuriko. Pia mwanangu ameshindwa kwenda shule kutokana na kupotelewa na vifaa vya shule, hali hii inarudisha nyuma maendeleo yake kielimu.
Kwa kiasi kikubwa vyanzo vya maji vimeharibika, maana mafuriko hayo yameharibu miundo mbinu ya maji, hivyo kwa sasa swala la maji ni gumu.
Kabla ya mafuriko: dakika 20Sasa: dakika 20
(Hakuna jibu)
« Jibu lililotanguliaJibu lifuatalo »

« Rudi nyuma kwenye ripoti