Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Kero ya Maji Kikuyu Hadi lini?

Wakazi wa kata ya Kikuyu Kusini Manispaa ya Dodoma hawajui hatima yao dhidi ya kero ya maji wanayo endelea kuipata kwa miongo kadhaa hadi sasa. wakazi hao wamekuwa wakitumia maji ya visma vifupi yasiyo safi wala salama kwa kipindi kirefu imeelezwa.                                                       

Kama picha inavyoonesha hapo juu; wakazi hawa wamedai kuwa wameishi katika kata ya Kikuyu kwa zaidi ya miaka ishirini na matumaini pekee waliyo nayo kuhusiana na maji ni visima vifupi wanavyo vitumia katika eneo hilo lenye wakazi wa kipato cha kati.

Licha ya kukubali kupigwa picha na kukataa kutaja majinayao; wakazi hao wameeleza kuwa wamedumu kwenye eneo hilo tangu enzi za diwani mkongwe wa eneo hilo Al-maarufu Mkungugu Marehemu Mloge aliyedumu kwenye udiwani wa eneo hilo kwa awamu nne; Meya mstaafu wa Manispaa ya Dodoma na Diwani wa eneo hilo Mh Francis Mazanda na baadaye Kata hiyo ilimpata Diwani ambaye walimtaja kwa jina  la Baba Jofu ambaye alichaguliwa katika uchaguzi wa 2010 lakini alifariki dunia kabla ya kuapishwa.

Wakazi hao wamedai kuwa eneo hilo limesahaulika kwa kipindi kirefu kwa huduma hiyo muhimu licha ya ahadi kede-kede zinazotolewa na viongozi mbalimbali wa kisiasa na serikali kila wakati kuwa watatatua kero hiyo.         

Wakazi hao wameeleza kuwa maji hayo yanayo patikana kwenye visima vifupi vilivyopo kando ya barbara ya Iringa hatua chache kutoka stendi ya daladala za Kikuyu si safi wala salama kwa matumizi ya binadamu.

Eneo la Kikuyu ni miongoni mwa maeneo yenye uhaba mkubwa wa huduma ya maji safi na salama  jambo ambalo linasababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo kwa kulazimika kutumia muda mrefu kutafuta maji.                                                                                                                                                                                                                              

27 Gashyantare, 2011
« Inyuma Ahakurikira »

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.