Envaya

Envaya

Utafiti wa jamii kuhusu hali ya mafuriko jijini Dar-es-salaam

Vyanzo na ubora wa maji kwenu yamepata athari gani kutokana na mafuriko?

maji kwa upande mmoja tunayapata ila sio kama kabla ya mafuriko
bado hali ya maji haijarudi kama ilivyokuwa awali kutokana na miundo mbinu kuharibika
bado maji yanapatikana kwa shida kutokana na miundo mbinu kuharibika
maji bado ni shida toka mafuriko yatokee mabomba yamesombwa na maji
maji tunapata kwa shida sana na vyombo vya kuhifadhia maji hatuna
Ninachojua ni kwamba visima vya maji tuliyokuwa tunatumia navyo vimeathirika na mafuriko haya, baadhi ya visima vimebomoka, waliokuwa wanamatenki ya maji nayo yamesombwa na mafuriko kwa hiyo hali ya maji ya matumizi ni mbaya, tunaishi kwa neema.
Nidhahiri kuwa maji tunayotumia kila siku yameathirika kwa kiasi kikubwa, kutokana maji tunayotumia niya visima vilivyochimbwa, hivyo mafuriko haya yameweza kuharibu visima hivyo na kuweza kuchafua maji hayo, na kuweza kupoteza ile thamani ya kuwa maji ya kutumia katika familia.
ubora wa maji kwetu umekuwa na matatizo kidogo ukilinganisha na hali ya awali kabla ya mafuriko,hii inamaana kuwa miundombinu ya mabomba yamezolewa na mafuriko.
Most of the water pipes were uprooted by the floods and needs new ones to normalize water supply in our area
Maji yetu kwakweli ni masafi sana maana tunachota msikitini na pia hakuna milipuko ya magonjwa hapa kwetu
Maji kwa kweli ni masafi tunamshukuru Mungu,huwa tunachota msikitini kwa bila malipo
« Swali lililotanguliaSwali lifuatalo »

« Rudi nyuma kwenye ripoti