Envaya

Envaya

Dar es Salaam Flooding Community Survey

Photos showing the effects of the flooding (optional)

Sehemu ya nyumba katika mtaa wa mabibo relini iliyoathiriwa na mafuriko ambayo ilibomolewa na mafuriko huku makazi yakiendelea kukabiliwa na changamoto ya mmomonyoko wa udongo katika kingo za mto
Haya ni masalia ya daraja lililokuwa likitegemewa sana na wakati wa mabibo relini wanapokwenda kupanda mabasi ya kwenda tabata,ubungo na buguruni.Kwa sasa kuna daraja la muda ambalo wakati wa masika halitaweza kuwasaidia.Angalia picha zinazofuata utaona daraja la muda lilivyo.
Hili ndilo daraja la muda linalotumiwa na wakati wa mabibo relini.Wakati wa asubuhi ni foleni kwa kuwa watu wawili hawawezi kupishana,inabidi kusubiliana.Angalia picha inayofuata.
Angalia hali ya daraja la muda wanalotumia wakazi wa mabibo relini.Picha inaonyesha mtu akivuka.Hata mvua kidogo tu ikinyesha daraja hili linamezwa.
Hizi ni baadhi ya nyumba jirani za eneo la mabibo bondeni zilizobomolewa na mafuriko.Wakazi wanajitahidi kuweka kifusi kilichoko katika magunia kuzuia tishio la kuharibika zaiidi kwa nyumba zao mara masika yanapoanza.
Hizi ni baadhi ya nyumba zilizonusulika kusomba na maji katika eneo la mabibo bondeni.Mmomonyoko wa udongo uliochochewa na mafuriko umezidi kupanua kingo za mto na kufanya wakazi wanaoishi kando ya mto kuwa katika hatari ya makazi pindi mvua za masika zitakapoanza kunyesha.
nyumba hii iliyopo pembezoni mwa bonde ilianguka na wakazi wanahitaji eneo jipya
Draja hili la mabibo sahara halikuadhirika sana na mafuriko haya ila nyumba za pembezoni zimeharibika sana
Nyumba hii nzuri lakini kama unavyojionea msingi wake umeathiriwa na mafuriko nahapo ilipo ni mkondo wa maji yanapo pita hivyo kama mvua itarudi tena basi wakazi wa eneo hili la mabibi sahara watakuwa kwenye wakati mgumu sana
nyumba ikiwa imeanguka na thamani za ndani zikiwa njea na godoro hilo ndilo ambalo jioni familia hutandika chini na kulala.
picha hii tulipaiwa na mkazi mmoja na kutuambia kuwa pamoja na Diwani kuwatembelea ambaye ni huyo mama aliyeshia bahasha bado hakuna jambo lolote ambalo limefanyika kuwasaidia kwa haraka zaidi
vyoo pamoja na mabafu vikiwa vimeathirka na mafuriko
baadhi ya nyumba zingine ambazo tuliziona njiani katika maeneo ya mabibo zikiwa kwenye bonde hili ambalo maji yalipita kwa wingi
Hadi wakati huu nyumba hii bado haijakauka maji ya mafuriko na familia hii imeyahama makazi hadi hapo hali itakapo rudi kama mwanzo
hali ya maji yaliyotuama katika maeneo ya Tabata yanaashiria kutokea magonjwa ya mlipuko pamoja na kuongezeka Mbu ambao wanazaliana kwa kasi zaidi
huu ndio mkondo wa maji ulio leta maafa katika eneo hili la tabata kisukuru maarufu kama maji chumvi
« Previous questionNext question »

« Back to report