Envaya

Envaya

Dar es Salaam Flooding Community Survey

Photos showing the effects of the flooding (optional)

Nyumba ikiwa imeangushwa na mvua ya mafuriko
Mitaa ya Tandale baada ya mafuriko kuna uwezekano wa magonjwa ya mlipuko
Eneo la kwa mtogole na adhari za mafuriko hapa kulikwa na barabara
Choo kikiwa kimebomolewa na mafuriko
Maji yalivyo haribu nyumba
Madaftari ya watoto yakiwa yameharibika na wengine wakiwa wanalalamika vyeti vyao vya Taaluma vimeenda na maji
Baadhi ya vitu vikiwa vimehabika baada ya mafuriko
Mzee huyu akieleza timu ya Envaya na N.V.R.F wakiwa wanapewa Maelezo juu ya Mafuriko na uharibifu wake
Hii ni sehemu ya ukuta wa uzio unaolalamikiwa na wakazi wa maeneo ya Kigogo na msimbazi kuwa ulichangia kwa kiasi kikubwa kuathiriwa kwa maeneo haya na mafuriko.Angalia umbali wake kutoka kwenye mto.Ukuta huu ukiangalia utaona kama haujamalizika kujengwa isipokuwa ni mafuriko yaliyouangusha,na hiki ni kiashiria kwamba kweli ukuta huu upo kwenye njia ya maji.Uzio huu unaomilikiwa na kampuni ya Highland estates umejengwa eneo la Kigogo sambusa lililokuwa wazi kwa muda mrefu.Kwa mujibu wa maelezo ya diwani wa kata ya Kigogo Mh.Chegula wakati wa kipindi cha malumbano ya hoja cha ITV mwishoni mwa mwaka jana,ni kwamba aliyekuwa Makamu wa Rais Marehemu Dr.Omary Ally Juma alikataa pasijengwe,lakini baada ya yeye kufariki pamejengwa na kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi mmoja wa serikali ya mtaa wa msimbazi bondeni anasema wao kama viongoni wa mtaa hawakushirikishwa katika ujio wa kampuni hii katika eneo hili lililokuwa wazi.Swali lililopo ni kwamba je,kuwepo kwa uzio huu hapa hakujakiuka sheria za mazingira?Kama ndivyo kwa nini uendelee kuwepo?
Nyumba hii imeathiriwa na mafuriko
SEHEMU YA NYUMBA IKIWA IMEBOMOKA KUTOKANA NA MAFURIKO
Mwakilishi wa Envaya Ramadhani Mgaya akiwa anaangalia sehemu ya mafuriko na jinsi yalivyo athiri eneo la tabata kisukuru
Baadhi ya mabomba ya kiwa hayatoi maji baada ya mafuriko hakuna huduma ya maji
Mwakilishi wa Envaya Bwana Ramadhani Mgaya na wawakilishi wa asasi za kiraia wakiwa wanafanya mahojiano na wathirika wa mafuriko Tandale kwa mtogole
Mr Ezekiel NVRF akitaka kuvuka upande wa pili lakini alikosa sehemu ya kuvukia kwa sababu ya maji na matope mengi
Hili ni daraja linalo jengwa baada ya mafuriko kutokea katika eneo la Tandale kwa mtogole na linagharimu Tshs milioni 96 mpaka lilikamilika
Angalia chumba kikiwa kimeachwa wazi baada ya vitu vyake kubebwa na maji kipindi cha mafuriko
Bangaloo hili limebomolewa na maji
Sio mtu au wezi waliobomoa nyumba hii ni maji kipindi cha mafuriko
Nyumba hii itaanguka muda sio mrefu kwani ikokariu sana na mkondo wa maji
Baada ya mafuriko tabata maji hakuna na watu wameanza kuuza maji kama biashara
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa mtogole akitoa maelezo ya maafa ya mafuriko kwa wawakilishi wa Envaya ambao wameagizwa kufuatilia swala hilo.
Hapa kulikuwa na barabara ya kupita magari lakini angalia hali ilivyo baada ya mafuriko
Nyumba hii imeathiriwa na mafuriko
Bado nyumba zingine zikiwa na maji yaliyo tuamama baada ya nafuriko
Mitaro mingi ikiwa imeshindwa kupeleka maji
Athari za mafuriko zimewafanya watu kukimbia nyumba zao kwa sababu ya kuhofia kurudi tena
Mzee akielezea jinsi mafuriko yalivyo athiri maisha yake ya kila siku
« Previous questionNext question »

« Back to report