Envaya

Envaya

Dar es Salaam Flooding Community Survey

Photos showing the effects of the flooding (optional)

Mzee Abdul S. Mwakasanga akiwa mbele ya nyumba yake ambayo ukuta umeanguka kabisa na kuharibu thamani za ndani ombi lake ni atafutiwe makazi mapya
Mama huyo aliyeshika tama akiwa na huzuni mara baada ya nyumba aliyokuwa amepanga kuzolewa na mafuriko na Mhazini wa NVRF Ndg Ezekiel William akiwa amemshika mtoto wa mama huyo ambae ni wa miezi miwili tu mama anahitaji msaada wa karibu zaidi ili aweze kumlea mtoto .
Ngugu Ezekiel William akiwa ameshika daftari na akichukua maelezo ya kina na kwa makini ya mzee huyu Abdul aliyepata janga hili la mafuriko
Mhazini wa NVRF akiwa na mtoto ambaye familia yao imepatwa na dhoruba ya mafuriko na mtoto huyu ameshindwa kwenda shule kwa ajili nguo za shule kubebwa na mafuriko ila NVRF WALICHUKUA JUKUMU LA KUMNUNULIA unform na jumatatu anaanza masomo yake.
Thamani za ndani hizi zikiwa zimeharibika kabisa .
ndugu huyo mnae muona hapo alikuwa anaeleza viongozi wa NVRF waliomtembelea jinsi maji yalivyokuwa yamefika usawa wa dirisha juu na familia hii haijarejea kwenye makazi yao
hiyo ni nyumba ya mamaCECILIA DOMINIC ikiwa imebomoka yote na kwa sasa amepewa hifadhi na majirani na hata nguo hana ndio maana amejifunga kanga tu na kilio chake ni kupatiwa makazi mapya
Baadhi ya vitu vya ndani tulivyo vikuta vikiwa vimeharibika kabisa
hivi ni baadhi ya vitu mara baada ya nyumba hii kuanguka familia ilijitahidi kuokoa vitu bila mafanikio
hii gari sio kana kwamba imepaki hapana imepata dhoruba ya mafuriko na kuharibika kabisa
mtunza fedha wa NVRF akiangalia nyumba hii ambayo wakazi hawapo mara baada ya mafuriko kutokea na bado nyumba hii imejaa maji ndani.
mzee huyu akiwa bado anaendelea na ukarabati huku nyumba ikiwa iko chini anakusanya matofali ili aanze ujenzi upya.
hapa hata choo pamoja na bafu hakuna uwezekano wa familia hizi kupata magonjwa ya mlipuko ni mkubwa
Unavyoona msitari ndani ndipo maji yalipo ishia na kuondoka na kila kitu
Bara bara ni shida kubwa
Hapa mwazo kulikuwa na Barabara
Hapa kulikuwa na nyumba imekwenda na maji
Tatizo ni kubwa twendeni tukaone tabata kisukuru wamesahaulika
Mzee huyu anasema maisha yake yameharibika kabisa
Hizi sio taka taka ni nguo za mtu tena za kuvaa zimekuwa hivi kwa sababu ya Mafuriko
Hili ni Godoro la mzee huyu na ndilo lililo salia hana lingine
Mzee Rashidi Ally Mhina anasema amebebewa kila kitu na maji
Unapoona unyevu wa maji kwenye ukuta ni nyumba ya mzee Rashidi anaomba kuhamishwa yuko tayari kuhama kilio chake ni kwanba wamekumbukwa watu wa Jangwani tu lakini watu wa Tabata hawaja kumbukwa.
« Previous questionNext question »

« Back to report