Photos showing the effects of the flooding (optional)

Hii ni sehemu ya ukuta wa uzio unaolalamikiwa na wakazi wa maeneo ya Kigogo na msimbazi kuwa ulichangia kwa kiasi kikubwa kuathiriwa kwa maeneo haya na mafuriko.Angalia umbali wake kutoka kwenye mto.Ukuta huu ukiangalia utaona kama haujamalizika kujengwa isipokuwa ni mafuriko yaliyouangusha,na hiki ni kiashiria kwamba kweli ukuta huu upo kwenye njia ya maji.Uzio huu unaomilikiwa na kampuni ya Highland estates umejengwa eneo la Kigogo sambusa lililokuwa wazi kwa muda mrefu.Kwa mujibu wa maelezo ya diwani wa kata ya Kigogo Mh.Chegula wakati wa kipindi cha malumbano ya hoja cha ITV mwishoni mwa mwaka jana,ni kwamba aliyekuwa Makamu wa Rais Marehemu Dr.Omary Ally Juma alikataa pasijengwe,lakini baada ya yeye kufariki pamejengwa na kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi mmoja wa serikali ya mtaa wa msimbazi bondeni anasema wao kama viongoni wa mtaa hawakushirikishwa katika ujio wa kampuni hii katika eneo hili lililokuwa wazi.Swali lililopo ni kwamba je,kuwepo kwa uzio huu hapa hakujakiuka sheria za mazingira?Kama ndivyo kwa nini uendelee kuwepo?
(No Response)
(No Response)
(No Response)
(No Response)
(No Response)
(No Response)
(No Response)
(No Response)
(No Response)

Mwakilishi wa Envaya Ramadhani Mgaya akiwa anaangalia sehemu ya mafuriko na jinsi yalivyo athiri eneo la tabata kisukuru

Mwakilishi wa Envaya Bwana Ramadhani Mgaya na wawakilishi wa asasi za kiraia wakiwa wanafanya mahojiano na wathirika wa mafuriko Tandale kwa mtogole

Mr Ezekiel NVRF akitaka kuvuka upande wa pili lakini alikosa sehemu ya kuvukia kwa sababu ya maji na matope mengi

Hili ni daraja linalo jengwa baada ya mafuriko kutokea katika eneo la Tandale kwa mtogole na linagharimu Tshs milioni 96 mpaka lilikamilika
(No Response)
« Back to report