How did the flooding affect your own property and possessions?
Nilikuwa na mwezi mmoja tu nikiwa nimehamia katika nyumba ya niliyokuwa nimepanga huku nikiwa nimelipa kodi ya mwaka mzima.Biashara yangu ni ya kubangaiza.Najiuliza nitatoa wapi tena kodi ya nyumba ambayo nimetumia muda mrefu kuitafuta kwa kujinyima.
Naishi maisha ya shida na msamaria mwema mmoja.Amejitolea kunihifadhi katika kipindi hiki kigumu.Mke wangu anakaa kwa mama mmoja ambaye tunasali wote kanisa moja,wakati watoto nao wanaishi kwa ndugu.Ni kama familia imesambaratika.Inaniumiza sana.
Mtaji wa biashara nilikuwa nimekopa kwenye taasisi ya fedha.Kikundi changu wananidai fedha nilizokopa.Wamenifuata kuangalia kama kuna vitu vimesalia katika mafuriko ili wavipige mnada,wakanikuta sina kitu.Wananisumbua.
Vitu vyangu vingi sana vimechukuliwa na maji lakini kinachoniuma ni vifaa vya kusomea vya wanangu vilivyosombwa na maji huku wakitegemea kufanya mitihani ya taifa mwaka huu
Hata vitu vyangu vichache vilivyokuwa vimebaki bila kuchukuliwa na maji,vibaka walivunja nyumba na kuiba.Nimebaki hivihivi.
vitu vyangu vilivyookolewa vingi havifai,vimelowa na maji.Vingine vilisombwa na maji pamoja na mtaji wangu wa vitumbua.
Vitu vyangu vingi vimepotea,naanza maisha upya.
Kama unavyoona narudia kujenga upya karibu nusu ya nyumba yangu iliyobomolewa na mafuriko
Choo cha nyumba yangu vimesombwa na maji,kwa sasa tunajisaidia nyumba ya jirani.
Nilikuwa na banda la mifugo limesombwa na maji pamoja na mifugo.
Nyumba yangu imeharibika kabisa.Chumba kimoja kilisombwa na maji na vyombo vyote vilivyokuwemo.
Nyumba ambayo tulikuwa tumepanga imeharibika vibaya, vilevile vitu vya ndani karibu vyote vimeharibika, kwa hiyo ni maafa makubwa.
Athari ni kubwa kwa maana kwamba nyumba tunayoishi imepoteza ubora, mafuriko yamesababisha ikawa na nyufa nyingi. Kubwa zaidi mali au vitu vingi vya ndani vimepotea na vingine kuharibika, kama vile vitanda, viti, meza, kabati, vifaa vyote vinavyotumia umeme.
Mafuriko yaliyotokea yameongeza ugumu wa maisha kutokana na kwamba mali nyingi zimepotea kutokana na mafuriko, kwa mfano mimi nimepoteza vyombo vya ndani, vyakula (maharage, unga, mchele), mifugo (kuku) vyote vilisombwa na mafuriko.
Mimi ni mpangaji na nyumba ambayo nilikuwa nimepanga, ilikuwa na jumla ya wapangaji kumi, lakini cha kusikitisha mafuriko haya yameleta maafa makubwa sana, maana mali au vitu mbalimbali vimepotea, kibaya zaidi ndugu wa mpangaji mwenzangu amesombwa na maji na kufariki, hivyo unaona ni kwa jinsi gani ambavyo mafuriko yameathiri maisha yetu.
Vitu vingi vimeharibika sana kwa mfano vifaa vya ndani pamoja na vyakula vyote viliharibiwa na maji, madaftari, nguo za shule za mtoto wangu vyote vilisombwa na maji, hivyo mpaka sasa hivi mwanangu hajaenda shule kutokana na athari za mafuriko.
Nyumba imebomolewa na mafuriko, vifaa vya shule kwa wanafunzi vimechukuliwa, Vifaa vyote vya ndani vimechukuliwa, Nguo zote zimechukuliwa na maji,
nyumba nyingi zilizopo katika bonde la sahara ziko hatarini kuanguka na kama mvua itarudi tena kuna hatari kubwa itakayo tokea
makazi yameharibika kwa kiwango kikubwa sana.
Vitu vya ndani pamoja na vyoo vimeharibika kabisa
« Back to report