Injira
Lift Life Foundation Development (LLFD)

Lift Life Foundation Development (LLFD)

Madizini, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

UHARIBIFU WA MAZINGIRA.

Katika maisha ya sasa uhalibifu wa mazingira umekuwa ni kiwango cha juu sana kiasi kwamba kampeni zote zinazopigwa inaonekana ni kama kutwanga maji kwenye kinu.

Fedha nyingi sana zinatolewa kuhifadhi misitu lakini inaonekana haziwafikii walengwa na kusababisha uharibifu kuendelea kama jinsi kamera yetu ilivyonasa uharibifu huu wa miti katika harakati za uchomaji mkaa.

wapendwa wana harakati hamjambo? Lift Life Tulinyamaza kitambo kwa kuwa bado tulikuwa tunajipanga kikazi zaidi.

Habari mpya tulizonazo leo ni kuhusu kujenga uwezo kwa vijana kwa matumizi ya kompyuta(kichakato kikuu) mwaka jana shirika letu tumeendesha mradi wa kujenga uwezo kwa vijana juu ya matumizi ya kiku kwa maana ya kompyuta, na tulifaulu kuwajengea vijana wapatao 20 na sasa wameweza kutumia kompyuta kwa mawasiliano mbalimbali pamoja na kujiajili.

mradi ulianza November 01 2011 na kukamilika January 2012. Mradi huu ulifadhiliwa na watanzania na uligharimu kiasi cha shilingi za kitanzania 3,000,000/=(milioni tatu)

HABARI ZA UTAWALA BORA.

Katika mapambano ya kupunguza umasikini,ujinga na maradhi utawala bora na nyenzo mhimu katika mapambano haya. Lakini unaweza kushanga kusikia kuwa tangu uchaguzi umemalizika kuna kijiji kimoja hakina serikali kwa mda wa miezi kadhaa na hivyo kusababisha maendeleo ya eneo husika kuzorota kutokana na maswala ya kisiasa tu. Kijiji kimoja katika wilaya Mvomero tarafa ya Turiani na Kata ya Dingoya kinachojulikana kwa jina la Lusanga hakina serikali kutoka na kujiuzuru kwa serikali iliyokuwepo ya chama cha mapinduzi na kumuacha mwenyekiti wa chama cha cuf akibakia pekee bila serikali na hivyo kuwa na wakati mgumu wa kutoa maamuzi yanayohusu maendeleo ya kijiji hicho. Kijiji hiki ni moja ya vijiji vyenye miradi mingi toka wahisani mbalimbali pamoja na serikali lakini miradi hiyo haitekelezwi kwa ufanisi na viwango vinavyohitajika hii ni kutokana na utawala duni wa kijiji hicho.

Mfano ni mradi wa soko na maji ambayo kwa pamoja viligharimu kiasi cha sh 160 milioni hivi, lakini utekelezaji wake ni wa kiwango cha chini mno kiasi cha soko kuanza kubomoka kabla hata halijatumiwa au kufunguliwa, wakati maji yenyewe bado ni kitendawili katika kijiji hicho, wanawake hukaa visimani hadi saa 6 usiku wakisubiri kuchota maji na hivyo kushindwa kufanya kazi za maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

MAZINGIRA.

Je wajua kuwa ile dhahabu ya miti iitwayo mitiki inapatikana katika kijiji hicho cha Lusanga na vijiji vingine vya Kunke,Dihinda na Madizini lakini wananchi wake ndio wanaongoza kwa umasikini illihali mrahaba wa msitu huo ukiishia mifukoni mwa wachache wenye ujanja,hivi karibuni pamekuwa na ugawaji wa cbm kadhaa kwa wananchi ili kushiriki uvunaji shirikishi, kupitia ukurasa huu tutawajulisheni wanaharakati yaliyojili katika mgao huu kama walengwa watapatiwa kipaumbele. Hapa tunamaanisha msitu wa mitiki mtibwa.

UTETEZI

Ukizungumza juu ya ukeketaji watu wengi wanamulika mikoa ya Mara,Arusha,Dodoma, Kilimanjaro na Manyara. Lakini aminiusiamini mkoa wa Tanga unaoongoza kwa ukeketaji pia, pana ukeketaji wa kisiri sana kwa kabila la wazigua kwani kitendo cha kumuweka mwali ndani huambatana na ukeketaji ambao huwa siri kubwa sana kwa wahusika kiasi cha kutishwa ikiwa atatoa siri ya ngoma hiyo ya mwali. Huu ni utafiti uliofanywa na asasi yetu kwa mda mrefu na kubaini matokeo, hivyo tunajulisha wapendwa wanaharakati kuelekeza jitihada za kwatetea wanawake katika maeneo husika katika mkoa wa Tanga na Morogoro kwani sisi pekee hatuwezi kutoshereza huduma hii japo tunaifanya sasa.

Shirika letu kwa sasa tumeweza kuwasaidia watoto 45 wanaoishi katika mazingira hatarishi wa vijiji vya Lusanga, Kwadoli na Dihinda kupunguza makali ya maisha kwa kuwapatia chakula,nguo na vifaa vya kusomea.

Pia upande wa VVU/UKIMWI shirika limeweza kuendesha zoezi la kupima kwa hiari katika kijiji cha Lusanga  ili kubaini maambukizi mapya hapo mwaka 2009 na 2010 na kubaini waathirika 18 ambao wanapata huduma ya dawa za kurefusha maisha sasa.

ELIMU:Shirika limeendelea kutoa elimu ya tekinolojia kwa vijana na watu wazima chini ya mradi wake wa ongeza maarifa ya tekinohama(omayate), mpaka sasa vijana 17 na watu wazima 10 wamepata elimu ya tekinohama,mradi huu ulianza mwezi wa July 2010 na ni mradi endelevu.

Shirika linakusudia kuendesha mradi wa kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji katika Tarafa 2 za Turiani na Mvomero hapo ifikapo June 2011 kama tutapata ufadhili mapema.