Injira
Lift Life Foundation Development (LLFD)

Lift Life Foundation Development (LLFD)

Madizini, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Shirika la LIFT LIFE FOUNDATION DEVELOPMENT (LLFD) lilianzishwa mwaka 2006 katika Tarafa ya Turiani wilaya Mvomero mkoa Morogoro, likiwa na lengo la kupambana na umasikini, ujinga na maradhi ili kuwapa watanzania maisha bora. Shirika lilisajiliwa rasmi katika ofisi ya makamu wa raisi mwaka 2007 July kwa usajili wa kitaifa. SHirika lina wanachama 16.

Shirika lilipata ufadhili wa kwanza mwaka 2009 toka the Foundation for Civil Society ukiwa ni wa mzunguko mfupi kwa ajili ya kujenga uwezo wa shirika kiutendaji.Hadi wakati huu shirika linaendelea kuhudumia wananchi katika miradi mbalimbali ya utawala bora, utetezi na elimu.