Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

HABARI ZA UTAWALA BORA.

Katika mapambano ya kupunguza umasikini,ujinga na maradhi utawala bora na nyenzo mhimu katika mapambano haya. Lakini unaweza kushanga kusikia kuwa tangu uchaguzi umemalizika kuna kijiji kimoja hakina serikali kwa mda wa miezi kadhaa na hivyo kusababisha maendeleo ya eneo husika kuzorota kutokana na maswala ya kisiasa tu. Kijiji kimoja katika wilaya Mvomero tarafa ya Turiani na Kata ya Dingoya kinachojulikana kwa jina la Lusanga hakina serikali kutoka na kujiuzuru kwa serikali iliyokuwepo ya chama cha mapinduzi na kumuacha mwenyekiti wa chama cha cuf akibakia pekee bila serikali na hivyo kuwa na wakati mgumu wa kutoa maamuzi yanayohusu maendeleo ya kijiji hicho. Kijiji hiki ni moja ya vijiji vyenye miradi mingi toka wahisani mbalimbali pamoja na serikali lakini miradi hiyo haitekelezwi kwa ufanisi na viwango vinavyohitajika hii ni kutokana na utawala duni wa kijiji hicho.

Mfano ni mradi wa soko na maji ambayo kwa pamoja viligharimu kiasi cha sh 160 milioni hivi, lakini utekelezaji wake ni wa kiwango cha chini mno kiasi cha soko kuanza kubomoka kabla hata halijatumiwa au kufunguliwa, wakati maji yenyewe bado ni kitendawili katika kijiji hicho, wanawake hukaa visimani hadi saa 6 usiku wakisubiri kuchota maji na hivyo kushindwa kufanya kazi za maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

MAZINGIRA.

Je wajua kuwa ile dhahabu ya miti iitwayo mitiki inapatikana katika kijiji hicho cha Lusanga na vijiji vingine vya Kunke,Dihinda na Madizini lakini wananchi wake ndio wanaongoza kwa umasikini illihali mrahaba wa msitu huo ukiishia mifukoni mwa wachache wenye ujanja,hivi karibuni pamekuwa na ugawaji wa cbm kadhaa kwa wananchi ili kushiriki uvunaji shirikishi, kupitia ukurasa huu tutawajulisheni wanaharakati yaliyojili katika mgao huu kama walengwa watapatiwa kipaumbele. Hapa tunamaanisha msitu wa mitiki mtibwa.

UTETEZI

Ukizungumza juu ya ukeketaji watu wengi wanamulika mikoa ya Mara,Arusha,Dodoma, Kilimanjaro na Manyara. Lakini aminiusiamini mkoa wa Tanga unaoongoza kwa ukeketaji pia, pana ukeketaji wa kisiri sana kwa kabila la wazigua kwani kitendo cha kumuweka mwali ndani huambatana na ukeketaji ambao huwa siri kubwa sana kwa wahusika kiasi cha kutishwa ikiwa atatoa siri ya ngoma hiyo ya mwali. Huu ni utafiti uliofanywa na asasi yetu kwa mda mrefu na kubaini matokeo, hivyo tunajulisha wapendwa wanaharakati kuelekeza jitihada za kwatetea wanawake katika maeneo husika katika mkoa wa Tanga na Morogoro kwani sisi pekee hatuwezi kutoshereza huduma hii japo tunaifanya sasa.

June 3, 2011
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.