Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

1.UTAWALA BORA

 Lit Life kwa kutambua umuhimu wa utawala bora katika kupunguza umasikini tumekuwa na mradi wa kuwajengea uwezo viongozi wa vijiji katika kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji katika wilaya Mvomero kwenye kata za mtibwa, kanga na diongoya.

Mradi huu tumeufanyia utafiti yakinifu tayari na kukusanya takwimu zinazohitajika na tutaanza utekelezaji wake hapo Augost.

2. UUNDWAJI WA KATIBA MPYA.

Kwa kuwa asasi ya yetu ni mdau katika kuhakikisha wananchi wanafikiwa na kutoa maoni yao juu ya katiba mpya, asasi tumekuwa na mradi wa kuwajengea uwezo vijana katika kutambua umuhimu wao kuhusika katika maoni ya mabadiliko ya katiba kwa kuwa 40% ya watanzania ni  vijana.

Hivyo wanaharakati wote tuliangalie jambo hili kwa umakini sana kuhakikisha watanzania wengi wanafikiwa na kutoa maoni yao hasa wale walio vjijini kwani ndio wengi na hawatambui mabadiliko yoyote yanapotokea kwani mambo mengi yanaishia mijini.

3. TEKNOLOJIA YA MAWASILIANO

Asasi yetu imekuwa ikiendesha mradi wa tekinolojia ya habari na mawasiliano kwa kuwajengea uwezo vijana wa kuanzia umri wa miaka 12 - 30 kwa kuwapatia mafunzo ya computer kwa lengo la kuwaandaa kuutumia mkonga wa kitaifa hapo utakapokamilika mwakani. Mradi huu tunautekeleza katika kata ya Mtibwa wilaya Mvomero katika shule ya msingi Mtibwa iliyopo katika mji mdogo wa Madzini.

4.MAZINGIRA

Aasasi yetu katika kuhifadhi mazingira tumekuwa na mradi wa kuwahamasisha waoteshaji wa miti na wananchi wanaoishi katika maeneo yaliyo katika vyanzo vya maji kuotesha miti kwa lengo la kuhifadhi uotoo wa asili. Ambapo zaidi ya miti ipatayo 13,000 imeoteshwa katika kipindi cha mwaka mmoja katika tarafa ya Turiani inayozungukwa na milima ya unguu, pia zaidi ya vikundi 30 vya waoteshaji miti vimeanzishwa na ni endelevu chini ya mradi wa ANZISHA MSITU WAKO (AMWA)

Hivyo wapendwa wanaharakati tunaomba ushirikiano kwani kuna changamoto nyingi katika kutekeleza miradi hii ikizingatiwa mingi tunajitolea kwa kuwa hatuna uwezo wa kutosha kifedha.