Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
HakiElimu yazindua shindano la Insha na michoro
![]() |
Shindano la insha na michoro la HakiElimu |
katika uzinduzi huo, mwenyekiti wa jukwaa la katiba Bw Deus Kibamba aliwaomba watanzania kutoa mawazo yao juu ya nini wanataka kijumuishwe kwenye katiba mpya kuhusu elimu kwa kufafanua kwamba katiba ya sasa inaiongelea elimu kama ni haki ambayo watanzania hawawezi kuidai.
"Katiba ya sasa inatoa fulsa ya kuwa kila mtanzania ana haki ya elimu kwa kujitafutia yeye mwenyewe", alisema Kibamba akifafanua kuwa katika mazingira hayo mtanzania hawezi kuidai haki hiyo mahali popote.
Mwisho wa kupokea insha au michoro ni tarehe 30 Juni 2012 ambapo washindi watatangazwa mwezi septemba.
Izingatiwe kuwa washindi tuu ndo watakaotangazwa.
Ibitekerezo (0)
Wanafunzi 5,000 waliofaulu hawajui kusoma, kuandik

Monday, 09 April 2012 20:42 |
0digg Fredy AzzahIMEBAINIKA kwamba wanafunzi 5,200 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu, hawajui kusoma wala kuandika. Kutokana na sababu hiyo, habari kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinasema kwamba wanafunzi hao wataachishwa masomo na Serikali inaangalia uwezekano wa kuchukua hatua za kisheria wanafunzi hao na wakuu wa shule wanazotoka ili kukomesha tatizo hilo. Wanafunzi hao wanatoka katika mikoa yote ya Tanzania bara, isipokuwa Kigoma ambao taarifa zake hazijafika katika wizara hiyo. Wanafunzi hao wamebanika kutojua kusoma wala kuandika baada ya kupewa majaribio ya kupima uwezo wao wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) baada ya kuripoti shuleni kama ilivyoagizwa na Serikali. Desemba 14, mwaka jana wakati akitangaza matokeo ya Mitihani ya Darasa la Saba, Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo aliagiza wanafunzi wote watakaoingia kidato cha kwanza mwaka huu wapimwe kwanza uwezo wao wa Kusoma na Kuandika. Agizo hilo lilitokana na udanganyifu uliojitokeza kwenye mtihani huo na kusababisha watoto 9,736 kufutiwa matokeo. Wanafunzi waliofanya mtihani huo walikuwa 983,545 na waliofaulu ni 567,567. Kati yao wasichana walikuwa 278,377 sawa na asilimia 54.48 na wavulana walikuwa 289,190 sawa na asilimia 62.49. Akizungumza na wafanyakazi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) mwishoni mwa wiki, Mulugo alisema tathmini inaonyesha kuwa Mkoa wa Kilimanjaro umeongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi wasiojua kusoma na kuandika. "Mkoa wa Kilimanjaro una wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wapatao 660, Tanga 490 na Dar es Salaam 208," alisema Mulugo bila kutaja matokeo ya mikoa mengine. “Hili ndilo janga la kitaifa sasa. Siyo hayo mengine ambayo watu wanasema ni majanga ya kitaifa. Lazima tujiulize kwa nini watoto wanamaliza darasa la saba wakiwa hawajui kusoma wala kuandika na halafu wanafaulu?” alihoji kuongeza: “Je, siku hizi hakuna tena somo la kusoma na kuandika? Kwa nini mtoto amalize shule bila kuwa na maarifa ya KKK? Mitaala (mitalaa) mnayoandika kwa nini hamsaidii mtoto katika hili? Nataka leo nijue tatizo liko wapi, mengine (matatizo) ya Serikali; walimu, vitabu, miundombinu na majibu yake sisi tunayo.” “Jambo la kusikitisha kuna mpaka baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tatu, ambao hawajui kusoma wala kuandika. Tulipofikia siyo pazuri hata kidogo, lazima tuwe makini jamani. Tuheshimu Baraza la Mitihani (Necta) tupate ufumbuzi wa mambo haya taifa hili ni letu sote, lazima tuhakikishe linasimama imara.” Alisema Serikali kwa upande wake, imejipanga kufanya utafiti na kujua chanzo cha tatizo na kuwa imepata Sh150bilioni kutoka Global Partnership for Education (GPE), kwa ajili hiyo. Kaimu Mkurugenzi wa TET, Habib Fentu alisema mitalaa waliyoandika imesisitiza mwalimu kufanya tathmini ya kile alichofundisha kila baada ya mada husika kumalizikia. “Kwa hiyo hapa sasa suala la uwajibikaji linakuja, inakuwaje mtoto amalize darasa la saba akiwa hajui kusoma, kuandika wala kuhesabu na mwalimu wa darasa yupo, mwalimu wa taaluma, mwalimu mkuu na kamati ya shule vipo?” Katika matokeo ya darasa la saba yaliyotangazwa mwaka jana, Mkoa wa Manyara uliongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliofutiwa matokeo ukifuatiwa na Arusha. Habari kwa hisani ya gazeti la Mwananchi |
WALIMU 50 WALALA CHUMBA KIMOJA WAKIDAI MAFAO YAO WILAYANI MBOZI – MBEYA.
Walimu tuna hali ngumu maisha yetu yamewekwa rehani kwenye maduka na Maafisa watendaji wa Kijiji, ambao wamekuwa wakitukopesha pesa za kujikimu.
Zaidi ya walimu 50 waliopata ajira mpya hivi karibuni katika Shule za Msingi na Sekondari katika Wilaya ya Mbozi, Mkoani Mbeya wamejikuta wakilala chumba kimoja baada ya Ofisi ya Halmashauri ya wilaya hiyo kufungwa huku walimu hao hawajapata sitahili zao.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea kwa siku mbili mfululizo, baada ya walimu hao waliotokea maeneo tofauti tofauti wilayani humo na baada ya kufika katika Ofisi hizo za Halmashauri hawakuweza kupata stahili zao kama vile pesa za kujikimu, nauli na mishahara kwa muda wa miezi miwili mpaka sasa.
Mnamo Machi 6 mwaka huu, walimu hao walimuona Mkuu wa Wilaya hiyo Bwana Gabriel Kimoro ambapo walilipwa posho ya shilingi laki moja (100,000) kwa kila mmoja kwa ahadi ya kuwa mwishoni mwa mwezi stahili zao zote zingelipwa, lakini mambo yalikuwa tofauti Machi 27 na 28 kwani madai yao yalikuwa hayajashughulikiwa.
Kiongozi wa walimu hao Mwalimu Carlos Magoyo amesema baada ya maafisa wa halmashauri kutawanyika waliamua kulala katika ofisi hizo za Mkuu wa wilaya kwani walikuwa hawana pesa za nauli na kujikimu, kabla ya kutokea msamaria mwema aliyewapa chumba hicho kimoja na kuchanganyika jinsi zote huku wakiimba pambio na kutafuna mahindi ya kuchoma.
Aidha Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo Bwana Levson Chilewa amesema madai yao ya posho yanaanza kushugulikiwa mara moja na Ofisi ya fedha ya halmashauri hiyo lakini kuhusiana na mishahara yao ipo nje ya uwezo wake kwani suala hilo linashughulikiwa na Serikali kuu yaani Hazina kuu.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya Bwana Kimoro ameahidi kufuatilia madai hayo kwa ukaribu zaidi na amesikitishwa kwa kitendo hicho cha kucheleweshwa mishahara kwani baadhi ya walimu wanatoka mbali na mji wa Vwawa na asingependa kuona walimu wakiishi maisha ya kuombaomba.
Naye, Afisa Elimu Mkoa wa Mbeya Bwana Juma Kaponda amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kwamba atawasiliana na Mkurugenzi wa wilaya hiyo ili walimu hao walipwe mapema iwezekanavyo, ingawa kwa sasa yupo safarini kikazi nje ya mkoa.
Baadhi ya walimu walionekana wakiwa na watoto wadogo na baadhi yao wamekesha wakiwa wamewapakata watoto wao kutokana na kukosa eneo la malazi sambamba na kukosa hata chakula cha watoto ambao wapo chini ya umri wa miaka miwili.
Habari na picha kwa hisani ya mtandao wa Mbeya yetu
Pinda ataka wadau wa elimu kutafuta muarobaini wa changamoto za elimu Tanzania

Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda akizungumza
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewataka washiriki wa mkutano wa taifa juu ya maendeleo ya elimu nchini kutafuta njia bora ya ufumbuzi wa changamoto zinazochangia kudhoofisha maendeleo ya sekta ya elimu nchini.
Waziri Pinda ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa mkutano huo wa taifa wa elimu ulioandaliwa na Shule ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuinua kiwango cha elimu nchini.
Kuhusu elimu ya awali, amesema kuwa watanzania wengi hususani wa vijijini wamekuwa hawaipi kipaumbele kiasi kwamba watoto wakipelekwa shule za msingi wanacheza kwa sababu wamekosa fursa ya kucheza katika shule za awali. Amesisitiza kuwa kila shule ya msingi iwe na darasa la awali ili kuwafanya watoto kuzoea mazingira ili wanapoanza shule ya msingi waanze kukabiliana vizuri na masomo.
Akizungumzia suala la mikopo kwa elimu ya juu, Pinda amesema serikali ilianzisha hilo kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi ambao wanakwenda kujiendeleza katika masomo hayo lakini hivi sasa imebaini kuwa kuna changamoto kubwa serikalini kwani fedha hazitoshi kutokana na wanafunzi kuwa wengi. Amewataka wadau hao kuja na mbinu mpya ya kuweza kutoa mikopo kwani wanafunzi hao wamekuwa hawarejeshi mikopo yao hali inayoipa serikali wakati mgumu.
Naye Mkuu wa Shule hiyo ya Elimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Professa Alistella Balalulisa amesema kuwa wameamua kufanya mkutano huo kutokana na taaluma ya elimu inavyokwenda hapa nchini ikizingatiwa kwamba kiwango cha ufaulu katika shule za msingi na shule za sekondari kimekuwa kikishuka mwaka hadi mwaka na kulalamikiwa na wadau mbalimbali wakiwemo wazazi ambao wanaitupia lawama sekta ya elimu nchini.
Amesema wao kama wanataaluma wameamua kuitisha mkutano huo ili kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo na kutoa njia ama mbinu mbalimbali za kukabiliana na changamoto hizo. Mkutano huo wa siku tatu umewakutanisha wadau mbalimbali wa elimu nchini ambao ni watafiti na walimu wanaofundisha katika sekta mbalimbali za elimu hapa nchini.
Habari na picha kwa mujibu wa mtandao wa Thehabari.com
Short URL: http://www.thehabari.com/?p=14978
Wanafunzi 159 wa Shule ya Sekondari Maneromango wakimbia mitihani

Mwalimu wa Taaluma wa Shule ya Sekondari Maneromango iliyopo Kata ya Maneromango, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Jonas Buheruko alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa mtandao wa Thehabari.com (hayupo pichani) jana ofisini kwake.
Na Joachim Mushi, Thehabari.com-Kisarawe
WANAFUNZI 159 wa Shule ya Sekondari Maneromango wametoroka kufanya mitihani ya majaribio ya robo muhula iliyoanza juzi katika shule hiyo.
Wanafunzi hao ambao ni vidato mbalimbali kuanzia cha kwanza hadi cha nne, ni kati ya wanafunzi 383 wa Shule ya Sekondari Maneromango waliotakiwa kuanzia kufanya mitihani yao Machi 27, 2012 shuleni hapo.
Akizungumza katika mahojiano na mtandao wa Thehabari.com katika shule hiyo iliyopo Kata ya Maneromango, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani, Mwalimu wa taaluma wa shule hiyo, Jonas Buheruko alisema ofisi yake imebaini utoro huo baada ya kukusanya taarifa kutoka vidato vyote.

Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari Maneromango iliyopo Kata ya Maneromango, Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani wakifanya mitihani yao ya majaribio ya robo muhula jana.
Alisema taarifa zilizokusanywa siku ya kwanza kuanza kwa mitihani hiyo, Machi 27 mwaka huu, zimebaini kidato cha nne ndiyo wanaoongoza kwa utoro wa mitihani kwani kati ya wanafunzi 106 waliotakiwa kuanza kufanya mitihani hiyo ya majaribio ni 45 pekee walifanya huku 65 wakiingia mitini.
“Taarifa zangu nilizokusanya baada ya kuanza tu kwa mitihani zinaonesha kidato cha kwanza wametoroka wanafunzi 10 kati ya 81, kidato cha pili wametoroka 31 kati ya 103, kidato cha tatu wametoroka 53 kati ya 93 waliotakiwa kuanza kufanya mitihani hiyo,” alisema Mwalimu Buheruko.
Hata hivyo alisema kitendo cha utoro wa mithani shuleni hapo sasa kinaendelea kuwa sugu licha ya walimu kufanya jitihada za kuwafuatilia wanafunzi na kutoa adhabu mbalimbali kulingana na taratibu za shule.
Aidha aliongeza mwaka 2011 wanafunzi 34 wa kidato cha nne kati ya 85 walikimbia kufanya mtihani wa majaribio wa Wilaya shule hapo jambo ambalo linawakatisha tamaa walimu katika utoaji wa elimu shuleni hapo.
“Wamekuwa wakikimbia mitihani mara nyingi…tunawapa adhabu lakini wapo radhi kufuraia adhabu unayowapa kuliko kuja kufanya mitihani…wakati mwingine tunapozidiwa tumekuwa tukipeleka majina ya watoro kwa Mwenyekiti wa Kijiji na Ofisa Mtendaji wa Kata lakini bado hatujaweza kudhibiti utoro huu,” aliongeza mwalimu Buheruko.
Akizungumzia hali hiyo, Mratibu wa Elimu Kata ya Maneromango, Nicolaus Lemma amesema wamekuwa wakiwaita mara kadhaa wazazi wa wanafunzi na kuwashtaki pale inapobainika wanachangia utoro wa watoto wao, ila tatizo hilo si kwa sekondari pekee bali hata shule za msingi eneo hilo.
Habari hii ni kwa hisani ya mtandao wa Thehabari.com
Short URL: http://www.thehabari.com/?p=14982
Kumbukumbu ya band ya shule Liwale Mkoani Lindi

Viongozi wa band ya shule wakiongoza wenzao kuingia madarasani huku wakipita kwa ukakamavu mbele ya ofisi ya mwalimu mkuu.

Wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Magereza wilayani Liwale wakiwa kwenye gwaride la kuingia madarasani baada ya chakula cha mchana.Shule hii imepeleka wanafunzi wote sekondari (ufauru ni asilimia 100).

Lowassa Akuatana na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto kujadili sababu za kufanya vibaya kwenye mtihani wa Taifa


Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza kwa kusisitiza wakati wa mkutano wake na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Engutoto,Wilayani Monduli kuhusiana na hali ya elimu katika shule hiyo kutoridhisha na kupelekea wanafunzi wengi wa shule hiyo kufeli kwenye mtihani wa taifa wa kidato cha nne.Mkutano huo umefanyika leo shuleni hapo,ambapo walimu wa shule hiyo walitoa changamoto mbali mbali wanazomabiliana nazo.Mh. Lowassa amewaasa walimu wa Shule hiyo kuwa wafanye kazi kwa juhudi ili kuwaandaa vijana wa taifa la baadae.Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo,Bw. Joseph Lukumay.










Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akimsikiliza kwa makini,Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Shule ya Sekondari ya Engutoto,Bw. Joseph Lukumay.
Picha na habari na Blog ya HakiNgowi
Hongera Tido Mhando kwa kuwa mkurugenzi mpya wa Mwananchi Communications LTD

HakiElimu inatoa pongezi kwa uteuzi huo.
Mpango wa Elimu Kata ya Kipawa.flv
Kata ya Kipawa ipo katika Manispaa ya Wilaya ya Ilala, Mkoani Dar Es Salaam. Wilaya hii ndipo sehemu zifuatazo zinapopatikana, Ikulu , Makao Makuu ya Jeshi la Wananchi, Benki Kuu ya Tanzania, Makao Makuu ya Wizara Mbalimbali ikiwemo ile ya Elimu, Klabu Maarufu za Mpira Nchini Simba na Yanga, Mashirika na Asasi za Maendeleo nchini , Hospitali Ya Taifa Muhimbili nk .Pamoja na hayo yote wilaya hii bado ina changamoto za elimu kama inavyoonekana katika video hii. Cha kuvutia ni jitihada ambazo Mheshimiwa Diwani wa Kata hii Bonnah Kaluwa ambazo ameamua kuchukua kwa nafasi aliyopewa na wananchi wake katika kutatua matatizo katika eneo lake . Je Ni Viongozi wangapi wamethubutu kuchuka hatua? Muunge mkono na pia elimisha viongozi wa eneo lako wachukue hatua kama alivyofanya Diwani huyu, |
From:
hakielimutz
Views:
61
![]() ![]() ![]() ![]() ![]() 0
ratings | |
Time: 07:54 | More in Nonprofits & Activism |
DVD (1)
Uploaded with Free Video Converter from Freemake www.freemake.com |
From:
hakielimutz
Views:
51
![]() ![]() ![]() ![]() ![]() 0
ratings | |
Time: 02:32 | More in Film & Animation |