Injira
HakiElimu

HakiElimu

Dar Es Salaam , Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Maisha ya 'geto' ni chanzo cha mimba kwa wanafunzi sekondari ya Iwalanje

1.jpg
Mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Iwalanje akijisomea katika moja kati ya chumba cha darasa kilichogeuza bweni shuleni hapo
2.JPG
mmoja kati ya wanafunzi wa shule ya sekondari Iwalanje Mbeya akitoka gheto kuelekea shule

4.JPG
Makamu mkuu wa shule ya sekondari Iwalanje Frank Meck akizungumza na waandishi wa habari waliofika shuleni hapo
3.JPG
Maisha ya geto
WAZAZI wanaosomesha watoto wao katika shule ya sekondari ya Iwalanje kata ya Ijombe wilaya ya Mbeya mkoani Mbeya wamedai kuwa chanzo cha watoto wa kike kukatisha Masomo kwa mimba limechangiwa uamuzi wa serikali kuwatoa wanafunzi hao katika bweni na kuwaacha kuishi katika katika vyumba vya kupanga maarufu Kama magheto .

Hali hiyo umepelekea baadhi ya wananchi wa kijiji hicho cha Iwalanje kutumia mwanya huo kuwarubuni watoto hao wa kike kwa kuwapangisha nyumba zao na mwisho wa siku wamekuwa wakiwataka kimapenzi na kuwageuza wanafunzi hao ni nyumba ndogo .

Wakizungumza na wanahabari kijijini hapo Jana wazazi hao walisema kuwa pamoja na shule hiyo kuendelea kuwa na sifa nzuri ya kufaulisha ila bado mimba kwa watoto wa kike zimeendelea kuwa ni tatizo .

Anna mwanjala alisema kuwa wananchi wa kata hiyo ya Ijombe walikuwa wamejitolea kujenga bweni kwa ajili ya watoto wa kike Kama njia ya kupunguza tatizo la Mimba kwa watoto hao ila serikali iliamua kuwatoa wanafunzi hao katika bweni lao na kuwaweka watoto wa kiume ambao wanasoma kidato cha Tano na sita.

Alisema kuwa uamuzi huo wa serikali kuifanya shule hiyo kuwa high school na kuwatoa watoto wa kike katika bweni lao na kuwaweka wanafunzi hao wa kiume kutoka nje ya kata hiyo ,wao Kama wazazi na wananchi wa eneo hilo ambao walijitolea kujenga bweni Hilo hawajapendezwa .

Hivyo alisema ili kuondoa masikitiko kwa wananchi waliojenga bweni hilo kwa ajili ya watoto wao wa kike wanaotoka vijiji vya mbali na shule hiyo ni vema serikali kutimiza ahadi yake ya kuwajengea bweni watoto hao wa kidato cha kwanza hadi cha nne ambao wamekuwa wakipata shida kwa kupanga katika magheto mitaani.

"kweli tunashindwa kujua uamuzi wa serikali yetu kuwapokonya bweni watoto wa kike na kuwaweka watoto wa kiume wakati sisi wananchi tulijenga bweni hilo kwa ajili ya watoto wetu wa kike Kama njia ya kupunguza tatizo la mimba"

John Samweli amasema kuwa mbali ya baadhi ya wamiliki wa nyumba kijijini hapo kuwageuza wanafunzi hao kuwa ni wake zao wadogo bado baadhi ya vijana wamekuwa wakiwarubuni wanafunzi hao kwa kuwapa vizawadi vidogo Kama chakula ,mboga na miwa .

Alisema kuwa kutokana na baadhi ya wanafunzi kuishi mbali kijiji hicho wamekuwa wakishindwa kurudi Kwao mwisho wa wiki kwa ajili ya kufuata mahitaji na kutoa nafasi kwa vijana hao kuwasaidia mahitaji hayo kwa sharti la kupewa mapenzi.

Kwani alisema katika kijiji hicho kumekuwepo na matukio ya wanafunzi kukatisha Masomo kwa mimba na kesi zinapopelekwa ofisi za serikali za vijiji na kata wahusika wamekuwa wakiachiwa ama kubadilishiwa mashtaka na kupewa Yale ambayo yanaunafuu wa kupewa dhamana .

Aidha alisema kuwa tatizo la watoto wa kike kukaa nje ya shule ndilo limekuwa likichangia kuwepo kwa mazingira hatarishi ya wanafunzi hao kujisomea.

Makamu mkuu wa shule hiyo Frank Meck alikiri kuwepo kwa tatizo la mimba katika shule hiyo na kuwa chanzo ni jamii inyozunguka shule hiyo kutokuwa na mwamko wa elimu.

Meck alisema kuwa shule hiyo inajumla ya wanafunzi 681 Kati yao wasichana ni 317 na kuwa wanafunzi Wanafunzi wavulana 68 ambao ni Wa kidato cha tano na sita ndio wanakaa katika mabweni Mawili yaliyo shuleni hapo.

Alisema kuwa wanafunzi hao wanaoishi bweni ni wale wanaotoka maeneo ya mbali na kata hiyo huku wanafunzi wasichana 20 Kati ya 68 waliokuwa wakiishia bweni wamekuwa wakilala katika vyumba viwili vya madarasa vilivyogeuzwa Kama mabweni ya muda kwa wanafunzi hao.

Kuhusu tatizo la mimba alisema kuwa Kati ya mwaka 2011 hadi sasa jumla ya wanafunzi 7 wameshindwa kuendelea na msomo kutokana na mimba .

Alisema mwaka 2011 wanafunzi wanne walipata mimba na mwaka 2012 wanafunzi watatu akiwemo mwanafunzi mmoja wa kidato cha nne na wawili kidato cha tatu.

Meck alisema pamoja na kuwa idadi kubwa ya mimba zimesababishwa na jamii inayoizunguka shule hiyo pamoja na wafanyabiashara mmoja Kati ya wanafunzi hao Saba waliokatisha Masomo kwa mimba alipewa mimba hiyo na mwanafunzi mwenzake ambaye walikuwa wamepanga katika getho moja mtaani.

Afisa Elimu sekondari katika wilaya ya Mbeya mwalimu Magreth Mbwilo mbali ya kuthitibidha ukubwa wa tatizo hilo la mimba katika shule hiyo ya Iwalanje bado alisema kuwa katika Wilaya hiyo changamoto kubwa ni mabweni kwa wanafunzi na kuwa kati ya shule 27 za sekondari katika wilaya hiyo ni shule mbili pekee ndizo zinamabweni japo bado hayatoshi.

Alisema mkakati uliopo ni kuendelea kujenga Hosteli zaidi na tayari ujenzi wa Hosteli 10 unaendelea katika shule mbali mbali huku Kati ya Hosteli hizo tatu zipo katika hatua ya mwisho.PICHA NA HABARI NA BLOG YA FRANSIS GODWIN(http://francisgodwin.blogspot.com)
 












Haki Elimu HakiElimu

Nini matarajio yako kwa bajeti ya 2012/2013, unadhani vipaumbele viende wapi?

Kaloleni Sekondari: Shule ya kata inayoonesha njia mkoani Arusha




Photo+3-+kaloleni.JPG
 Ile dhana ya kwamba shule zote za kata ziko katika mazingira magumu na hazifanyi vema katika maendeleo ya elimu siyo inaanza kupingwa kwa vitendo,utafiti uliofanywa na mwandishi kutoka HakiElimu mkoani Arusha umegundua kuwa ingawa shule nyingi za kata hazifanyi vyema na kukabiliwa na changamoto lukuki, kuna baadhi ya shule za sekondari za Kata ambazo zina maendeleo mazuri kitaaluma kushinda hata zile shule Kongwe za Serikali na Shule nyingi za binafsi.

photo+1-+kaloleni.JPG Mfano wa shule za kata zinazofanya vema ni shule ya sekondari ya kata ya Kaloleni iliyoko wilayani Arusha. Shule hii ilianzishwa mwaka 1998 ni moja ya shule zinazofanya vema kielimu ambapo katika mtihani wa kitaifa wa mwaka jana wa kidato cha nne , shule hii ilishika nafasi ya 12 kati ya shule 137 za mkoa wa Arusha zilizofanya mtihani huo na kushika nafasi ya 179 kati ya shule  3108 zilizofanya mtihani huo nchini  .Shule hii ilikuwa na jumla ya watahiniwa 179 waliofanya mtihani huo ambapo watahiniwa 15 walipata daraja la kwanza, 17 wakapata daraja la pili, 47 walipata daraja la tatu, 85 wakapata daraja la nne na 15 walifeli kwa kupata daraja 0.
Photo+9-+kaloleni.JPG
Vibao mbali mbali kuonesha sehemu na huduma mbalimbali shuleni hapo



photo+8-+kaloleni.JPG
Baadhi ya magari ya walimu na wageni yakiwa yameegeshwa shuleni hapo kusubiri wamiliki wao wakiwa kazini

Photo+4-+kaloleni.JPG Mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya sekondari Kaloleni, Mrs Machange M.J

Tofauti na shule nyingine za kata , shule hii ina maabara kwa ajili ya masomo ya sayansi ambapo mwandishi alifanikiwa kutembelea maabara za somo la Fizikia, Kemia na Bailojia. Pia jambo lingine la utofauti ni mazingira ya shule kuwa mazuri ikiwemo sehemu ya kuegeshea magari ya wafanyakazi na wageni ambapo mwandishi aliduwazwa na neema aliyoiona ya eneo hilo tofauti ya shule nyingine za kata zenye mazingira magumu. Hii huenda ikawa ni kutoka na mazingira ya shule hii kuwa katikati ya jiji la Arusha eneo la Kaloleni.
photo+5-+kaloleni.JPG
Maabara kwa shule ya sekondari ya Kaloleni si jambo geni kwani zipo maabara za kila somo la sayansi.hii ni maabara maalumu ya elimu ya viumbe (Baiolojia)

photo+6-+kaloleni.JPG
Maabara ya Chemistry

photo+7-+kaloleni.JPG
Maabara ya Physics


Photo+10+-+kaloleni.JPG

Pamoja na mafanikio hayo, shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo mlundikano wa wanafunzi ambapo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 967 wa kidato cha kwanza mpaka cha nne, huku kukiwa na idadi ndogo ya walimu na kulazimika kuajiri walimu waliohitimu kidato cha sita kuokoa jahazi. Pia shule hiyo ni moja ya shule zilizopokea wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika katika kidato cha kwanza ambapo jumla ya wanafunzi watatu walikuwa na maksi mbaya sana katika mtihani uliotolewa kwa kupata maksi chini ya tano katika mitihani iliyofanywa ya kuhesabu kusoma na kuandika kufuatia wimbi kubwa la wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika nchini kuchaguliwa kujiunga na masomo ya Sekondari jambo ambalo lilipigiwa kelele na wadau mbalimbali likiwemo shirika la HakiElimu.

Habari na picha zote na Abraham Lazaro alieyekuwa Arusha





Uhaba wa madawati bado ni changamoto shule za msingi Musoma

Uhaba+wa+madawati.JPG
Wanafunzi wa shule ya Msingi Etaro wakiwa darasani wakimfuatilia mwalimu.wanafunzi wengi katika shule hii wanakaa chini kutokana na uhaba wa madawati.

Wakiwa+wanamsikiliza+Mwalimu+darasani+na
Wanafunzi wakiendelea na masomo yao huku wengine wakitumia magoti yao kama sehemu za kuandikia huku wakiwa wamekaa chini.

Uhaba wa madawati katika shule za msingi na sekondari umeendelea kuumiza vichwa vya wapenda elimu pamoja na wazazi kwa ujumla nchini.

Upungufu wa madawati katika shule za msingi umeendelea kudidimiza kiwango cha elimu nchini huku ukichangia kuongezeka kwa utoro kwa kusababisha wanafunzi wengine kukata tamaa ya kusoma na mazingira ya shule kwa ujumla ambayo si rafiki kwao.

Matokeo ya wanafunzi kukaa chini husababisha wanafunzi kuandika wakiwa wameinama na wengine hata kulala kifudi fudi na wengine kuchuchumaa na hivyo kushindwa kuandika vizuri na pia kuchoka mapema.Hali hii kupelekea matokeo mabaya nyakati za mitihani hasa ya kitaifa.


Wanafunzi+wa+shule+ya+msingi+Etaro+wakiw
Hali halisi ndiyo hii wilayani Musoma vijijini
DSC05238.JPG


DSC05245.JPG
Wanafunzi wengine wakiyageuza madawati mabovu angalau wapate sehemu ya kukaa

DSC05247.JPG
Wengine wanatumia viatu vyao kukalia, na wasio na viatu wanakaa kwenye vumbi

DSC05248.JPG

Habari Katika Picha:Uhaba wa madawati katika shule za sekondari

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu
Sekondari ya Ilulu wilayani Kilwa inaupungufu wa madawati, wanafunzi wengi wanakaa katika benchi, stul za maabar.Shule hii ina upungufu wa madawati na kusababisha baadhi ya wanafunzi kukaa juu ya meza wakikosa sehemu ya kuegemea ili kufanya kazi zao za darasani.

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu
Wanafunzi wakiwa darasani


Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu
Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Sekondari+ya+Ilulu+wilayani+Kilwa+inaupu

Kusoma na kuandika kikwazo Mbarali Mbeya


Philipo-Mulugo1.jpgNAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO PHILIP MULLUGO.

****** 
Habari na Joachim Nyambo wa Kalulunga Community Media-Mbarali
 
Wakazi 18,333  Wilayani Mbarali mkoani Mbeya hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu hali inayozua changamoto kwa serikali na wadau wengine kuwabadilisha wakazi hao ili watambue umuhimu wa elimu kwa watoto wao.
 
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo Kened Ndingo uwepo wa idadi kubwa ya wananchi wasiojua kusoma,kuandika na kuhesabu unachangia kuwepo kwa uelewa duni juu ya umuhimu wa elimu wilayani humo

Ndingo ameyasema hayo  katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa kanisa la Lutherani katika mji mdogo wa Rujewa na kufafanua kuwa pamoja na juhudi kubwa inayofanywa na serikali kuhakikisha kila mtoto anapata elimu stahili,uthamani wa elimu kwa wakazi wa wilaya hiyo unaonekana kushuka siku hadi siku.

Amesema tofauti na maeneo mengine ambako wakazi wanakimbilia elimu kwa kuhakikisha waanawawezesha watoto wao kuipata,wakazi wilayani kwake hawaoni umuhimu huo na imefika waakati sasa hawajali elimu hata kwa watoto wao.

Kwa upande wake ofisa elimu shule za msingi Wilayani humo Rustika Turuka amesema Wilaya imekuwa ikishika kati ya nafasi ya 6 na 8 ya ufaulu kimkoa kati ya wilaya 8 zilizopo mkoani Mbeya katika matokeo ya darasa la saba.

Naye mmoja wa wadau waliohudhuria kikao hicho Ophia Nzobonaliba  amesema tatizo kubwa lipo kwa jamii za wafugaji ambao wamekluwa wakiona bora watoe fidia kwa kutopeleka watoto wao shule na kuwaacha waendelee kuchunga mifugo yao.
 

Madiwani na kitendawili cha elimu maalumu Namtumbo



000000000000000000000000001maalum.jpg

BaadhiyawanafunziwenyeulemavuwaakilikatikaShuleyaMsingiNamtumbo.Uongoziwahalmashauriyawilayahiyounalaumiwakwakutengakiasikidogo cha fedhakuendelezaelimumaalumuwilayanihumo.
Na Vicent Mnyanyika
BARAZA la Madiwani katika Wilaya ya  Namtumbo, mkoani Ruvuma linatajwa kuwa chanzo cha kuzorota kwa elimu maalumu wilayani humo.Kitendo hicho kimesababisha watoto wengi wenye mahitaji maalumu na wenye umri wa kwenda shule,  kubaki nyumbani bila kupata haki yao ya elimu.
Uchunguzi wa Mwananchi  uliofanyika hivi karibuni umebaini baraza la madiwani halitilii mkazo aina hiyo ya elimu kwa kupanga bajeti ndogo isiyorandana na mahitaji halisi ya mipango iliyoanzishwa ya kuendeleza elimu maalumu wilayani humo.
Kwa sasa Wilaya ya Namtumbo ina kitengo kimoja tu cha watoto wenye mahitaji maalumu kilichopo katika Shule ya Msingi Namtumbo  kinachohudumia wanafunzi wenye ulemavu wa akili tu. Kitengo hiki kina mwalimu mmoja na wanafunzi watano wanaohudhuria kati ya 26 walioandikishwa.
Kitengo hicho kilichoanzishwa mwaka 1997  ndicho kitengo pekee kinachoshughulika na utoaji wa  elimu kwa watoto wenye ulemavu katika wilaya nzima, huku kikishindwa kuwahudumia makundi mengine ya wanafunzi wenye ulemavu kama walemavu wa macho na wasiosikia.
Mratibu wa Elimu maalum wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo,  Joseph Chengula anasema changamoto kubwa inayozorotesha elimu maalumu katika wilaya hiyo ni bajeti ndogo inayotengwa na mamlaka husika hususan baraza la Madiwani.
“Labda kwa mwaka huu ndio kidogo imepangwa Sh milioni saba kwa ajili ya elimu maalum. Miaka mingine huwa ndogo sana,  unakuta inapangwa  milioni moja au laki tano,” anasema.
Changamoto nyingine anazozitaja ni pamoja  na upungufu wa walimu wenye utaalamu anaosema kwa sasa wapo wawili tu kwa wilaya nzima. Nyingine ni ukosefu wa miundombinu na vifaa vya kufundishia na  kujifunzia.
Takwimu za mwaka 2011 zinaonyesha kuwa, Wilaya ya Namtumbo ina jumla ya walemavu 252, kati yao wanafunzi 181 ndio wanaosoma katika shule mbalimbali kupitia  elimu jumuishi.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, idadi hiyo inajumuisha wanafunzi 34 wenye ulemavu wa akili, wanafunzi 18 wasioona, 11 wasiosikia, walemavu wa viungo 109 na walemavu wa ngozi tisa.
 Wanafunzi 71 waliokuwa na umri wa kwenda shule hawajaandikishwa na hawapo shuleni,  wakiwamo wenye ulemavu wa akili 21, wasioona mmoja, wasiosikia  11, walemavu wa  viungo 35 na walemavu wa ngozi watatu.
Makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo,  Kassim Ntara anasema halmashauri yake haijawahi kupewa fedha maalumu kutoka serikalini kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wenye ulemavu, badala yake fedha inayotolewa anasema ni ya jumla kwa ajili ya maendeleo ya sekta za elimu, afya na huduma nyinigine.
“Hata hivyo Ntara anasema:  “Katika mwaka mpya wa fedha wa 2012/2013, halmashauri imetenga kiasi cha Sh milioni saba kwa ajili ya kitengo cha walemavu wa akili na kwamba kuna mpango wa kujenga shule moja kwa ajili ya   walemavu kama ilivyoagizwa na Serikali.”
Mwalimu pekee
Mkuu wa kitengo cha walemavu kilichopo katika Shule ya Msingi Namtumbo,  Lezile Kampango anatamani kuomba uhamisho wa kwenda wilaya nyingine,  ili aweze kuitumia taaluma yake vema,  kwani anahisi analipwa mshahara  wa bure bila ya kufanya kazi kama alivyokuwa amedhamiria.
“Natamani kuomba uhamisho kwenda mahali pengine ili elimu yangu niweze kuitumia katika mazingira bora na rafiki kwa wenye ulemavu. Hebu fikiria mimi nawafundisha wanafunzi chini ya mti, wakati wa mvua nakwenda kuwafundishia  nyumbani kwangu. Nimetoa taarifa katika ofisi ya Ofisa Elimu na mkurugenzi,  lakini hakuna hatua zilizochukuliwa hadi sasa,’’anasema.
Anaeleza kuwa ni dhahiri kitengo hicho kimesahaulika kwa kuwa tangu alipopangiwa hapo  mwaka 2005 hadi sasa,  kitengo hakijawahi kupata ruzuku yeyote kwa ajili ya chakula pamoja na mahitaji mengine muhimu kwa watoto .
Anasema mahitaji ya msingi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu hasa wenye ulemavu wa akili ni chakula, vifaa vya kufundishia, madarasa na walimu.
“Watoto kama hawa hawawezi kusoma bila chakula, kwani mwanafunzi akihisi njaa tu anatoka nje na kurudi kwao bila hata ya kuuliza, gari ikipita wote wanatoka na kukimbilia gari. Ukiwa mwalimu inabidi uhakikishe kuna vivutio vya kutosha kuwafanya wafike shule na kukaa darasani,” anafafanua.
Kampango anaeleza kuwa mara nyingine hulazimika kuwafundisha nyumbani kwake na  kuwapatia chakula kwa gharama zake ili waendelee kusoma.
Kinachosikitisha ni kwamba wananchi na Serikali wilayani humo wameshindwa japo kujenga chumba kimoja cha daraa kwa ajili ya watoto hao, hali inayomlazimu kuwafundisha chini ya mti ama nyumbani kwake.
Ruzuku kwa wanafunzi
Ofisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo,  Rhoda Mbilinyi  anasema mbali ya kuwa na kitengo maalumu kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa akili, wanafunzi wengine wamekuwa wakichanganywa na wanafunzi wa kawaida katika shule mbalimbali kupitia mfumo wa elimu jumuishi.
Kuhusu ruzuku anasema japo huletwa kwa kiwango kidogo, wamekuwa wakipokea fedha zinazojumuisha wanafunzi wote bila mgawanyo maalumu kwa ajili ya walemavu.
“Ni kweli wanafunzi wenye ulemavu wanahitaji mazingira rafiki,  vikiwemo vivutio. Katika kitengo cha walemavu Namtumbo kuna vivutio vichache. Wakati fulani walikuwa wanapata uji, lakini hivi sasa uchangiaji umekuwa mgumu,’’anasema na kuongeza:
 Tunahamasisha katika kipindi hiki cha mavuno waanze kuchangia na  mwaka huu katika bajeti yetu tumetenga fedha kwa ajili ya kitengo cha elimu maalumu.’’
Takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (Unicef ) za mwaka 2002,  zilionyeesha kuwa asilimia 98 ya watoto wenye ulemavu katika nchi zinazoendelea,  ikiwemo Tanzania hawapatiwi kabisa elimu jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wao.
Inaelezwa kuwa asilimia hii ndogo inasababishwa na kuwepo kwa shule chache maalumu kwa ajili ya watu wenye ulemavu,   ukosefu wa wataalamu, ukosefu wa vifaa na miundombinu duni isiyokidhi mahitaji  ya watu wenye ulemavu.
Aidha,  sera na sheria nyingi za nchi hizo  hazitaji moja kwa moja au kutoa utaratibu mzuri wa kutoa elimu kuhusu watu wenye ulemavu.

Baadhi ya shule za kata wilayani Kilwa zimeanza kuwekeza katika maabara

24Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+
Wanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari ya Kinjumbi  wilayani Kilwa wakisoma kemia kwa vitendo katika maabara ya shule.Shule hii ipo rtakribani kilometa 70 toka Kilwa Masoko
1Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+y
Hivi ndivyo tukichanganya inatokea kwenye 'test tube'
25Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+
Hii ni result ya huu mchanganyiko.Mananisikia?Mwanafunzi akiwaelekeza wanafunzi wenzake juu ya mchanganyiko alioufanya kwenye 'test tube' na reaction iliyotokea.
8Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+y
Majaribio ya maabara yakiendelea.wanafunzi hawa ni wa kidato cha nne na wanategemea kufanya mtihani wao wa Chemistry,Biology na Physics kwa vitendo.
9Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+y
Embu leye hiyo test tube.ingawa hatuna groves na miwani kwaajili ya kujikinga kama reaction mbaya itatokea.
4Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+y
tunaendelea hivi
10Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+


3Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+y
Unaona inavyokuwa?Tunachanganya hivi

5Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+y

6Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+y

7Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+y

20Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+


23Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+

0Wanafunzi+wa+kidato+cha+nne+sekondari+y
Chumba cha maabara ya shule ya sekondari ya Kinjumbi




Tazama kipindi cha Tafakari Time kupitia ITV leo saa moja kamili jioni kuhusu maisha ya geto kwa wanafunzi

Ongezeko la shule za sekondari za kata limeleta maisha mapya kwa wanafunzi wanaosoma shule hizo.Wanafunzi wengi wanatoka mbali na shule zilipo na hivyo kuishia kupanga vyumba mtaani katika vikundi na kuishi waisha ya kuchangia kila kitu (maisha ya geto).

Maisha ya geto kwa wanafunzi ni njia mbadala ambayo wanafunzi wanatumia ili kukabiliana na uhaba wa mabweni mashuleni hasa shule za kata, maisha haya ya geto yameelezwa kuwa ni chanzo cha kufanya vibaya kwenye mitihani ya taifa, kuzuka kwa tabia mbaya kwa wanafunzi kama uvutaji wa bangi, ngono nzembe zinazopelekea wanafunzi wengi hasa wa kike kuishia kupata mimba.

Fuatana nasi katika mfululizo wa vipindi utakao kufungua macho wewe mzazi, mlezi na serikali juu ya maisha halisi ya watoto wetu huko mashuleni.

Matangazo mapya ya HakiElimu haya hapa

 
Kutokujua kusoma na kuandika mashuleni

 
Udanganyifu katika mitihani 
 
HakiElimu ina matangazo mapya mawili, la kwanza linaongelea wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika(Illiteracy in schools) na la pili linaongelea udanganyifu katika mitihani unaofanywa na baadhi ya shule(Pass no mater what).Shule zinazofanya udanganyifu zimewakilishwa na shule ya msingi Janja janja kwenye tangazo.Tune ITV,Chanel 10,Mlimani TV kwa Television.Radio zinazorusha matangazo haya mapya ni RFA,Clouds FM,Radio 5 Arusha,Abood Media Morogoro,Mlimani FM Udsm,Bomba FM Mbeya,Radio Kwizera Ngara, Ebony FM Iringa,Sibuka FM Maswa na Sport FM Dodoma