Injira
HakiElimu

HakiElimu

Dar Es Salaam , Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Shule za Sekondari wilayani Kilwa mambo safi

1Wanafunzi+wa+sekondari+ya+Mpunyule+wila
Mwanafunzi akifanya mazoezi kwenye kompyuta
2Wanafunzi+wa+sekondari+ya+Mpunyule+wila
Mwanafunzi akiwa anafanya mazoezi kwenye kompyuta
3Wanafunzi+wa+sekondari+ya+Mpunyule+wila
Wanafunzi ndani ya somo la TEHAMA kwa vitendo
4Wanafunzi+wa+sekondari+ya+Mpunyule+wila
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mpunyule wilayani Kilwa wakijifunza somo la TEHAMA kwa vitendo.Shule nyingi nchini zinafundisha somo la TEHAMA kwa nadharia hivyo wanafunzi kubaki na uelewa mdogo wa stadi husika kutokana na kukosa uhalisia wa vifaa vya kufundishia.
6Wanafunzi+wa+sekondari+ya+Mpunyule+wila
 Wanafunzi wa sekondari ya Mpunyule wakiendelea na mazoezi ya Kopyuta.
7Wanafunzi+wa+sekondari+ya+Mpunyule+wila
Huu ni mfano wa kuigwa kwa shule zingine kwani kuwepo kwa mazingira na vifaa vya kufundishia kama vile Kompyuta kunarahisisha uelewa wa wanafunzi. Safi sana shule ya sekondari Mpunyule.

Shule tatu wilayani Kilwa zipo kwenye mpango wa kusaidiwa kompyuta na shirika lisilokuwa la kiserikali la UKENGEE FOUNDATION ambalo toka mwaka 2009, limesaidia zaidi ya wanafunzi 9,000  kusoma  somo la TEHAMA kwa vitendo tofauti na shule zingine za serikali ambao husoma nadharia tuu.

Shule ya Sekondari Mpunyule ni shule ya kata, ina jumla ya kompyuta 20 zinazotumiwa na wanafunzi 264 wa kidato cha kwanza mpaka cha nne.Kutokana na shule kutokuwa na umeme, kompyuta hizi zinatumia umeme wa jua. Shule hii ipo kilometa 105 kutoka kilwa mjini.Hii ni mojawapo ya shule tatu za wilaya ya kilwa zenye vifaa hivi adimu kwa shule nyingi nchini. Shule zingine zenye kompyuta wilayani Kilwa ni Kilwa Day na Ilulu.
Picha zote na Edwin Mashasi aliyekuwa Kilwa.

Haki limu - Pass no matter What

Uploaded with Free Video Converter from Freemake www.freemake.com
Views: 30
0 ratings
Time: 01:16 More in Film & Animation

Haki Elimu - Illiteracy

Uploaded with Free Video Converter from Freemake www.freemake.com
Views: 13
0 ratings
Time: 01:09 More in Film & Animation

Taswira katika Elimu

Watoto wakila miwa huku wakieliekea nyumbani;kutokana na ukosefu wa chakula, wanafunzi huamua kujitafutia chochote cha kula kama walivyokutwa na mpiga picha wetu katika eneo la kanazi mkoani Kagera.


watoto wenye umri wa kwenda shule wakitafuta kuni masaa ambayo wanatakiwa kuwa shule kama kamera yetu ilivyowanasa katika kijiji cha Nyakasibi wilayani Karagwe mkoani Kagera





Mazingira ya kujifunzia ni chanzo cha utoro wa wanafunzi walemavu Namtumbo


2Wanafunzi+walemavu+wa+Hakili+shule+ya+m
Wanafunzi walemavu wa Hakili shule ya msingi Namtumbo wakiwa ofisi ya walimu.Wanafunzi hawa hawana darasa maalumu la kusomea kwani wakati mwingine huchuliwa na mwalimu wao na kuwapeleka nyumbani kwake ili kuwapatia chai na kuwafundishia nyumbani kwake. Ukosefu wa chakula na madarasa ya kusomea kwa wanafunzi walemavu umesababisha wanafunzi hawa kuwa na mahudhurio madogo na wengine kutokuhudhuria kabuisa.

Mwalimu wa kietngo maalumu cha shule ya msingi Namtumbo Bw Lezile Kampango amesema changamoto kubwa katika kituo hicho pekee cha wanafunzi wenye ulemavu wa hakili wilayani namtumbo ni ukosefu wa chakula,vifaa vya kufundishia, madarasa na walimu.



“Watoto kama hawa hawawezi kusoma bila chakula, kwani mwanafunzi akihisi njaa tu anatoka nje na kurudi kwao bila hata ya kuuliza, gari ikipita wote wanatoka na kulikimbilia, ukiwa mwalimu inabidi uhakikishe kuna vivutio vya kutosha kuwafanya wafike shule na kukaa madarasani,” alisema Kampango.


Wanafunzi+walemavu+wa+Hakili+shule+ya+ms


Wilaya ya namtumbo ina kitengo kimoja tu cha watoto wenye mahitaji maalumu kilichopo katika shule ya msingi Namtumbo kinachohudumia wanafunzi wenye ulemavu wa hakili tu.Kitengo hiki kina mwalimu mmoja na wanafunzi watano wanaohudhuria kati ya 26 walioandikishwa.

Kitengo hicho akilianzishwa mwaka 1997 na ndicho kitengo pekee kinachoshughulia kutoa elimu kwa watoto wenye ulemavu katika wilaya nzima ya Namtumbo kwa kuwa hakuna kitengo wala shule ambayo inatoa elimu maalum katika makundi mengine ya wenye ulemavu kama wasioona na viziwi.


Wanafunzi+walemavu+wa+Hakili+shule+ya+ms


 Takwimu za mwaka 2011za zinaonesha kuwa, wilaya ya Namtumbo ina jumla ya walemavu 252, kati yao wanafunzi 181 ndio wanaosoma shule mbalimbali katika elimu jumuishi wakiwemo wenye ulemavu wa akiri 34,wasioona 18,viziwi 11,walemavu wa viungo 109 na albino tisa.
Wanafunzi 71 waliokuwa na umri wa kwenda shule hawajaandikishwa na hawapo mashuleni wakiwemo wenye ulemavu wa akiri 21,wasioona mmoja,viziwi 11,wenye ulemavu wa viungo 35 na albino watatu. 




wanafunzi+wa+shule+ya+msingi+namtumbo+wa



Takwimu za shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia watoto ulimwenguni(UNICEF) za mwaka 2002 zilionesha kuwa asilimia 98 ya watoto wenye ulemavu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hawapatiwi kabisa elimu jambo ambalo ni hatari kwa ustawi wao.

Imeelezwa kuwa asilimia hii ndogo inasababishwa na kuwepo kwa shule chache maalum hapa nchini kwa ajili ya watu wenye ulemavu,ukosefu wa wataalamu,sera na sheria nyingi za nchi hizo  hazitaji moja kwa moja au kutoa utaratibu mzuri wa kutoa elimu kuhusu wenye ulemavu,ukosefu wa vifaa maalum na muhimu vya kuwawezesha kusoma pamoja na miundo mbinu duni  isiyokidhi mahitaji  ya watu wenye ulemavu.



Serikali inasita nini kutumia Kiswahili kufundishia shule za sekondari? 


0000001hakielimu.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Elizabeth Missokia (aliyesimama katikati) akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha Kemia kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili na Kingereza 'Furahiya Kemia'
Na Fredy Azzah - Mwananchi

MJADALA wa lugha gani itumike kufundishia katika shule za sekondari na hata vyuoni, umedumu kwa muda mrefu sasa nchini bila ya kuwapo ufumbuzi mwafaka.


Hata hivyo, watetezi wa Kiswahili wakiwamo  na watunzi wa vitabu wanaendelea na juhudi zao kuthibitisha kuwa lugha hiyo ina uwezo mkubwa wa kutumika kama lugha ya kufundishia shuleni na hata vyuoni.

Mfano mzuri wa juhudi hizo ni uandishi wa kitabu cha somo la Kemia kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kutumika katika shule za sekondari nchini.

“Tukiendelea kukishikilia Kiingereza, hatutatoka hapa asilani. Mbona wenzetu wa Ufaransa, Ujerumani na China wanatumia lugha zao?” anasema  Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya uchapishaji vitabu ya Mkuki na Nyota, Walter Bgoya katika  uzinduzi wa kitabu hicho hivi karibuni.

Anaeleza kuwa  kitabu hicho kiitwacho “Furahia Kemia”, kimeandikwa na jopo la walimu na kimelenga kujibu hoja ya watu wanaodai kuwa Kiswahili hakiwezi kutumika kufundishia shule za sekondari.




"Hiki ni kitabu cha kwanza tu kuandikwa, lengo letu ni kuandika vitabu vya masomo yote ya sayansi kwa lugha ya Kiswahili," anaongeza kusema.

Hata hivyo,  anasema kitabu hicho pia kimeandikwa kwa lugha ya Kiingereza kwa kuwa bado mtalaa wa elimu ya sekondari nchini unaitambua lugha hiyo kama lugha ya kufundishia.
Kwa mujibu wa Bgoya, uandishi wa kitabu hicho kwa lugha zote mbili siyo tu  unaweza kumrahisishia msomaji, lakini pia  unamwezesha mwanafunzi kujifunza lugha       hizo.

"Ni kweli kuwa lugha ya Kiingereza ni tatizo kwa watoto wetu, badala ya kujifunza dhana ya Kemia ama somo jingine, utakuta wanajifunza lugha na ndiyo maana akisoma kidogo, hutafuta kamusi ya Kiswahili ili imsaidie," anabainisha na kuongeza:
"Kamusi hizi wanazotumia ni za lugha siyo za Kemia, kwa hiyo mtoto anashindwa kupata dhana  anayoitafuta.  Lakini kwa kutumia kitabu hiki, kitamwezesha kujua kila kitu kwa ufasaha."

Bgoya anasema licha ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kukikataa kitabu hicho kwa kuwa kimeandikwa kwa lugha ya Kiswahili, tayari kimeshapata baraka na kukubaliwa na wataalamu wa Kemia nchini, Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita)  na Taasisi ya Elimu Tanzania Nchini (TET).
"Wangesema kina upungufu wa kitaalamu tungekibadilisha, lakini wamekikataa tu kwa sababu eti kimeandikwa katika Kiswahili. Tatizo la Taifa hili ni viongozi wetu wa elimu, lugha ni daraja tu la kufikisha maarifa, hivyo Kiswahili kikitumika watoto watayapata vizuri sana maarifa kwa sababu ni lugha wanayoifahamu,"anafafanua.

Kwa upande wake, mtunzi mashuhuri wa vitabu na mwalimu mstaafu wa somo hilo, William Mkufya anasema vitabu vya aina hiyo vitasaidia kuinua kiwango cha wanafunzi kuelewa masomo ya sayansi na kuwasaidia kuwa wabunifu.
Mkufya aliyewahi kufundisha katika shule za sekondari za Mzumbe na Zanaki, anasema mbali na kitabu hicho kuwafundisha watoto dhana za sayansi kwa kutumia lugha mama yao, pia kitawasaidia kujua lugha za  Kiingereza na Kiswahili kwa pamoja.

“Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi imekuwa na kigugumizi cha muda mrefu  kubadilisha mfumo wa elimu na lugha ya Kiswahili kutumika kuwafundisha watoto, lakini hali halisi  tunaiona shuleni jinsi watoto wanavyoteseka,” anasema na kuongeza:
“Hata mwalimu akifundisha kwa Kiingereza ili mtoto aelewe, inabidi afafanue kwa Kiswahili. Mtoto naye anasoma kwa Kiingereza, lakini anakimbilia kamusi ya Kingereza na Kiswahili ili kupata maana. Hata hivyo, hizi kamusi ni za lugha siyo Kemia, kwa hiyo watoto wanapotoka zaidi.”

Aidha, anasema faida nyingine kubwa ya kitabu hicho ni kuwafanya wanafuzi kuwa wabunifu kwa sababu kimeeleza jinsi ya kutengeneza vifaa vya  majaribio ya Kemia  kwa kutumia vifaa vilivyo kwenye mazingira wanamoishi, badala ya kutegemea majaribio ya kwenye maabara ambazo hata hivyo hazipo katika shule nyingi nchini.
Mkurugenzi wa shirika la HakiElimu, Elizabeth Missokia, anasema kuandikwa kwa kitabu hicho ni moja ya ubunifu wa hali ya juu kwa kuwa kimeandikwa na jopo la walimu wa Kitanzania na kwa kutumia lugha wanayoifahamu wanafunzi.
“Unapomfundisha mtoto somo lolote kwa lugha mama, anaelewa vizuri zaidi kuliko kutumia Kiingereza. Hapa kwetu wote ni mashahidi kuwa wanafunzi wanapokwenda shuleni hutumia muda mwingi kujifunza Kiingereza na wakifika kidato cha tatu ndio wanaanza kujifunza dhana za masomo,” anasema na kuongeza:

“Itakuwa ni vizuri sana kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, itaona kuwa huu ni ubunifu na ianze kuufanyia kazi, kwani ni jambo litakalowasaidia watoto wetu.’’
Naye Mchunguzi wa Lugha kutoka Baraza la Kiswahili, Gertrude Joseph anasema asilani kamusi za lugha haziwezi kuwasaidia wanafunzi kujifunza dhana za masomo wanayosoma, hivyo anawahimiza walimu kuandika vitabu  kwa lugha ya Kiswahili ili viwasaidie watoto kuelewa  wanachojifunza.

“Sisi Bakita tunataka Kiswahili kifundishwe kuanzia mwanzo mpaka mwisho, kama kweli tunataka watoto wetu waelewe kile wanachofundishwa. Lugha yetu ndiyo itawasaidia watoto wetu kuwa wabunifu na wagunduzi,”  anaeleza.
Kwa upande wake, mwalimu Euniesta Saru anasema kwa muda mrefu amekuwa akipata tabu kufundisha somo hilo kwa kutumia lugha ya Kiingereza ambayo wanafunzi hawaielewi barabara.

“Wanafunzi wanaotoka shule za mchepuo wa Kiingereza ni afadhali, lakini kwa wanaotoka  shule za kawaida kweli wanapata shida. Ni  vema hivi vitabu vikasambazwa katika shule zote ili vitusaidie walimu na hata wanafunzi,” anasema mwalimu huyo.

Pamoja na kukubali kutokuwapo kwa athari ya kitabu hicho kimatumizi, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inasema haiwezi kukitambua kitabu hicho kwa kuwa kimekataliwa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo ndiyo mamlaka pekee nchini inayotoa ithibati ya vitabu vya kutumika shuleni.
Aidha,  TET yenye jukumu la kuandika na kusimamia mitalaa nchini inasema kuandika kitabu hicho kwa kutumia lugha ya Kiswahili, ni kuvunja utaratibu kwa kuwa mfumo wa elimu ya sekondari unakitambua Kiingereza kuwa lugha ya kufundishia.

“Athari ya moja kwa moja kwenye mitalaa siwezi kusema kama ipo, lakini ninachokiona ni kuvunja utaratibu uliowekwa kwa kuwa lugha ya kufundisha ni Kiingereza,” anasema ofisa wa TET, Habib Fentu.

Mkuki na Nyota na HakiElimu Wazindua Kitabu cha Kemia cha Kiswahili


DADA+BETTY.jpg
 Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia (kushoto) akipokea zawadi ya shukrani kutoka Mkurugenzi Msaidizi wa Mkuki na Nyota Publishers.

BETTY2.jpg
Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia (aliyesimama katikati) akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha Kemia 'Furahiya Kemia' kilichochapishwa kwa Kiswahili.

DADA3.jpg


Mkurugenzi Mtendaji wa Mkuki na Nyota Publishers, Walter Bgoya (kulia) akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia mara baada ya kuzindua kitabu cha Kemia 'Furahiya Kemia' kilichochapishwa kwa Kiswahili.



KAMPUNI ya Uchapishaji wa Vitabu na machapisho anuai kwa mara ya kwanza imezindua kitabu cha somo la Kemia kilichochapishwa kwa lugha nyepesi ya kiswahili. Kitabu hicho kilichopewa jina la Furahia Kemia (Enjoy Chemistry) kilichochapishwa kwa ushirikiano na Taasisi ya HakiElimu kimezinduliwa Mei 9, 2012 na Mkurugenzi Mtendaji wa HakiElimu, Bi. Elizabeth Missokia.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Bi. Missokia alisema kuzinduliwa kwa kitabu hicho kutaleta chachu ya wanafunzi kupenda masomo ya sayansi hasa Kemia ambayo yamekuwa yakiwatatiza wanafunzi wengi kutokana na lugha ya kigeni inayotumiwa.


HADHARA.jpg


Baadhi ya wazazi ambao ni miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Somo la Kemia kwa lugha ya Kiswahili pamoja na Kiingereza uliofanyika jana katika Ukumbi wa Quality Plaza Dar es Salaam.

VITABU.jpg
Baadhi ya nakala za vitabu hivyo vya Furahia Kemia kama vinavyoonekana kwenye picha
Alisema ndani ya kitabu hicho wanafunzi wataweza kusoma na kuelewa vizuri somo la Kemia kwa lugha nyepesi ya Kiswahili jambo ambalo linaibua morali ya wanafunzi kuona masomo ya sayansi ni ya kawaida kujifunza kama yalivyo masomo mengine.
Awali akizungumza kabla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mkuki na Nyota Publishers, Walter Bgoya alisema kitabu hicho kimechapishwa kwa lugha mbili yaani Kiswahili na Kiingereza ili kuwarahisishia wanafunzi kujifunza sayansi ya Kemia kwa lugha mama ya Kiswahili.
Aidha alisema kitabu hicho kimepitiwa na kukubaliwa na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) kwamba kinaweza kutumika kutokana na kuwa na maneno rahisi na sahihi ya Kiswahili ambayo yatawarahisishia wakati wa kujifunza mada anuai za Kemia hasa kidato cha kwanza.

HADHARA.jpg
Baadhi ya wazazi ambao ni miongoni mwa wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kitabu cha Somo la Kemia kwa lugha ya Kiswahili pamoja na Kiingereza uliofanyika jana katika Ukumbi wa Quality Plaza Dar es Salaam.

Pamoja na hayo, Bgoya aliishukuru taasisi ya HakiElimu kwa kusaidia kuchapishwa kwa kitabu hicho na kuwataka wadau wengine waungane na juhudi hizo za kuinua lugha ya Kiswahili katika matumizi ya kufundishia hata masomo ya sayansi.
Naye akitoa maoni yake juu ya kitabu cha Furahiya Kemia mmoja wa walimu wa Sayansi, John Bosco alisema kitabu hicho kitakuwa daraja litakalo wawezesha wanafunzi kuvuka na kuyapenda masomo ya sayansi hasa kemia. Alisema kitabu hicho kina mazoezi ya kutosha kiasi cha kumfanya mwanafunzi apende kujifunza kwa dhati.


Uhaba Wa Walimu Na Madarasa Kero kwa Wanafunzi na Walimu



SHULE+YA+MSINGI+SELOU.JPG

Hili ni mojawapo ya madarasa ya Shule ya Msingi Selous (Darasa la Sita) Wilaya ya Namtumbo hapa wanafunzi wanaendelea na masomo.

MOJAWAPO+YA+MDARASA+YA+SHULE+YA+MSINGI+S

wanafunzi wa darasa la tano wakiwa kwenye darasa la Nyasi katika shule ya msingi Selous wilayani Namtumbo

Mwalimu+wa+darasa+la+awali+Fransis+Ndung

Mwalimu wa darasa la awali, Fransis Ndunguru wa Shule ya Msingi Rwinga Wilaya ya Namtumbo akiwa darasani. Darasa hili ni kibanda cha nyasi wanalotumia watoto.


Na Vicent Mnyanyika, Aliyekuwa - Namtumbo

UHABA wa vyumba vya madarasa ni moja ya changamoto kubwa inayoikabili sekta ya elimu Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma hali inayosababisha kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani humo.
Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni wilayani hapa baadhi ya walimu wanaofundisha katika shule za msingi wilayani Namtumbo wamesema wanatamani kuacha kazi au kuhama kutoka na changamoto nyingi zinazowakabili kwa muda bila ya kupatiwa ufumbuzi. Wanasema kuwepo kwa changamoto hizo za muda mrefu kuchangia kushusha kiwango cha elimu katika shule nyingi za mjini.
Uchunguzi uliofanywa katika shule za msingi Rwinga, Selou, Mkapa na Kidugalo zote kutoka Kata ya Rwinga umebaini shule hizo kukabiliwa na uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa hali inayowalazimu walimu kujenga vibanda vya nyasi ili kuwaepusha wanafunzi kukosa masomo kwa sababu ya uhaba huo wa madarasa.


MWANDISHI+WA+HABARI+TOKA+STAR+TV+NA+RADI

 Mwandishi wa Habari na muwakilishi wa Star TV Radio Free Africa akiwa darasani akishangaa mtindo wa kuchanganya madarasa mawili katika chumba kimoja cha darasa.

WANAFUNZI+WA+MADARASA+MAWILI+SHULE+YA+MS

Wanafunzi wa madarasa mawili wa shule ya msingi Kidugalo (Darasa la tano na la sita) wakiwa katika chumba kimoja cha darasa wakisoma kwa mtindo wa kugeuziana migongo na kufundishwa kila darasa tofauti.Njia hii inatumika sana wilayani Namtumbo ikiwa ni njia ya kukabiliana na uhaba wa vyumba vya madarasa.Shule hii ipo kilometa nne tu toka ofisi za wilaya zilipo.

WANAFUNZI+WA+MADARASA+YA+AWALI+SHULE+YA+


Hali hiyo pia imewalazimu walimu kutumia kutumia vyumba vichache vilivyopo kwa kuwachanganya wanafunzi wa madarasa mawili katika chumba kimoja hali inayotia shaka mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi.
Mwandishi ametembelea Shule ya Msingi Kidugalo na kushuhudia zaidi ya wanafunzi 200, wa kuanzia darasa la tatu mpaka la sita wanasoma katika vyumba viwili vya madarasa huku wakiwa wamegeuziana migongo hali ambayo inachangia kushusha taaluma katika shule hiyo.
Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ina shule za msingi 107 kati ya hizo shule 105 zinamilikiwa na Serikali na shule mbili ni za watu binafsi na mashirika ya dini.

Uzinduzi wa shindano la Insha na Michoro la HakiElimu katika picha



Mwenyekiti wa jukwaa la katiba, Deus Kibamba akitoa ufafanuzi wa shindano la Insha na michoro lenye kichwa cha habari 'Katiba mpya iseme nini kuhusu elimu?' nia ya shindano hili ni kutafuta mawazo ya watanzania wa kada zote juu ya mchakato wa uandikaji katiba mpya na elimu isemweje ndani ya katiba?

KIBAMBA.JPG

Meneja katika idara ya habari na utetezi, Nyanda Shuli akifafanua malengo ya insha na mategemeo ya HakiElimu.Pia alitangaza zawadi kwa washindi watakaopatikana.Hata hivyo ndugu Shuli aliweka sawa kuwa watakaotangazwa mwisho wa shindano ni washindi tuu na si vinginevyo.

media.JPG

Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini maelezo toka kwa watoa maada wa HakiElimu na Jukwaa la katiba huku wakichukua matukio kwaajili ya kuwapasha watanzania.