Fungua
Marafiki wa Elimu Dodoma (MED)

Marafiki wa Elimu Dodoma (MED)

Dodoma, Tanzania

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka (unknown language) kwa Kiswahili. Ona asili · Hariri tafsiri

MED Hewani Kuanzia Mach 2011.

Asasi ya Marafiki wa Elimu Dodoma (MED) inatarjia kuanza kuendesha vipindi vyake vya Radio kuhusu Elimu kuanzia mwezi Machi, 2011. Wanachama wa MED na wadau wote wa Elimu wanakaribishwa kushiriki kwenye vipindi hivyo.

Hayo yameelezwa na Mratibu wa MED Bw. Davis Makundi alipkuwa akiongea na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake. Bw. Makundi amesema vipindi hivyo vitaendeshwa kwa udhamini wa mashirikaya HakiElimu na Uwezo.net yote ya jijini  Dar Es salaam                                                                                        

"Vipindi hivi vitakuwa vya moja kwa moja kutoka studio (Live) na vitaruhusu wasikilizaji walio nje ya studio kupifa simu au kutuma SMS kwa lengo la kuchangia mada au kuuliza maswali alisema" Bw. Makundi.

Vipindi hivyo vitakavyosikika kwa muda wa nusu saa (dk. 30); vitakuwa vikisika kwenye Radio Kifimbo 89.8 inayorusha matangazo yake kwenye masafa ya FM Mkoani Dodoma.            Bw. Davis Makundi

25 Februari, 2011
Ifuatayo »

Maoni (2)

[maoni yamefutwa]
Radhina Kipozi alisema:
Ntakuwa nafuatilia kwa ukaribu sana tovuti yenu! hasa ukurasa wa ''je wajua?"!!! nimependa sana style yenu!!! Keep it up!
9 Machi, 2011 (ilihaririwa 5 Oktoba, 2011)
Glory henry (Currently in Sweden) alisema:
Ninyi ni marafiki wa kweli maana mnaonekana kwenye shida. Taarifa zenu zimekuwa msaada sana katika Elimu ya Tanzania. Kupitia tovuti yenu mim binafsi nimeona hali halisi iliyoko uvunguni mwa kitanda. Kwa hiyo ni changamoto pia hata kwa wadau wa elimu katika mipango ya maendeleo ya elimu (Educational development planning). Keep it up.
12 Februari, 2013

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.