Injira
Marafiki wa Elimu Dodoma (MED)

Marafiki wa Elimu Dodoma (MED)

Dodoma, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

MARAFIKI WAJADILI NAMNA YA KUBORESHA MMES II- MOROGORO


Wawakilishi wa harakati za Marafiki wa Elimu kutoka kanda tatu za Mashariki, Kusini na Nyanda za juu Kusini; walikutana mjini Morogoro kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mustakabali wa Elimu na namna nzuri ya kuboresha ushiriki wa wananchi katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Elimu.

Aidha washiriki hao waliipongeza Serikali kwa juhudi zake za kuboresha kiwango cha Elimu kupitia mipango yake ya maendeleo ya Elimu kama MMEM I&II, MMES I&II na Mafunzo ya Ualimu Kazini (TDMS).

Wanaharakati hao walitambua mafanikio ya mipango hiyo kuwa ni pamoja na kufanikiwa kujenga shule nyingi za msingi na sekondari, ongezeko kubwa la uandikishaji wa watoto katika shule zetu, ongezeko la juhudi za kupeleka pesa shuleni kwa lengo la kuboresha hali ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia katika shule nyingi hapa nchini.               Moja ya Maktaba katika Shule ya Sekondari zilizoko Mkoani Dodoma.

Ushauri ulitolewa na wanaharakati hao kwa serikali kwamba; katika kutekeleza MMES II uliozinduliwa Januari 2011; ambao unalenga kuboresha kiwango cha elimu ya sekondari, uandikishaji wa wanafunzi, mfumo wa uongozi na mfumo wa ukaguzi; ni budi serikali iyafanyie kazi mapungufu yaliyojitokeza kwenye mipango iliyopita.

Walitaja mapungufu yaliyojitokeza katika mipango iliyopita kuwa ni pamoja na udahili wa wanafunzi shuleni ambapo wanafunzi wenye hata chini ya alama 150 walichaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari, watendaji wa mipango hiyo hasa wakuu wa shule, bodi na kamati za shule kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na mipango na kwa kiasi kikubwa wananchi ambao ndio wadau wakuu hawakuelimishwa wala kushirikishwa kama mpango unavyoeleza.Wanafunzi wa darasa la Saba wanaojiandaa kuingia kidato cha kwanza 2012.

Marafki wa Elimu kwa kauli moja waliazimia kuishauri serikali kutekeleza mambo 6 ambayo wanaamini kuwa kama yatafanyiwa kazi ipasavyo; mafanikio chanya yatapatikana katika maendeleo ya elimu haa nchini. Maazimio hayo ni pamoja na:-

  • Serikali ihakikishe kuwa inapeleka fedha za ruzuku mashuleni kwa kiwango cha mpango kwa wakati.
  • Serikali ihakikishe kuwa wadau wote muhimu katika kutekeleza mpangio wanakuwa na uelewa wa kutosha kwa kuelimishwa kuhusu wajibu wao, haki zao na kushirikishwa kikamilifu katika kila hatua yautekelezaji.
  • Serikali ihakikishe kuwa inaimarisha ukaguzi wa ndani na wa nje katika shule na pia ukaguzi huo ufanyike mara kwa mara ili kudhibiti na kubaini ubadhirifu wa rasilimali za shule.
  • Serikali izingatie viwango vya ufaulu vilivyotamkwa  kwenye serra ya Elimu katika kuchagua watoto wa kujiunga na elimu ya sekondari na kuhakikisha kuwa taarifa za maendeleo ya wanafunzi pamoja na matokeo halisi ya mwisho yanakuwa ndio kigezo cha kumchagua mwanafunzi kujiunga na sekondari.
  • Serikali ihakikishe kuwa inaongeza idadi ya walimu mashuleni na kuwapatia walimu mafunzo kazini mara kwa mara na kuboresha mazingira ya walimu hasa wanaofanya kazi maeneo ya vijijini.
  • Serikali ihakikishe kuwa uteuzi wa wasimamizi wa shule unazingatia vigezo vya uteuzi kama miongozo inavyoelekeza; wakuu wa shule wapewe semina za mara kwa mara kwa ajili ya kuboresha utekelezaji wa majukumu yao na kuhakikisha kuwa Bodi na Kamati za shule zinajengewa uwezo wa mara kwa mara ili kuboresha usimamizi wa majukumu yao.

Tamko hili la wanaharakati halina budi kuungwa mkono na wadau wote wapenda maendeleo ya Elimu nchini hasa kwa kuzingatia ushindani wa ubora wa Elimu tunaokabiliana nao hasa katika Muungano wetu wa Jumuia ya Shirikisho la Afrika Mashariki.

12 Nyakanga, 2011
« Inyuma Ahakurikira »

Ibitekerezo (1)

Freadrick Amandus (Tabora) bavuzeko
Hongera sana MED kwa kazi yako nzuri, endelea kuweka taarifa kila wakati nasi tunazifuatilia kwa kina.
12 Nyakanga, 2011

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.