How has the quality of the water where you live been affected by the flooding?
Kuna baadhi ya nyumba nimeona toka mafuriko yatokee mabomba yake hayatoi maji,wakati kabla ya mafuriko zilikuwa zikitoa maji na tulikuwa tukienda kuchota hapo.
Mimi hapa kwa sasa ni mkazi wa muda kwa kuwa serikali inasema mwezi wa pili tuondoke inakuja kuvunja makazi.Hivyo vyanzo vya maji viwe vimeathiriwa au la,hali kadharika vyanzo vya maji hili si swala la kufikiriwa.Hata kama kungekuwa na uharibifu,serikali haiwezi kuja kufanya maboresho sehemu ambayo inataka kuvunja nyumba.
Vyanzo vya maji haviwezi kukosa kuathiriwa katika mafuriko haya wala ubora wa maji.Isipokuwa sijafanya utafiti wa hali ya sasa na hali kabla ya mafuriko.
Jaribu kuuliza kwa wale ambao nyumba zao hazikuathiriwa na mafuriko.Wao wanaweza kukueleza habari za vyanzo vya maji.Mimi nafikiria nitaenda wapi serikali ikija kuvunja nyumba hizi.
Sijui maana nipo eneo hili lakini akili yangu haipo tena eneo hili.
Eneo hili unajua nyumba zinabomolewa,na mimi nilikuwa mpangaji.Sijafuatilia.
Wake zetu walipata shida ya kutafuta maji ya bomba nyakati za mafuriko.Kidogo naona kuna unafuu kwa wakati huu.Hiki nadhani ni kiashiria kwamba vyanzo vya maji viliathiriwa na mafuriko.Yawezekana serikali imechukua hatua.Ila bila hata mafuriko,mabibo maji ya bomba ni tatizo.
Sielewi kama vimepata athari au la kwa kuwa maji ya mabomba yanatoka kwa nadra toka hata kabla ya mafuriko.Labda wanawake ambao ni wachotaji maji wanaweza kugundua kama kuna athari.
Kulikuwa na shida kubwa ya maji ya bomba kipindi kile cha mafuriko lakini hali imerudi kama kawaida.
Kulikuwa na mabomba yalikatwa na mafuriko,hali ya maji ya bomba ikawa mbaya sana nyakati za mafuriko.Tulitegemea maji ya kununua ambayo ni maji chumvi lakini idara ya maji walikuja kutengeneza baadaye.
Maji kwa ujumla siyo mazuri, kutokana na kwamba mafuriko hayo yaliharibu visima vingi hapa kwenye mtaa wetu, kiasi kwamba sasa hivi inatubidi kwenda masafa marefu kwa ajili ya kutafuta maji.
Kwa ujumla ubora wa maji hakuna, maana mafuriko yameharibu vyanzo vya maji, pia maji haya yatakuwa yamechafuliwa na maji machafu hasa yanayotoka vyooni, sasa hii ni hatari kwa afya zetu.
Huduma ya maji baada ya mafuriko limekuwa na changamoto nyingi kutokana na uharibifu wa miundo mbinu kwa maana kwamba watu wa mtaa huu walikuwa wanategemea zaidi maji ya visima, lakini baada ya mafuriko hayo visima vingi vimeharibika ambapo vilivyokuwa na matenki baadhi ya matenki hayo yaling`olewa na mafuriko.
Mafuriko haya yamechafua maji ya matumizi, kwa maana kwamba maji yaliyopo sasa ni machafu hayafai kwa matumizi, hali ngumu kwa sababu maji ya visima yamechanganyika na maji ya vyooni, maana kipindi cha mafuriko vyoo vingi vilijaa maji na vingine vilibomoka kabisa, uchafu mwingi kutoka vyooni uliingia kwenye visima vya maji, sasa unaweza kuona jinsi tulivyo na maji machafu kwa sasa, hali siyo shwari.
Kwa kiasi kikubwa vyanzo vya maji vimeharibika, maana mafuriko hayo yameharibu miundo mbinu ya maji, hivyo kwa sasa swala la maji ni gumu.
Maji tunayotumia sio salama, mabomba yamechukuliwa na mafuriko na maji yanayotumika ni ya mitaani ambayo ni machafu sana.
mabomba yamesombwa na mafuriko
kuna baadhi ya maeneo vyanzo havijaharibika sana.
maji bado hayajawa katika hali yake ya kila siku
« Back to report