Envaya

Envaya

Dar es Salaam Flooding Community Survey

How did the flooding affect your own property and possessions?

Mali zangu za ndani zilipotea,na kuharibika kama tv redio, friji, komputa, cherehani 3, vyombo vya jikoni, vitanda ,magodoro,nguo,vifaa vya shule vya watoto 4 nguo za wateja za sikukuu ya krismas na mwaka mpya 2012
ukuta wa uzio wa nyumba ulibomoka ,mali zote za ndani zimepotea,Tv,radio, friji,vitanda ,magodoro, mashuka ,vifaa vya shule vya watoto pamoja na vyeti vyangu vya shule, vyeti vya kuzaliwa vya watoto, vyombo vya jikoni, maturubai na machuma yake yalipotea, vifaa vya kuhifadhia maji, masanduku ,pesa za karo na kununulia mahitaji ya watoto laki nane{800,000)
Nyumba yangu imeharibika kwa sababu maji yalidumu ndani kwa muda wa wiki moja hivyo kumong,onyoka kidogo kidogo,mali zote za ndani zimeharibika,zikiwamo komputa,tv friji, redio ,cherehani, vifaa vya shule vya watoto wangu,makabati yanahitaji matengenezo,vitanda,magodoro hivyo vimepotea kabisa.
Baiskeli 2 za biashara. vifaa vyote vya ndani, tv,radio , makabati 3 , magodoro, vitanda, nguo ,vyombo vya jikoni, mifugo yangu yote ,ambayo ni , kuku waliokuwa wametaga mayai,kanga,na bata.
pikipiki yangu iiondoka na maji ambayo ilikuwa inafanya kazi ya boda boda {biasharaa].vitu vyote vya ndani kupotea makabati.magodoro,sofa,tv,friji,nguo,vifaa vyote vya jikoni vilielea juu ya maji ,vifaa vya shule na pesa ya mchezo laki tano ambayo niliiweka ndani kwa ajili ya kumkabidhi mwenyewe tarehe 24 dec
Vitanda, magodoro ,deepfreezer 2 za biashara , tv,radio friji,kabati 2 la vyombo na nguo,
nguo za familia ya watu 7 zimepotea, ukuta wa nyumba umeathirika kwa maji yaliyo dumu kwa siku 20.pesa taslim laki mbili za karo ya shule ya mtoto wangu kupotea
All human basic needs has been taken away by the flood.
ukuta wa nyumba kubomoka,vifaa vyote vya ndani ,vitanda 2,kabati 1, vifaa vya kuhifadhia maji, Radio, tv. nguo zote za famila yangu yenye watu 6, kamera yangu ya digital ambayo ndio ofisi i yangu kupotea ikiwa na picha za wateja,picha za wateja za harusi zenye thamani ya laki tatu kuharibika,raptop 1 nayo kupotea
Vitanda vitatu vimesombwa na maji, magodoro, pesa taslimu shilingi 130,000, nguo za wakubwa na watoto zimesombwa na maji pamoja na vyombo vya ndani.
Kabati 2 zimeharibika,Radio,friji,tv,vyombo vyote vya jikoni,genge langu lote lenye thamani ya laki nane na arobaini limepotea,pesa taslim laki moja na ishirini zimepotea kwenye suluali ,mashuka, magodoro ,mito, na mbuzi wangu watatu.kisima kubomoka
Magodoro, Nguo , Vyombo vya ndani, Vitabu ,Chakula na unifom za shule za wanafunzi,
Tv,Radio,Friji, vitanda vinne,makochi ,magodoro,nguo zote za watoto na za kwetu na mke wangu ,vifaa vya shule vya watoto wa tatu unifom,vitabu, madaftari vyombo vya jikoni vyote,sina hata kijiko,pesa taslim kiasi cha laki tano na thelathin elfu..
Nyumba imebomoka na mafuriko,vitu vyote vya ndani vimechukuliwa na maji,sare za shule za wanafunzi zimesombwa na maji, nguo zimechukuliwa na maji.
« Previous questionNext question »

« Back to report