Envaya

Envaya

Dar es Salaam Flooding Community Survey

What is your neighborhood's most important need right now?

Watu wengi wanaoishi eneo hili wameathirika sana na mafuriko haya, siku ile ya mafuriko nyumba nyingi zilijaa maji na kusababisha mali nyingi kuharibika na kupotea, baadhi yetu sasa hatuna sehemu ya kuishi, hivyo nionavyo mimi ni kwamba tupatiwe mahitaji muhimu na ya dharura mfano tupewe malazi mf magodoro, vyakula, nguo, n.k.
Kwa sasa mtaa unahitaji sana kuwe na mifereji au njia za kupitisha maji, maana hakuna mifereji ya maana inayoweza kupitisha maji kwa urahisi na kuweza kuzuia mafuriko yasitokee.
Chakula, mavazi kwa jamii na wanafunzi,mitaji ya biashara zao ndogondogo na mahitaji madogomadogo.
A bridge linking us to the main road (The previous was washed by the floods
Ningependa watu wote wa mtaa huu tuhamishwe kwenye haya maeneo,na pia serikali itupatie mtaji wa kujenga kwenye viwanja wanavyotupa,pia watupe misaada ya mitaji tuanze biashara upya.
Tuboreshewe mazingira ili tuweze kuishi vizuri,kama vile tusafishiwe mitalo ili maji yaliyotwama yaondoke ili kuepusha magonjwa ya milipuko.Kuna msemo unasema kwako ni kwako tu.
« Previous questionNext question »

« Back to report