TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION
OFISI YA MKURUGENZI MKUU
TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI
YAH: KUFUNGWA KWA MFUKO WA ELIMU YA JUU WA SHIRIKA LA TSSF
Hii ni kuutarifu umma wa wanachama wa Shirika la TSSF, wadau wa Shirika la TSSF, waombaji wote walioomba mikopo nafuu ya elimu kutoka Shirika la TSSF, vyombo vya habari, na umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla kwamba, kwa kuzingatia utamaduni, misingi, na mila za utii wa raia kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kwa kuzingatia kauli ya Serikali iliyotolewa mnamo tarehe 14 Novemba 2017 na Mhe. William Tate Ole Nasha ambaye ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo kauli hiyo ilisimamisha mara moja shughuli za utoaji mikopo zilizokuwa zinafanywa na Shirika la TSSF;
Kwa kuzingatia masharti ya kauli hiyo, ikiwa ni pamoja na kutii na kuiheshimu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Shirika la TSSF limesalimu amri kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kufunga rasmi Mfuko wa Elimu ya Juu wa Shirika la TSSF ambao ndio uliokuwa na wajibu wa kutoa mikopo nafuu ya elimu, ufadhili wa masomo ya elimu ya juu, gharama za matumizi wakati wa kuhudhuria masomo ya elimu ya juu, na punguzo la ada ya masomo ya elimu ya juu. Mfuko huo umefungwa rasmi kuanzia leo tarehe 18 Desemba 2017.
Sababu za kufungwa kwa Mfuko wa Elimu ya Juu wa Shirika la TSSF ni;
1. Amri ya Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Jamhuri ya Muungano ambayo imetaka kusimamishwa kwa Shughuli za Utoaji Mikopo nafuu ya elimu ya Juu kutoka Shirika la TSSF.
2. Amri ya Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambaye amesimamisha shughuli zote za Shirika la TSSF ili kupisha uchunguzi unaofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya tuhuma za utapeli zinazolikabili Shirika la TSSF.
3. Akaunti za Shirika la TSSF kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi ambapo Jeshi la Polisi limeomba amri ya Mahakama ili kuendelea kushikilia akaunti za Shirika la TSSF kwa miezi sita zaidi. Endapo kama Shauri hilo litasikilizwa na Jeshi la Polisi kuendelea kushikilia akaunti hizo, tafsiri yake ni kwamba akaunti hizo zitashikiliwa mpaka mwishoni mwa mwezi Juni 2018.
4. Kusimama na Kuchelewa kwa utekelezaji wa taratibu za kuhakiki fomu za maombi ambazo zilikuwa zimekusanywa, kuzipangia mikopo nafuu au aina nyingine ya ufadhili, pamoja na kuchakata miamala ya malipo ya mikopo nafuu kwa walengwa, pamoja na malipo ya ada kwa vyuo husika.
Ni dhahiri kwamba, muda umekwenda sana na kwamba kwa sasa wanafunzi wanakaribia kufanya mitihani wakati ambapo Shirika la TSSF halina uwezo wala nyenzo za kuwezesha lolote kutekelezeka kwa wakati kutokana na Serikali kuweka zuio na kushikilia nyenzo zote ambazo Shirika la TSSF lilikuwa likizitumia katika kufanya shughuli zake.
Kutokana na uamuzi huo wa kufunga shughuli za Mfuko wa Elimu ya Juu, na baada ya kufanya tafakuri ya kina, Shirika la TSSF limeona kuwa hakuna sababu ya kugombania fito au tofali wakati nyumba tunayoijenga ni moja. Kwa mantiki hiyo, Shirika la TSSF limeamua kufanya yafuatayo;
1. Kuungana na Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa njia ya kuwezesha upatikanaji wa fedha zitakazowezesha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ya Jamhuri ya Muungano kuwahudumia Wanafunzi Wengi Zaidi
Shirika la TSSF linatangaza nia yake hadharani ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kugharamia mafunzo ya elimu ya juu kwa njia ya kuwezesha kupatikana kwa fedha ambazo zitatunisha mfuko wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na hivyo kuifanya Bodi hiyo kuweza kuhudumia wanafunzi wengi zaidi. Uwezeshaji huo ni pamoja na kubuni programu mbalimbali ambazo zitawezesha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi na hivyo kuweza kufikia malengo ya kuhakikisha kuwa kila Mtanzania mwenye sifa za kupata elimu ya juu anapata elimu hiyo. Katika kufanikisha azma hiyo, Shirika la TSSF litafanya maandikiano na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kuweza kufanikisha mazungumzo, taratibu na masuala mengine ambayo yatawezesha kufanikiwa kwa azma hiyo chini ya Mpango wa Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi yaani (Public – Private Partnership).
Ni imani ya Shirika la TSSF kwamba, kwa kuwa Serikali yetu ni sikivu, inayojali wanyonge, na iliyojizatiti katika kukuza na kuwezesha ukuaji wa sekta binafsi hapa nchini, itatupokea kwa furaha na itatushauri, kutukosoa pamoja na kutuongoza vyema ili kuhakikisha kwamba, azma hiyo inafanikiwa, na inatekelezeka kwa ajili ya ustawi wa elimu ya juu hapa nchini. Ni imani yetu kwamba, kama mapokezi ya nia hii yatakuwa mazuri kama tunavyotarajia, matunda ya utekelezaji wa azma hii yataanza kuonekana kuanzia Mwaka ujao wa masomo wa 2018/2019.
2. Kurejesha Malipo Mbalimbali yaliyopokelewa na Shirika la TSSF kwa niaba ya ya Mfuko wake wa Elimu ya Juu
Kwa kuzingatia masharti ya kanuni za uanachama wa Shirika la TSSF, 2014 hasa Fungu la 18, 19, 20(b), 21(b), 23, 24(b), 27, na 28 zote yakisomwa kwa pamoja, yafuatayo yatafanyika;
2.1 Kwa kuwa wote ambao waliomba mikopo ya elimu ya juu kutoka TSSF ni wanachama halali wa Shirika la TSSF kutokana na kulipa ada ya fomu ya maombi kama inavyoelezwa kwenye Fungu la 19, 20(b), 21(b) na 23 la Kanuni za Uanachama wa Shirika la TSSF, toleo la Mwaka 2014 watastahili kurejeshewa malipo mbalimbali yaliyokusanywa kutoka kwao endapo kama wataamua kujiondoa kwenye Shirika la TSSF kama inavyofafanuliwa kwenye Fungu la 27 na la 28 la Kanuni za Uanachama za TSSF toleo la 2014. Wale watakaopenda kuwa wanachama wa TSSF kwa hiari yao wenyewe hawatazuiwa kufanya hivyo.
2.2 Fedha zote zilizolipwa kwa Shirika la TSSF kama ada mbalimbali za kuombea mikopo, zipo kwenye akaunti za Shirika la TSSF na zipo salama. Kwa kuwa akaunti hizo zinashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya uchunguzi, Uongozi wa Shirika la TSSF hauwezi kufanya muamala wowote iwe ni kuweka au kutoa. Kwa mantiki hiyo, TSSF haiwezi kufanya marejesho yoyote ya fedha kwa wanachama wake kwa sasa. Kwa kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na Uchunguzi wake dhidi ya tuhuma za Utapeli dhidi ya Shirika la TSSF, na kwa kuwa Maafisa wa Shirika la TSSF hawawezi kufanya shughuli yoyote kwa sasa kutokana na Ofisi za TSSF kufungiwa kwa muda na Msajili, na kwa kuwa TSSF inatambua kwamba wapo wanachama wake ambao walilipa ada za fomu lakini fomu zao hazikuwa zimefika TSSF kutokana na sintofahamu kadhaa zilizojitokeza hivi karibuni, utaratibu wa kurejesha malipo yote kwa wale watakaojiondoa TSSF utakuwa kama ifuatavyo;
2.2.1 Uongozi wa Shirika la TSSF utaharakisha jitihada zake za kuhakikisha kuwa Ofisi zake zinafunguliwa na huduma ka kiofisi na kiutawala ambazo siyo za utoaji wa mikopo zinarejea kama kawaida.
2.2.2 Baada ya huduma za kiofisi kurejea, na akaunti za Shirika la TSSF kufunguliwa, Shirika la TSSF litatoa fomu ya madai (Claim Form) ambayo itajazwa na wale wote ambao walilipa malipo mbalimbali kwa TSSF kisha TSSF itahakiki madai hayo na kuyalipa kwa wahusika.
2.2.3 Wale ambao watapenda kuendelea kuwa wanachama wa TSSF watajaza fomu za kuhuisha taarifa zao.
2.2.4 Kuhusu suala la ni lini malipo hayo yatakapoanza kulipwa, ni mpaka pale Jeshi la Polisi litakavyo achilia akaunti za TSSF. Taarifa kuhusu kufunguliwa kwa akaunti hizo, na kuanza mchakato wa madai na malipo zitatangazwa hapo baadae.
3. Kuhusu Barua zilizoandikwa vyuoni kama Dhamana kwa Waliokuwa Wamepangiwa Mikopo katika Awamu ya Kwanza
3.1 Barua Zilizowasilishwa Vyuoni kama Dhamana
Shirika la TSSF litaviandikia vyuo vyote ambavyo viliandikiwa barua za dhamana, kusitisha dhamana hizo kutokana na kufungwa kwa Mfuko wa Elimu ya Juu wa Shirika la TSSF. Wale wote ambao walikuwa wamepewa barua hizo za dhamana pamoja na wale wote waliokuwa wameomba mikopo nafuu ya elimu kutoka TSSF wanashauriwa kutafuta vyanzo vingine vya ufadhili ili waweze kugharamia masomo yao.
3.2 Waliokuwa Wamepangiwa Mikopo katika Awamu ya Kwanza
Hii ni kuwataarifu wale wote ambao walikuwa wamepangiwa mikopo nafuu ya elimu katika awamu ya kwanza kwamba, mikopo yao imefutwa kutokana na kufungwa kwa Mfuko wa Elimu ya Juu wa Shirika la TSSF. Wale wote ambao walipangiwa mikopo hiyo nao wanastahili kurejeshewa malipo yote ambayo walikuwa wamelipa kwa TSSF kama watajiondoa kwenye Shirika la TSSF na wanashauriwa kutafuata ufadhili wa masomo yao kutoka kwenye vyanzo vingine ili waweze kugharamia masomo yao.
4. Maendeleo ya Shirika la TSSF
Kwa kuzingatia misingi ya historia ya Shirika la TSSF tangu Mwaka 2011, Shirika la TSSF litaendelea na shughuli zake za kuboresha huduma za afya, uchumi hasa kwa vijana, utalii na utawala bora.
Imetolewa na:
Donati Primi Salla
MKURUGENZI MKUU
18 Desemba 2017
TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION
OFISI YA MKURUGENZI MKUU
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA
YAH: KAULI YA SHIRIKA LA TSSF DHIDI YA TAMKO LA WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUHUSU SHIRIKA LA TSSF
Shirika la Tanzania Social Support Foundation linakiri kupokea tamko la Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia lilitolewa na Mhe. Profesa Joyce Ndalichako katika majibu yake kwa Mhe. Cosato David Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini, aliyeomba mwongozo kuhusu uhakika wa Shirika la TSSF katika kutoa mikopo nafuu ya elimu kwa wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kufutia matangazo ya Shirika la TSSF yaliyotolewa hivi karibuni yakialika wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu kuomba mikopo hiyo. Tamko hilo linakwenda sanjari na taarifa kwa umma iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, leo Ijumaa Novemba 10, 2017. Kimsingi taarifa ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekiri kutokufahamu Shirika la TSSF na kuwataka wananchi kuupuza taarifa zinazotolewa na Shirika la TSSF.
Shirika la TSSF limeshtushwa na kusikitishwa kutokana na namna ambavyo juhudi zake za kuwasaidia watoto masikini wa kitanzania kupata elimu ya juu ambayo ni haki yao ya kimsingi na ya kikatiba zinavyominywa na kuzodolewa kila kona ya nchi hii kutokana na hisia hasi za kitapeli. Jambo hili linaikatisha tamaa sekta binafsi hapa nchini katika kusukuma gurudumu la maendeleo hasa katika kipindi hiki ambapo nchi yetu inapigana vita vya kiuchumi kama inavyofafanuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Shirika la TSSF limepokea tamko la Mhe. Waziri Prof. Joyce Ndalichako kwa niaba ya Serikali kama tamko ambalo limetolewa kwa kutahayari katika hali ya taharuki na tahamaki kutokana na kutokuwa na taarifa za kina kuhusu Shirika la TSSF kwa sababu mapema leo asubuhi, Ofisi Ndogo za Shirika la TSSF zilizopo Jijini Dar es Salaam zilipokea ugeni wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutoka Makao Makuu ya Wizara hiyo yaliyopo Mkoani Dodoma ambao uliongozwa na Ndugu Moshi J. Kabengwe, ambaye ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu na Mhe. Wakili Msomi Patricia M.K Maganga ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria, wote wakiwa ni watumishi waandamizi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Ugeni huo umekagua Cheti cha Usajili wa Shirika la TSSF, Katiba ya Shirika la TSSF, Andiko la Mradi wa Mfuko wa Elimu ya Juu wa Shirika la TSSF, Mkataba wa Shirika la TSSF na mfadhili wake ambao ndio chanzo cha fedha zinazotolewa kwa wanufaika wa Mfuko wa Elimu ya Juu wa Shirika la TSSF pamoja na nyaraka ambazo zinashuhudia uwepo wa Shirika la TSSF tangu Mwaka 2011 mpaka sasa. Ushahidi wa ugeni huo kufika ofisini kwetu, upo katika Kitabu cha Wageni Maalum wa Shirika la TSSF walichokisaini leo Ijumaa Novemba 10, 2017 ambapo baada ya kijiridhisha na taarifa hizo pamoja na uhai wa Shirika la TSSF, waliagiza kutolewa nakala kivuli za nyaraka zote muhimu za Shirika la TSSF ili waziwasilishe kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Aidha, ni jambo la kawaida kabisa kwa mtu kuhoji uhalali wa kitu fulani pale anapotilia shaka na kwamba; Shirika la TSSF linathibitisha uhalali wa kufanya shughuli zake kutokana na sababu zifuatazo;
- 1. Uhalali wa Kisheria
Shirika la TSSF limesajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali, Sura ya 56, ya Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama ilivyofanyiwa marekebisho mnamo mwaka 2005 kupitia Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Amendment of Miscellaneous Written Laws) Na. 11 ya Mwaka 2005. Aliyelisajili Shirika la TSSF ni Msajili wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vilevile Cheti cha Usajili wa Shirika la TSSF kinatoa maelekezo kwamba, TSSF itafanya kazi katika mikoa yote ya Tanzania Bara, na itajiendesha kwa mujibu masharti ya Katiba yake. Namba ya Usajili wa Shirika la TSSF ni 00NGO/00006998. Cheti hiki ndicho kinachotoa uhalali wa Shirika la TSSF kufanya kazi zake katika umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 18 cha Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya Mwaka 2002 ambacho kinasema ;
“18(1) A certificate Of registration shall be a conclusive evidence of the authority to operate as specified in the constitution or in the certificate of registration
18(2) A registered Non-Governmental Organization shall, by virtue of registration under this Act, be a body corporate capable in its name of;
(a) Suing and be sued.
(b) Acquiring, purchasing or otherwise disposing of any property, movable or immovable;
(c) Entering into contract; and
(d) Doing or performing all acts which can be done by a body corporate and which are necessary for proper performance of its duties and functions.”
Malengo ya TSSF yaliyotajwa katika Ibara ya 13(iv) ya Katiba ya TSSF toleo la Mwaka 2014 yanasema kwamba;
“To promote the higher educational welfare and all matters related to educational welfare in Tanzania”
Vilevile Ibara inayofuatia ya 13(v) ya Katiba ya TSSF toleo la Mwaka 2014 inasema kwamba,
“To establish the educational plans and institutions that shall help the poorest people to get education in affordable ways”
Masharti hayo ya Katiba ya TSSF ambayo yametajwa hapo juu, yanalindwa na Kifungu cha 30(1) cha Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya Mwaka 2002;
“30. -(1) The constitution and other documents submitted by founder Governing members to the Registrar at the time of making application for registration documents or any subsequent constitution and documents submitted to the Registrar shall be the governing documents in respect of such Non-Governmental Organization.”
- 2. Utoaji wa Mikopo Nafuu ya Elimu kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu chini ya Mfuko wa Elimu ya Juu Shirika la TSSF
Mfuko wa Elimu ya Juu wa Shirika la TSSF unaendeshwa chini ya Katiba ya TSSF kama ibara zake zilivyoainishwa hapo na umelenga kuwasaidia wenye uhitaji. Swali ambalo limekuwa likiwatatiza watu wengi ni kwamba, Je, NGO inaweza kutoa mikopo nafuu? Jibu lake ni kwamba, kwa mujibu wa Sheria za Tanzania inawezekana. Sheria ya Kodi ya Kipato (The Income Tax Act, Cap.332 R.E 2008) inatambua shughuli zote za kipato zinazofanywa na mashirika yasiyo ya kiserikali kama biashara ya ukarimu “Charitable Business” ambayo inatozwa kodi. Hii ni kwa mujibu wa Kifungu cha 64 cha Sheria ya Kodi ya Kipato.
64.-(1) A charitable organisation or religious organisation shall be treated as conducting a business with respect to its functions referred to in subsection (8) as the "charitable business".
(2) For the purposes of calculating the income of a charitable organisation or religious organisation for any year of income from its charitable business –
(a) there shall be included, together with any other amounts required to be included under other provisions of this Act, all gifts and donations received by the organisation; and
(b) there shall be deducted, together with any other amounts deductible under other provisions of this Act –
(i) amounts applied in pursuit of the organisation or religious organisation’s functions referred to in subsection (8) by providing reasonable benefits to resident persons or, where the expenditure on the benefits has a source in the United Republic, persons resident anywhere; and
(ii) 25 percent of the organisation or religious organisation's income from its charitable business (calculated without any deduction under subparagraph (i) and any investments.
(3) This subsection shall apply to any amount applied by a charitable organisation or religious organisation during a year of income other than in the manner referred to in subsection (2)(b)(i) or as a reasonable payment to a person for assets or services rendered to the organisation by the person.
(4) Where subsection (3) applies –
(a) the organisation or religious organisation shall be treated as conducting a business other than its charitable business; and
(b) the sum of amounts to which that subsection applies for the year of income less any income of the organisation or religious organisation from a business other than its charitable business or business referred to in paragraph (a) shall be treated as income of the organisation or religious organisation that has a source in the United Republic derived during the year of income from the business referred to in paragraph (a).
(5) Notwithstanding the provision of section 19, a charitable organisation or religious organisation -
(a) may not set any loss from its charitable business against its income from any other business; and;
(b) may only set losses from any other business against income from any such other business.
(6) Where a charitable organisation or religious organisation ceases to be a charitable organisation or religious organisation during a year of income –
(a) the organisation or religious organisation shall be treated as conducting a business other than its previous charitable business; and
(b) there shall be included in calculating the organisation or religious organisation’s income for the year of inccome from the business referred to in paragraph (a) any amounts claimed as a deduction under subsection (2)(b)(ii) during that year of income or any prior year of income during which the organisation was a charitable organisation or religious organisation.
(7) Where a charitable organisation or religious organisation wishes to save funds for a project that is detailed in material particulars and which the organisation is committed to, the organisation or religious organisation may apply to the Commissioner and the Commissioner may approve the saving as meeting the requirements of subsection (2)(b)(i):
(8) For the purposes of this section, “charitable organisation” means a resident entity of a public character that satisfies the following conditions:
(a) the entity was established and functions solely as an organisation for:
(i) the relief of poverty or distress of the public;
(ii) the advancement of education; or
(iii) the provision of general public health, education, water or road construction or maintenance; and;
(b) the entity has been issued with a ruling by the Commissioner under section 131 currently in force stating that it is a charitable organisation or religious organisation.
Kifungu hicho kinasomwa pamoja na Tafsiri ya maana ya NGO kama ilivyotafsiriwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 11 ya Mwaka 2005 ambacho kinatafsiri NGO kama taasisi ambayo inaweza kufanya shughuli za kipato bila ya kugawana faida isipokuwa kuelekeza faida hiyo katika shughuli zinazonufaisha umma.
Kwa mantiki hiyo, mikopo nafuu ya elimu ambayo inatolewa na TSSF ni halali.
- 3. Uhalali wa TSSF kutoza Gharama za Huduma zake
Gharama ambazo zinatozwa kwa minajili ya upatikaji wa huduma za TSSF ni sehemu ya kuinua mfuko wa Shirika la TSSF ili liweze kujiendesha, kuwa endelevu na kutoa huduma kwa umma. Gharama hizo zinatozwa kwa mujibu wa Ibara ya 10(viii) ya Katiba ya TSSF toleo la Mwaka 2014 ambayo inasema;
“To solicit and receive fund within and outside Tanzania, receive grants in cash or kind, and charge an appropriate fee in provision of services with a view to enhance development, expansion, and/or rehabilitation of the Organization”
Ibara hii inasomwa pamoja na Kifungu cha 32 cha Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya Mwaka 2002;
“32. Non Governmental Organization registered under this Act shall be entitled to engage in legally acceptable fund raising activities.”
- 4. Majibu ya TSSF Dhidi ya Tamko la Mhe. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako
4.1 Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutokutambua Taasisi ya TSSF
Shirika la TSSF halina mrejesho wa kusema dhidi ya tamko la Mhe. Waziri Ndalichako kuhusu yeye na wizara yake kutoitambua TSSF. Japokuwa TSSF imekwisha fanya jitihada mbalimbali za kujitambulisha kwa wizara hiyo bila ya kupata mrejesho wowote. Mnamo tarehe 01 Agosti 2017 saa 12:18 jioni, TSSF ilituma barua yake kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia email zifuatazo; ps@moe.go.tz na
info@moe.go.tz ambapo barua hiyo ya TSSF ilikuwa ni ya tarehe 31 Julai 2017 yenye Kumb. Na: TSSF/DG/16/2017/84/1 ambayo ilitumwa kwa wizara hiyo pamoja na Cheti cha Usajili wa Shirika la TSSF na Tangazo la Mwaliko wa Maombi ya Ufadhili wa Masomo ya elimu ya juu. Licha ya barua hiyo ya TSSF kuisihi Serikali kuchagiza mahusiano ya kikazi baina yake na TSSF lakini barua hiyo haikujibiwa mpaka tarehe ya kutolewa kwa taarifa hii. Kutokana na ukimya wa wizara ya elimu, Shirika la TSSF lisingeweza kuacha kutekeleza shughuli zake kwa sababu Shirika la TSSF haliwajibiki moja kwa moja kwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia bali linawajika kwa Msajili wa NGOs kwa kuwasilisha taarifa zake za kazi za kila mwaka na kulipa ada zake kwa Msajili wa NGOs pamoja na kujaza NGOA Fomu Na. 10 ambayo hujazwa kwa mujibu wa Kifungu cha 29 na 38 cha Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali Na. 24 ya Mwaka 2002.
4.2 Kuhusu Mhe. Ndalichako kutokuwa na Taarifa ya Mkutano wa TSSF na Taasisi za Elimu ya Juu wa tarehe 30 Novemba 2017 pamoja na yeye kutokuwa na Taarifa za Kuwa Mgeni Rasmi wa Mkutano huo.
Ni kweli kwamba, TSSF imepanga kuwa na mkutano na taasisi za elimu ya juu mnamo tarehe 30 Novemba 2017. Hata hivyo, katika matamshi ya TSSF kuhusu Mhe. Ndalichako kuwa Mgeni Rasmi wa Mkutano huo, TSSF ilisema kwamba Mhe. Ndalichako “anatarajiwa” na siyo “atakuwa” Mgeni Rasmi wa Mkutano huo.
- 5. Taarifa ya Wizara kwa Umma kuhusu TSSF
5.1 Kuhusu Taarifa za TSSF kutokuwa za Kweli
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia haiwezi kukanusha au kuthibitisha taarifa za TSSF kwa sababu, chanzo cha taarifa za TSSF ni TSSF yenyewe na siyo Wizara. Vilevile kwa Mujibu wa Katiba ya TSSF toleo la Mwaka 2014 Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia siyo Msemaji wa TSSF. Kwa hiyo mwenye mamlaka ya kuthibitisha au kukanusha taarifa za TSSF ni TSSF yenyewe na siyo mtu mwingine awaye yeyote.
5.2 Kuhusu Mkurugenzi Mkuu wa TSSF kutakiwa kufika katika Makao Makuu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia akiwa na Nyaraka zote za TSSF
Mkurugenzi Mkuu wa TSSF amepkea wito huo kwa mikono miwili japokuwa hajapokea barua ya wito wa kuitwa na wizara hiyo lakini atawasili kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Siku ya Jumanne ya terehe 14 Novemba 2017, Saa tatu kamili asubuhi akiwa na nyaraka zote muhimu kama alivyoagizwa.
- 6. Msimamo wa TSSF dhidi ya Huduma zake kwa Umma
Shirika la TSSF litaendelea kutoa huduma zake kwa umma kama kawaida ikiwa ni pamoja na kupokea maombi ya mikopo nafuu ya elimu mpaka tarehe 30 Novemba 2017. Vilevile Shirika la TSSF limesitisha kutoa barua za dhamana ambazo zilikuwa zikitumika kwa ajili kufanikisha usajili wa masomo kwa wanafunzi ambao ni wanufaika wa Mfuko wa Elimu ya Juu wa Shirika la TSSF ili waingie darasani na kuhudhuria mihadhara ya kitaaluma katika kipindi cha mwaka wa masomo 2017/2018 . TSSF imefanya hivyo ili kupata nafasi ya kushughulikia sintofahamu zilizojitokeza kati ya TSSF na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Aidha, Shirika linawaomba wale wote ambao wameomba mkopo nafuu wa elimu kutoka TSSF pamoja na wale waliokwisha kupata barua za dhamana na kufanya udahili vyuoni kuwa watulivu katika kipindi ambacho TSSF inapitia katika wakati mgumu mpaka pale taarifa nyingine itakapotolewa hapo baadae.
Imetolewa na:
Donati Primi Salla
MKURUGENZI MKUU
10 Novemba 2017
TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION
OFISI YA MKURUGENZI MKUU
TANGAZO
YAH: PUNGUZO LA ADA YA FOMU YA MAOMBI YA UFADHILI WA MASOMO YA ELIMU YA JUU KWA MWAKA 2017/2018
Hii ni kuutaarifu Umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba, baada ya kupokea maoni mbalimbali ya wadau kuhusu kushindwa kulipa ada ya maombi ya ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa mwaka 2017/2018 kutoka TSSF, na kwa kuzingatia agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kutaka kushushwa kwa bei za maombi ya huduma za elimu ya juu kwa wanafunzi, na kwa kuzingatia misingi ya falsafa ya Shirika la TSSF ambayo ni ‘kutoa msaada kwa jamii’, Shirika la TSSF limepunguza rasmi kiasi cha malipo ya ada ya fomu ya maombi ya ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kutoka TSSF ambapo ada hiyo imepunguzwa kutoka Tshs. 50,000/= hadi Tshs. 20,000/= kuanzia leo siku ya Jumatano ya tarehe 30 Agosti 2017.
Aidha, wale ambao walikuwa wameshalipia Tshs. 50,000/= watarejeshewa Tshs. 30,000/= na kwamba utaratibu wa kudai kurejeshewa malipo tajwa hapo juu utafanyika baada ya mdai kuwasiliana na Shirika la TSSF kupitia Na. 0624 700 666 au kutuma ujumbe wa barua pepe kwenda kwa anwani ifuatayo; registry@tssf.or.tz
Sanjari na hilo Shirika la TSSF linawakumbusha waombaji wa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwamba, mwisho wa kuomba ufadhili tajwa hapo juu ni tarehe 30 Septemba 2017.
Imetolewa na;
Donati Salla
MKURUGENZI MKUU – TSSF
30 Agosti 2017
TAASISI YA MSAADA WA KIJAMII TANZANIA
UANACHAMA WA TSSF
Kikao cha Tatu cha Bodi ya Utawala wa TSSF kilichoketi mnamo tarehe 12 Julai 2017 Jijini Dar es Salaam kimefuta Uanachama wa TSSF kwa watu ambao wameshindwa kutekeleza wajibu wao wa Kikatiba wa Mwanachama wa TSSF kwa Mujibu wa Katiba ya TSSF, 2014.
Majina ya Waliofutiwa Uanachama ni haya yafuatayo;
NA JINA JINSI ANAKOTOKEA
01 Abdulrahman Ameir Abdallah ME Mtwara
02 Abdulrahman Husein Kizulwa ME Tanga
03 Abel Ng’umbubhanu ME Singida
04 Adriana Leviwekuwisi KE Dar es Salaam
05 Adriana Molel KE Manyara
06 Alex Teu ME Dodoma
07 Ally Hemed Mngwali ME Dar es Salaam
08 Ally Swedi Ally ME Singida
09 Aloyce Mbuya ME Ruvuma
10 Anitha Bernad Masele KE Mtwara
11 Anna John Mallya KE Kilimanjaro
12 Asha Juma Salehe KE Mtwara
13 Ashura Abdallah KE Tabora
14 Aurelia Kamuzora KE Morogoro.
15 Benedict John ME Dodoma
16 Benedict Makatupula ME Katavi
17 Caroline Kamushanga KE Kagera
18 Deogratius Pisa ME Dar es Salaam
19 Dionis Mlela ME Rukwa
20 Eddah Mbuba KE Dar es Salaam
21 Edison John ME Mtwara
22 Eginald Mihanjo ME Dar es Salaam
23 Elinami Swai KE Dar es Salaam
24 Ezbon Oswald ME Mtwara
25 Fatma Said KE Pwani
26 Filbert Temba ME Dar es Salaam
27 Fortunatus Rwegoshora ME Kagera
28 Frateline Kashaga ME Dar es Salaam
29 Frida Fidelis KE Mtwara
30 Grace Mndali KE Tanga
31 Hadija Massare KE Pwani
32 Hamza Msola ME Dar es Salaam
33 Hanifa Mzee KE Dar es Salaam
34 Hassan Mtande ME Mtwara
35 Hidaya Ngozoma KE Mtwara
36 Ignatus Mponji ME Zanzibar
37 Jackson Julius ME Geita
38 Job Semboja ME Dar es Salaam
39 John Rite ME Mtwara
40 Joseph Karunze ME Njombe
41 Joseph Turuya ME Mwanza
42 Josephina Dallu ME Simiyu
23 Josiah Bethuel Kirundwa ME Kilimanjaro
24 Jovitha Mhagama KE Ruvuma
25 Juliana Aloyce Komu KE Dar es Salaam
26 Juliana Haule KE Dar es Salaam
27 Juliana Lekule KE Dar es Salaam
28 Juliana Mkeko KE Morogoro
29 Juma Bakari ME Arusha
30 Kokusiima Egla KE Dar es Salaam
31 Laurencia Mmole KE Lindi
32 Lilian Kiwango KE Lindi
33 Lilian Sawiya KE Dar es Salaam
34 Marry Julius Chacha KE Mara
35 Nuru Selemani ME Tanga
36 Paul David ME Mtwara
37 Paul Tarimo ME Mbeya
38 Paulo Aloisi ME Ruvuma
39 Peter Charles ME Morogoro
40 Peter Siriwa ME Dar es Salaam
41 Salum Kabenyeza ME Kigoma
42 Samson Suwi ME Mbeya
43 Scholarstica Mwageni ME Iringa
44 Shukuru Moses ME Dodoma
45 Silas Malima ME Mara
46 Straton Stephen ME Dar es Salaam
47 Tegemeo David ME Dar es Salaam
48 Tusubilege Benjamin KE Mbeya
49 Willavious Emmanuel ME Kilimanjaro
50 William Mchalo ME Dar es Salaam
Aidha Bodi ya Utawala wa TSSF imekataa Maombi ya Uanachama wa TSSF yaliyotoka kwa watu wafuatao kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya kudahiliwa katika Uanachama wa TSSF;
NA JINA ANAKOTOKEA
01 Abdallah Salim Makumbato ME Tanga
02 Abdul – halim Hammad Ali ME Zanzibar
03 Aden Fulgence Mapala ME Dar es Salaam
04 Agrey Mwatebela ME Mbeya
05 Ahlam Azzan KE Zanzibar
06 Ahman Kipogo Juma ME Zanzibar
07 Ahmed Mustafa Ramadhan ME Zanzibar
08 Ali Said Ali ME Zanzibar
09 Amon Chakushemeire ME Dar es Salaam
10 Daniel Lyimo ME Dar es Salaam
11 Daniel Massawe ME Kilimanjaro
12 Dkt. Luhanya Shadrack Luhigo ME Mwanza
13 Elineema Mchome ME Mtwara
14 Festus Amos Magembe ME Njombe
15 Frances Kato Mweyunge ME Kagera
16 George Julius Mkwaya ME Zanzibar
17 Haji Issa Rozzo ME Kigoma
18 Heriamen Manase ME Morogoro
19 Is-hak Kipogo Juma ME Zanzibar
20 Joseph Bureta ME Kilimanjaro
21 Juma Mohammadi Rashid ME Zanzibar
22 Kassim Hassan Ameir ME Zanzibar
23 Kevin Kevin Msuha ME Lindi
24 Luciana Mduma KE Dar es Salaam
25 Machano Ali Machano ME Zanzibar
26 Mariamu Michael KE Dar es Salaam
27 Mohamed Abdul-rabi Khamis ME Zanzibar
28 Mwajuma Ali Machano KE Zanzibar
29 Naima Abass KE Zanzibar
30 Noel Nguzo ME Dodoma
31 Omary Sefu ME Kilimanjaro
32 Peter David Kayanda ME Shinyanga
33 Sahia Hamis Suluhu KE Zanzibar
34 Selemani Nassoro ME Morogoro
35 Shaban Sizya ME Mwanza
36 Shadida Maliki Khatib KE Zanzibar
37 Silas Malima ME Mara
38 Sunday Hendry Nkwabi ME Dar es Salaam
39 Tabia Maulid Mwita KE Zanzibar
40 Twahili Athuman Kajugusi ME Mwanza
41 Vedas William Mabula ME Kilimanjaro
42 Willfredy Watambile ME Dodoma
43 Yusra Abeid Khamis KE Zanzibar
IMETOLEWA kwa MKONO WANGU leo Siku ya 13 ya Mwezi Julai 2017.
Donati Primi Salla
MRAJIS WA WANACHAMA
Nakala kwa:
- Msajili wa NGOs,
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
8 Barabara ya Kivukoni,
S.L.P 3448,
11486 DAR ES SALAAM.
TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION
OFFICE OF THE DIRECTOR GENERAL
REF: APPOINTMENT OF THE NEW DEPUTY DIRECTOR GENERAL
This is to inform all Members of the Tanzania Social Support Foundation and the general public that, the Governing Board of the Tanzania Social Support Foundation has appointed Mr. Ally Swedi Ally to be the Deputy Director General of the Tanzania Social Support Foundation with effect from this 05th day of February 2017.
Prior to this appointment, Mr. Ally Swedi Ally was the Interim Secretary General of the Teaching Society of Tanzania.
Mr. Ally Swedi Ally is a Teacher, Physicist and Mathematician by Profession and he is currently holding a Bachelor of Science with Education (Mathematics and Physics) from the Teofilo Kisanji University.
We are warmly welcoming him to the service of people of the United Republic of Tanzania through the Tanzania Social Support Foundation.
Issued by
SECRETARY TO THE TSSF GOVERNING BOARD
TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION
OFFICE OF THE DIRECTOR GENERAL
PUBLIC NOTICE
RE: 04th ANNIVERSARY OF THE TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION
This is to inform all the members, partners, and supporters of the Tanzania Social Support Foundation that, on 18th July 2015 the Tanzania Social Support Foundation shall commemorate the 04th Anniversary since its establishment.
You will recall that, Tanzania Social Support Foundation was established on 18th July 2011 and registered as a Non – Governmental Organization on 15th September 2011 followed by the change of its name and Constitution on 07th March 2014.
Recently, Tanzania Social Support Foundation has been offering its services and discharge its functions through the Directorate of Education and Directorate of Legal Aid Services.
In this anniversary, the Organization shall review its general conduct and improve where weaknesses shall be observed as well as introducing other new services in accordance to the legal framework of the Organization.
The Management of Tanzania Social Support Foundation wishes to thank each and every person who has contributed to achievements of the Organization whilst encouraging the progress of Unity, Solidarity, and participation among the members, partners, and supporters of the Organization.
Issued by
Donati Primi Salla
DIRECTOR GENERAL
SHIRIKA LA KUSAIDIA JAMII TANZANIA
OFISI YA MKURUGENZI MKUU
TANGAZO
Kutakuwepo na Kikao Cha I Cha Chama Cha Ualimu Tanzania – CUT, Kitakachofanyika Siku ya Jumapili ya Februari 08, 2015 Saa 08:00 Mchana hadi Saa 12:00 Jioni Katika Ofisi za Shirika la Kusaidia Jamii Tanzania – TSSF.
Kikao hiki kitafanyika Chini ya Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa TSSF na Watakaohudhuria ni Wale Wajumbe Waliopata Mwaliko Kutoka Katika Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa TSSF.
Imetolewa na;-
Mkurugenzi Mkuu – TSSF.
YAH: KUFUNGULIWA KWA SHUGHULI ZA TSSF RASMI KATIKA MWAKA 2015.
Uongozi wa Shirika la Kusaidia Jamii Tanzania (TSSF) unapenda kuwataarifu wateja wake, wananchi, na umma kwa ujumla kwamba, Shughuli za Shirika la TSSF zimefunguliwa kuanzia Januari 27, 2015 Mwaka huu. Hivyo basi, unaweza kutembelea ofisi za Shirika la TSSF zilizopo katika Ploti. Na.164, Barabara ya TANU Mkabala na Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali za Shirika letu.
Ofisi zipo wazi kila siku za Jumatatu - Ijumaa kuanzia Saa 08:00am - 5:00pm
na siku za Jumamosi kuanzia Saa 08:00am - 12:00pm
Kwa maelezo zaidi fungua tovuti yetu ambayo ni Http://www.tssf-org-tz.weebly.com
Imetolewa na
Ofisi ya Naibu Mkurugenzi Mkuu - TSSF.