TAARIFA KWA UMMA
YAH: TAMKO LA SHIRIKA LA TSSF DHIDI YA UNYANYASAJI WA KIUTU ALIOFANYIWA PROF. IBRAHIM LIPUMBA, MWENYEKITI WA TAIFA WA CUF, NA UKAWA
Shirika la Kusaidia Jamii Tanzania (Tanzania Social Support Foundation) linatoa tamko la kulaani vikali vitendo vya Jeshi la Polisi wa Tanzania vinavyofanyika kwa ajili ya kuwanyanyasa viongozi, wanachama, wafuasi, na wapenzi wa vyama vya upinzani hapa Tanzania.
TSSF inaamini kwamba vitendo hivi haramu vinavyofaywa na Jeshi la Polisi wa Tanzania, ni vitendo vya kuididimiza Demokrasia ya Tanzania na pia vitendo hivi havilengi kuitunza amani bali ni kuiharibu na kuipoteza kabisa.
Shirika la TSSF linaamini kwamba, Amani haipatikani kwa kunyanyasa na kuwatesa raia, wala amani haipatikani kwa matumizi ya mtutu isipokuwa kwa mazungumzo na kuheshimu Katiba ya Nchi pamoja na makubaliano yanayoafikiwa kati ya serikali na wananchi,au taasisi yeyote katika lengo la kuhakikisha kwamba maslahi ya Tanzania na Wananchi wake yanalindwa, kutetewa, na kupatikana wakati wote.
TSSF inaamini kwamba Jeshi la Polisi wa Tanzania lilikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa vitendo na vifungu vya katiba ya Tanzania ambavyo vimevunjwa ni kifungu cha 18, 20, na 21.
Shirika la TSSF linaitaka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanya mageuzi ya kimfumo katika uendeshaji wa shughuli za Jeshi la Polisi hapa Tanzania, kufanya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, na Sheria ya Makosa ya jinai ya mwaka 1985 ili kuvipa vyama vya siasa uhuru wa kufanya kazi zake bila ya kuingiliwa au kukandamizwa na serikali au chama kilichopo madarakani dhidi ya vyama vingine.
TSSF inawaomba wananchi, asasi za kiraia, na watu wote wenye mapenzi mema kuungana kwa pamoja kwa kupinga vitendo hivi haramu na kuhakikisha kwamba demokrasia ya Tanzania inakomaa.
Imetolewa;-
Uongozi
Shirika la TSSF.
Re: POSTPONEMENT OF AFRICAN YOUTH SUMMIT
Dear Brothers/Sisters
You will recall that, on February 22, 2014 the Management of Tanzania Social Support Foundation announced the great event in which the youths from all countries across Africa could have met at the Mwalimu Julius Kambarage Nyerere International Conference Center as African Youths Summit. The main agenda of the Summit was to make a critical discussion of African Development in Post 2015. It will also be remembered that, all these had to be conducted under the coordination of Tanzania Social Support Foundation.
That being the case, the aforesaid summit has been postponed until further notice in order to allow the Management of Tanzania Social Support Foundation proceeding with thorough preparations in respect of the aforesaid Summit.
The Management of Tanzania Social Support Foundation apologize for any inconveniences caused by this information, including the act of informing you about this postponement of the summit in late hours.
May you keep in touch with Tanzania Social Support Foundation.
Regards
The Management
Tanzania Social Support Foundation.
TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION
KURUGENZI YA ELIMU
TANGAZO
SHIRIKA LISILOKUWA LA KISERIKALI LA TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION KUPITIA KURUGENZI YAKE YA ELIMU LINAPENDA KUWATANGAZIA WANANCHI WOTE KWAMBA SASA SHIRIKA HILI LINATOA HUDUMA YA USHAURI (CONSULTANCY SERVICE) KATIKA SHUGHULI ZIFUATAZO;-
1. USHAURI KATIKA UANDISHI WA TAFITI (Research Writing Consultancy).
2. USHAURI KATIKA UANDISHI WA MIRADI YA MAENDELEO YA KIJAMII (Community Developmental Projects’ Writing).
3. USHAURI KATIKA UANDISHI WA WAZO LA KUANZISHA BIASHARA (Business Proposal Writing).
4. USHAURI KATIKA UANDISHI WA KATIBA, HATI ZA MAKUBALIANO, KANUNI ZA MIUNGANISHO YA WADHAMINI, PAMOJA NA NYARAKA MBALIMBALI ZA KUONGOZA TAASISI KAMA VILE NGOs, CBOs, FBOs, CSOs, SACCOS, VICOBA, MAKAMPUNI, VIKUNDI VIDOGO VIDOGO VYA UJASIRIAMALI NA WATU WANAOTAKA KUANZISHA MOJA YA TAASISI TAJWA HAPO JUU.
PIA SHIRIKA LINATOA HUDUMA YA USULUHISHI WA MIGOGORO INAYOTOKEA KWENYE TAASISI ZIFUATAZO;- NGOs, CBOs, FBOs, CSOs, SACCOS, VICOBA, WAMILIKI WA MAKAMPUNI, PAMOJA NA VIKUNDI VIDOGO VIDOGO VYA UJASIRIAMALI.
HUDUMA YA MAFUNZO YANAYOHUSU NAMNA YA KUSULUHISHA NA KUPATANISHA MIGOGORO MBALIMBALI INAYOTOKEA KWENYE NGOs, CBOs, FBOs, CSOs, SACCOS, VICOBA, MAKAMPUNI, VIKUNDI VIDOGO VIDOGO VYA UJASIRIAMALI NAYO INAPATIKANA IKIWA NI PAMOJA NA MAFUNZO YA UONGOZI NA UENDESHAJI WA NGOs, CBOs, FBOs, CSOs, SACCOS, VICOBA, MAKAMPUNI, NA VIKUNDI VIDOGO VIDOGO VYA UJASIRIAMALI.
SAFARI NA ZIARA RASMI ZENYE MALENGO MAHSUSI, ZA NDANI NA NJE YA NCHI KWA KIKUNDI CHA WATU, MTU BINAFSI, TAASISI N.K ZINAANDALIWA NA KUFANYIKA CHINI YA URATIBU WA SHIRIKA KUTOKANA NA MAOMBI YA WATEJA.
HUDUMA HIZI HUTOLEWA KWA BEI NAFUU.
KWA MAWASILIANO ZAIDI WAWEZA KUANDIKA KWA;-
MKURUGENZI MKUU,
TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION,
S.L.P 1328,
MTWARA
SIMU: +255 (0) 754 497 239.
AU FIKA KATIKA OFISI ZA KATIBU WA MBUNGE, JIMBO LA MTWARA MJINI ZILIZOPO KATIKA ENEO LA BIMA KARIBU NA OFISI ZA KAMPUNI YA DANGOTE.
NYOTE MNAKARIBISHWA!
Mr. JAPHES JOHNSTONE KATO TOOK THE OFFICE AS THE TSSF DEPUTY EXECUTIVE SECRETARY.
The Secretary General of Doli Foundation (Mr.Donati Salla) has met the STEMMUCSO Minister for Legal Affairs. for more report visit to http://www.dolifoundation.blogspot.com