Envaya

TANZANIA SOCIAL SUPPORT FOUNDATION
OFISI YA MKURUGENZI MKUU

TANGAZO
YAH: PUNGUZO LA ADA YA FOMU YA MAOMBI YA UFADHILI WA MASOMO YA ELIMU YA JUU KWA MWAKA 2017/2018


Hii ni kuutaarifu Umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba, baada ya kupokea maoni mbalimbali ya wadau kuhusu kushindwa kulipa ada ya maombi ya ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa mwaka 2017/2018 kutoka TSSF, na kwa kuzingatia agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kutaka kushushwa kwa bei za maombi ya huduma za elimu ya juu kwa wanafunzi, na kwa kuzingatia misingi ya falsafa ya Shirika la TSSF ambayo ni ‘kutoa msaada kwa jamii’, Shirika la TSSF limepunguza rasmi kiasi cha malipo ya ada ya fomu ya maombi ya ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kutoka TSSF ambapo ada hiyo imepunguzwa kutoka Tshs. 50,000/= hadi Tshs. 20,000/= kuanzia leo siku ya Jumatano ya tarehe 30 Agosti 2017.
Aidha, wale ambao walikuwa wameshalipia Tshs. 50,000/= watarejeshewa Tshs. 30,000/= na kwamba utaratibu wa kudai kurejeshewa malipo tajwa hapo juu utafanyika baada ya mdai kuwasiliana na Shirika la TSSF kupitia Na. 0624 700 666 au kutuma ujumbe wa barua pepe kwenda kwa anwani ifuatayo; registry@tssf.or.tz
Sanjari na hilo Shirika la TSSF linawakumbusha waombaji wa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwamba, mwisho wa kuomba ufadhili tajwa hapo juu ni tarehe 30 Septemba 2017.
Imetolewa na;


Donati Salla
MKURUGENZI MKUU – TSSF
30 Agosti 2017

August 31, 2017
« Previous Next »

Comments (24)

Erick Bihemo (Kibondo-Kigoma) said:
Tungepewa muongozo wa utoaji wa ufadhili. Zipo kozi zinazochukua miaka mingi Je nazo zina ufadhili. Vipaumbele ni vipi? Fomu na maelekezo mengine tunayapata wapi?
September 5, 2017
Bugota,Boniface venance (Tabora) said:
Ningependa kuuliza jinsi ya kuomba mkopo
October 22, 2017
ESAU J MANYELEZI (ILALA/VINGUNGUTI/DAR ES SALAAM) said:
mimi nimekosa mkopo loans body nilimaliza form six 2016 nikakosa mkopo hivyo nikashindwa kuendelea na masomo nikaahilisha mwaka na mwaka huu nimekosa na nilikuwa sijui kama kuna sehemu naweza kupata mkopo zaidi ya loans body lakini juzi trh 21/10/2017 nimepata taarifa yenu ya kutoa mkopo naomba msaada wenu nipate mkopo ili nami niendelee na masomo maana natoka ktk familia maskini sana hivyo haiwezi kumudu gharama za chuo kwani wazazi wangu niwakulima wadogowadogo,wapo dodoma vijijini hapa ninapokaa kwa sasa nimehifadhiwa kwa mda mfupi naamini elimu pekee ndio mkombozi wa maisha yangu form 4 index number ni P1156/0261/2014 na phone number 0714396329,please naomba msaada wenu nimechaguliwa chuo cha TIA dar es salaam kozi accounts.Ntashukuru kama ombi langu litafanyiwa kazi.ASANTE.
October 23, 2017
SHIJA LUHEGA BULUGU (MWANZA TANZANIA) said:
Mie naitwa shija luhega bulugu, kutoka mwanza tanzania, ndugu zangu namshuru mwenzi mungu kwa uwepo wa TSSF kwaajiri ya mimi na wale wenzangu wenye hali duni ya maisha lakini tukiungana na wale wenye navyo kulijenga taifa letu katika kuleta maendeleo kiujumla, ila tu twaitaji tumaini la TSSF katika kutuona kwa macho yake mawili (huruma) tunateseka kwa roho na mwili kutimiza hasa malengo yetu, shukrani za dhati ni kwa serikali iliopo madarakani kwa kulitizama jukwaa la wanyongo walio wengi ndani ya nchi yetu tanzania, Mungu ibariki tanzania Mungu wabariki wanataifa wote wa nchi ya tanzania.
Tusaidieni kwa lengo la maendeleo ya watu ote tu.
Ahsante sana.
October 24, 2017
SAIDI .A. JALUO (MTWARA TANZANIA) said:
Nimechaguliwa UDSM COMPUSS ya (MUCE) Bachelor of science with education 2017/2018 lakini cjapata mkopo kwa awamu zote mbili je naweza fanya maombi pia sina mdhamini wa kunidhamini je mnanisaidiaje kupata mkopo kwenu Namba yangu ya simu ni 0715854703 naomba msaada wenu.
October 27, 2017
Maria Manonga (Dar es salaam) said:
Naitwa Maria Manonga nimechaguliwa chuo cha maji ubungo katika kozi ya water quality laboratory technology, nimekosa mkopo kwenye bodi ya mikopo ya The registered trustees of water technicians fund. Naomba kusaidiwa kupata mkopo ili niweze kupata elimu yangu kama wenzangu kwani wazazi wangu hawana uwezo wa kunisomesha na hawajui umuhimu wa elimu.
October 28, 2017
Ezekiel (Dodoma) said:
naitwa Ezekiel msese ni continue student at st.John's university of Tanzania katika coz ya medical laboratory mimi familia yangu ni duni imeshindwa kuendelea kunisomesha naomba msaada wenu niweze kufanikisha ndoto zangu
October 30, 2017
(Anonymous) said:
Naitwa Mary Coster Mnyipembulo, nimechaguliwa katika chuo cha Hurbet Kairuki Memorial University katika kozi ya Medical Doctor ,nimetuma barua yangu ya kuomba mkopo tarehe 25/10/2017 . Chuo tayari kimeshafunguliwa , ada pamoja michango ni gharama sana. Mimi ni yatima ,nashidwa kukidhi gharama za chuo. Nauliza ni lini mtatoa majina ya waliopata mkopo . Namba yangu ni +255764871230.
Asanteni.
October 31, 2017
JUSTINE F OMBELA (GEITA VIJIJINI) said:
nilisply mkopo kwenu tssf katika facult ya environmental science huko sua. ama kweli nikiupata ninyi mtakua ni mungu wangu wa pili maana sina msaada wa aina yoyote japo naonekana kupendeza machoni pa watu mama na babaa wote ni maskini sanaa naa hawana njia yoyote ya kuweza kunisapoti mimi katika masomo japo nina ufaulu mzuri w3a kidato cha sita jina la bwana lihimidiwe. 0746780382 hiyo ndio namba yangu ya simu
November 1, 2017
T Z J (DAR ES SALAAM) said:
TSSF mkumbuke vyuo vimeshafunguliwa na huwezi kuripoti chuoni bila kulipa school fees na mambo mengine wanayohitaji kuyalipia sasa nawauliza ni lini mtatoa hayo majina kwa wale walioomba awamu ya mwisho ambapo mnadai deadline ni tar 30 November???? Hamuoni mtawapoteza wateja wenu ambao wanasubiria hiyo mikopo maana yake watashindwa kuripoti vyuoni jamani jitahidi kuharakisha utoaji wa hiyo mikopo ili kuwaweka wateja wenu katika mazingira salama na mimi nikiwa miongoni mwa hao tunaosubiria majina ya watakaopata mikopo
November 1, 2017
Sylvia Urio (Mbeya) said:
Naomba kujua taratibu wa kujaza fomu za mkopo
November 2, 2017
ancelemi chrispeneda (dar es salaama) said:
je muda wa kuomba umeisha au bado maana taarifa hii nimepata leo na nina hitaji
November 2, 2017
kibona denis (songwe) said:
naomba msaada wa mkopo kutoka tssf sijapata mkopo kutoka heslb namba yangu ya simu ni 0762100232,pia naomba kujua namna gani ntapata form ya tssf.
November 2, 2017 (edited November 2, 2017)
Octavian A. Temba (Moshi ( R )) said:
Asante sana kwa huduma hii . hakika itawasaidia wanyonge. Je, kwa wale ambao ndiyo tumelisoma tangazo hili na tuna shida ya mikopo , tutaruhusiwa kujaza fomu za kuomba? simu namba 0754399602
November 3, 2017
Yassin Yunusi (Tanga) said:
Tunaombeni msaada wenu kwani mpaka sasa sifahamu kama nitaendelea na masomo
November 3, 2017
Maulid Sadala (Dar es salaam) said:
naitaji maelezo namna ya kupata iyo fomu 0716 161677
November 3, 2017
issa b mnand (mabibo) said:
deadline lin na vgezo ni vp, mm npo mwaka wa pili vp naweza kuomba call 0713107572
November 3, 2017
Kenneth kessy (Dodoma town) said:
Naomba kuuliza kuwa inawezekana kwa sasa hivi kuendelea kutuma maombi baada ya ile mara ya kwanza kufunga maana wengine tulikosa kuomba na kama nafasi hizo zipo naomba tufahamishwe kwa kuandika kwenye page yenu. Call 0717872654
November 4, 2017 (edited November 4, 2017)
Ezekiel (Dodoma) said:
tunaomba kujua majibu mnatoa lini huku vyuoni tunakaribia kufukuzwa tunaomba msaada wenu
November 7, 2017
dasco kapyela (mbeya-tanzania) said:
nahitaji kujua je kwa wale tulioomba mkopo ajibu tutapokea lini

namba 0767753852
November 7, 2017
ashely abel (dar es salaam) said:
samahani Mimi ningeomba mnijuze tulioomba mkopo majibu yanatokaa lini 0752252240
November 9, 2017
KENFRID GAITAN (MOROGORO) said:
Habar Mimi naitwa KENFRID GAITAN ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza JORDAN UNIVERSITY COLLEGE tawi la SAUT kilichopo morogoro kwa kozi BAED nimekosa mkopo wa heslb nimechelewa kupata taarfa ya mkopo toka kwenu TSSF nimepa tarhe 7/december,,,,?Je kwa sisi tuliochelewa na Deadline mliyoitoa ishapita JE mtatusaidia vipi asa sisi tutokao familia za kimasikini,,,,?Namba ya simu 0716889098 na namba ya Form4=P2517/0697/2015,,,?pia namba ya usajili wa chuo ni 2017/0176,,,?Tunaomba m2saidie jamani
December 7, 2017 (edited December 7, 2017)
HELEN BENJAMIN (DUBAI) said:
TAFUTA MFARASHAJI WA MCHANGO

Tatua Tatizo lako la Fedha Ndani ya Masaa 24.

             Je, wewe ni Mmiliki wa Mshahara au Biashara?
      Pata kutoka kwa Euro 1,000 - 200,000, 000 Euro Mikopo ndani ya masaa 24

               Suluhisho la Fedha Rahisi.

Kwa Maswali zaidi wasiliana nasi kwa: immaculateloanprovidersltd@gmail.com
Mkurugenzi Mtendaji: Bibi Benjamine
au tembelea tawi letu: Level 29, Tiffany Tower, Jumeirah Lakes Towers Dubai. UAE


Wasiliana nasi kwa: immaculateloanprovidersltd@gmail.com

                              Asante
November 12, 2018
HELEN BENJAMIN (DUBAI) said:
TAFUTA MFARASHAJI WA MCHANGO

Tatua Tatizo lako la Fedha Ndani ya Masaa 24.

             Je, wewe ni Mmiliki wa Mshahara au Biashara?
      Pata kutoka kwa Euro 1,000 - 200,000, 000 Euro Mikopo ndani ya masaa 24

               Suluhisho la Fedha Rahisi.

Kwa Maswali zaidi wasiliana nasi kwa: immaculateloanprovidersltd@gmail.com
Mkurugenzi Mtendaji: Bibi Benjamine
au tembelea tawi letu: Level 29, Tiffany Tower, Jumeirah Lakes Towers Dubai. UAE


Wasiliana nasi kwa: immaculateloanprovidersltd@gmail.com

                              Asante
November 12, 2018

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.