Envaya

Mafunzo ya kuimarisha uwezo wa wanawake viongozi  Wilaya ya Mbozi kaza za Ichenjezia, Nyambili, Iyula, Isanza, Ipunga, Ihanda, Mlowo, Ruanda na Isandula. Kwa Ruzuku kutoka women Fund Tanzania.

 

June Mwaka 2016,Mpalano CDO kwa ruzuku kutoka Women Fund Tanzania (WFT) ilitekeleza mradi wa Kuwajengea uwezo Wanawake na Wasichana ili kukuza haki zao za kiuchumi na kisiasa Wilaya ya Mbozi, Songwe, Tanzania. Mradi huu uliwawezesha viongozi wanawake wa kuchaguliwa na wa vikundi vya kijamii wakiwemo wasanii kukuza sauti zao katika katika vyombo vya maamuzi. Vyombo hivyo ni pamoja na mahali wanapofanyia shughuli zao za kiuchumi na katika ngazi ya vijiji, mitaa na kata ili kuwa na ufanisi katika kuwasilisha na kuwakilisha sauti za wasichana na wanawake katika kudai haki kwenye ngazi husika za maamuzi katika wilaya ya Mbozi, mkoa mpya wa Songwe. Pichani ni sehemu ya washiriki  wa mafunzo hayo. Washiriki wanatoka katika kata 9 za Wilaya ya Mbozi: Ichenjezia, Nyambili, Iyula, Isanza, Ipunga, Ihanda, Mlowo, Ruanda na Isandula.

UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA

La Mgambo limelia…

Kesho Jumamosi tarehe Novemba 22, saa mbili mpaka saa tatu asubihi, siku moja kabla ya kuanza zoezi la kuandikisha orodha ya wapiga kura,  Mratibu wa Asasi ya Mpalano CDO, ataruka live katika kipindi cha TUWEKANE SAWA Cha redio ya Ushindi FM 98.6 ya mjini Mbeya, kufafanua masuala mbali mbali kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Desemba 14, mwaka huu.

Usikose fursa hii adhimu ili kujijengea uelewa wa masuala mbali mbali yanayohusu uchaguzi huu ikiwa ni pamoja na Uandikishaji kwenye orodha ya wapiga kura, kuhakiki majina na hatua za kuchukua ikiwa jina lako halipo ama limekaa sivyo ndivyo; uteuzi wa wagombea, kuweka pingamizi dhidi ya mgombea, kampeni na utaratibu wa upigaji kura.

Wote mnakaribishwa.

Bonyeza HAPA kusikiliza tangazo la hamasa

DESEMBA 14, 2014-

UCHAGUZI NGAZI ZA CHINI ZA SERIKALI ZA MITAA

 "Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 (kwa Mamlakaza Wilaya) na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288 (kwaMamlaka za Miji) zinaelekeza kuwa Uchaguzi wa Viongozi wa Mitaa, Vijijina Vitongoji hufanyika klabaada ya miaka mitano (5).

Kwa mwaka 2014, uchaguziwa Wenyeviti wa Vijiji, Vitongoji, Mitaa;Wajumbe wa Halmashauri zaVijiji, na Wajumbe wa Kamati za Mitaautafanyika nchini kote tarehe14Desemba,2014kama ilivyotangazwanaWaziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa tarehe 2 Septemba, 2014.

Katikakufanya maandalizi ya uchaguzi huo shughuli mbalimbali zamaandalizi zimefanyika na zinaendelea kufanyika ili kufikia hatuambalimbali za ukamilishaji." Kutoka website ya TAMISEMI.

 Soma Ratiba ya mchakato HAPA au na kusoma au kujipakulia Kanuni za uchaguzi, Mipaka ya mitaa na vijiji kwa ajili ya uchaguzi huu bonyeza HAPA.

Nyumba Imara ina Msingi Imara.

Uongozi Bora ktk Vijiji na Mitaa ndiyo msingi wa kustawi kwa Demokrasia na Maendeleo nchini. JISHIRIKISHE

large.jpg

Sehemu ya mandhari ya Mto Mbaka unaoanzia kama chemchemi za Mlima Rungwe wilaya Rungwe na kutiririsha maji yake katika Ziwa Nyasa. Pongezi kwa Serikali na wakazi wa wilaya za Rungwe na Kyela kwa kuyatunza Mazingira yanayozunguka mto huo. Jitihada zaidi zinahitajika kuendelea kuhifadhi utajiri huu maridhawa. Picha na Adam Gwankaja.

large.jpg

AMANDONGOMILO: Matunda mwitu, katika wilaya za Kyela na Rungwe. Hayaliwi sana, lakini huaminika kuwa na madini ya chuma kwa kiwango kikubwa. Vijana hutumia matunda haya kutega ndege.

large.jpg

AMANGULUNGULU- Matunda pori maarufu katika wilaya za Kyela na Rungwe. Yakikomaa na kuiva tayari kwa kuliwa hubadilika rangi na kuwa kahawia. Kutokana na uharibifu wa mazingira, MANGULUNGULU ni miongoni mwa matunda yanayoweza kutoweka kabisa. Picha na Adam Gwankaja

large.jpg

Baadhi ya Wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Mpalano CDO

large.jpg

Mratibu wa Miradi wa Mpalano CDO, Ndugu Edson akitoa taarifa ya zoezi la kubainisha hali halisi ya shughuli za kitamaduni katika wilaya za Kyela na Rungwe, Mbeya Tanzania.